Hapa sasa tunaona Ibrahimu ambavyo alikuwa anawashawishi malaika waliotumwa na Mungu kwa ajili ya kuiangamiza Sodoma na Gomora. Mwanzo18:32. “Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu wala hutaacha mji.Hasha usifanye hivyo,…BWANA akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha kwa ajili yao.”
Ibrahimu aliendelea kusema na wale malaika mpaka akafikia hesabu ya watu 10! Na ibrahimu akaishia hapo, kama Ibrahimu angeendelea kusihi bila shaka maangamizo yasingetokea. (Mwa 18:30-32). Zaidi sana walichokifanya malaika ni kumuondoa Lutu na mkewe na wanawe ambao inaonyesha hawakufika 10 kama wangekuwa 10 wasingetolewa ili mji uangamizwe kwa sababu Ibra alifanya maombi na yakajibiwa kwamba kwa idadi ya watu 10 tu na kama hao 10 wangekuwepo Sodoma na Gomora isingeangamizwa, wangeachwa na Mungu angetumia njia nyingine! Maana Alisema kama wamgekuwa 10 asingeuangamiza mji.
Michael Othiniel
July 11, 2020 at 11:12 am
MUNGU awabariki ninawafuatilia kwa ukaribu. Nabarikiwa na uchambuzi sahihi wa masomo yenu katika neno (YESU KRISTO)
Anonymous
July 11, 2020 at 11:13 am
Asante