RSS

Juu ya Huduma yangu.

Naitwa David Stamen. Mimi ni Mwingereza. Naishi hapa Uingereza. Kwa mara ya kwanza nilikuja Tanzania mwaka 1991. Nilikaribishwa kuhubiri na kufundisha semina katika makanisa huko mkoani Iringa na tokea hapo nimekuwa nikija Tanzania mara moja au mbili kwa mwaka nikihubiri pamoja na kufundisha Injili ya Bwana Yesu pamoja na kusaidia kazi ya Bwana makanisani. Nafanya kazi hasa katika mkoa wa Morogoro na nategemea kuanzisha huduma huko Dar Es Salaam. Ninafundisha na kufanya semina kwa wachungaji, viongozi na watumishi wengine wa Mungu, pamoja na vijana na wanafunzi mashuleni. Huduma hii imefika hadi katika makanisa ya maeneo ya Wamaasai. Katika kufanya kazi hii siwakilishi chama chochote wala shirika au hata dhehebu kutoka hapa Uingereza. Isipokuwa nilijiunga na waumini waliopo mkoa wa Morogoro na hapo kwa sasa ndio makao yangu makuu kihuduma. Lakini nafanya kazi ya Mungu pamoja na waumini wa kweli mahali po pote ninapokaribishwa hapo Tanzania. Najua  moyoni wangu kuwa Mungu ameniongoza kufanya kazi hii hapo Tanzania ninao moyo na wito wa kumtumikia Bwana Yesu huko Tanzania kwa kadiri ya neema yake. Huwa sitozi pesa wala sitafuti pesa yoyote kwa huduma hii. Najitoa bure tu kwa ajili ya kazi ya Bwana. Zaidi ya hayo yote ninawasaidia makanisa na waumini kwa mahitaji mengine, kama yatima na wajane.

Kama umebarikiwa kwa kusoma au kusikiliza jumbe kupitia tovuti yangu, ‘somabiblia.com’, na unapenda kunikaribisha kwa ajili ya mafundisho ya Biblia, unaweza kuniandikia kwa email yangu: dsta12@hotmail.co.uk   au unaweza kunipata kwenye facebook na jina David Stamen.

Hapo chini, nipo Dumila kwenye nyumba ya mtafsiri wangu.

David Stamen

Nafurahi sana kuwepo pamoja na washirika porini na kuhubiri Injili! Mimi na mtafsiri wangu huko Mororoi, karibu na Dumila.

IMG_0053

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Niliwasaidia waumini wa Mororoi kujenga jengo lingine (hapo chini).

jonny 235

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Nilihemishiwa kulala katika nyumba ya asili. Nimefanya hivyo mara nyingi!

Feb. 2013 057

 

 

DSC00817

 

jonny 167

Tuliwasaidia waumini maskini wakati wa njaa. Na ninawasaidia wajane na yatima.

sembe distribution 014

DSC00878

Nilifundisha kwenye semina ya CASFETA huko Morogoro. Wanafunzi wa shule ya sekondari na chuo kikuu.

DSC01939

Hapo chini tunaona vyoo bila milango kwa ajili ya wanafunzi 500 wa shule ya msingi huko Gairo. Niliwahurumia sana!

DSC02008

Niliwasaidia wapate milango. Walifurahi saaaana!

IMG_0137

 

Zaidi ya hayo tunahubiri Habari Njema ya Yesu Kristo!    

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kanisa huko Gairo. Ninawatembelea kila mwaka pia. (Hapo chini)

Tanz.2010 028

Haya kwa ufupi tu! Ni baraka kwangu na furaha yangu kumtumika Bwana Yesu hapo Tanzania,

M8

RUDI KWA HOMEPAGE

 

65 responses to “Juu ya Huduma yangu.

  1. Elly chacha

    October 21, 2019 at 12:40 pm

    Ndg karibu mwakitolyo no-5 shinyanga mimi ni mchungaji nimependa huduma yako karibu katika huduma ya Kristo

     
  2. Evance Fredrick Ndyetabura

    April 4, 2022 at 7:09 am

    Thanks, nimesoma huu mtandoa na kwangu naoni ni neema za Mungu kwa Ndugu yetu na rafiki yetu David Stamen. Nimefurahi Sana. Mungu akibariki nitajiunga nanyi katika mission.
    MUNGU AWABARIKI

     
    • dsta12

      April 15, 2022 at 12:37 pm

      Asante sana.

       
  3. Mwalimu Arigumaho Johnpaul

    April 21, 2022 at 4:43 am

    Karibu pia Uganda, tunahitaji kujishughulisha na mtu wa moyo mkunjufu Kama wewe… ASANTE sana…baraka za mungu NAKUTAKIA 🙏🙏🙏🙏

     
  4. Tainos Ngailo

    April 21, 2022 at 12:58 pm

    Ubarikiwe mtumishi wa Mungu,hakika umeitwa na Mungu,wengine baadhi huwa watumishi wa madhehebu yao badala ya Mungu!

     
  5. Anonymous

    May 20, 2022 at 12:11 pm

    Bwana yesu asifiwe natwa mchungaji frank erasto nachunga kanisa la TAG nipo mabwerebwere mahar ambapo pana uislam mpaka walichoma kanisa moto mpaka sasa bado sijapata jengo la kudum mungu akubari sana kama utaguswa ututembelee mabwerebwere AMINAno

     

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: