Tabia ya Maji ya Uzima
Maji hutiririka na kutafuta mahali pa chini kabisa. Maji hushuka mpaka hayawezi kushuka zaidi.
Je, tunapenda kubarikiwa? Je, tunataka kujawza na Roho Mtakatifu? Imeandikwa, “Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema. Basi nyenyekeeni chini…” (1 Petro 5:5,6). Kuhusu Yesu Kristo imeandikwa, “ alipotukanwa, hakurudisha matukano.” (1 Petro 2:23). Je, tunayo tabia na nia ya namna hiyo? Je, kama mtu mwingine akikushambulia kwa maneno bila sababu ya haki, je, unajisikia unayo haki kumdharau na kumshambulia pia? Au kama maji yanavyotafuta njia nyingine, wewe pia umejifunza kwamba, “Jawabu la upole hugeuza ghadhabu.” (Mith.15:1). Jihadhari, wengi – kwa sababu wanafikiri haki ipo upande wao, wanajiruhusu kutumia maneno makali na kuwadharau wengine. Hata kama haki ikiwa upande wetu, siyo sababu kuacha tabia na nia ya Yesu Kristo katika mazungumzo yetu na wengine, siyo sababu tujiinue juu ya wengine. “Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu…ambaye alijifanya kuwa hana utukufu na alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti ya msalaba.” (Wafil.2:5-8). Je, unahitaji sana tena sana uwe na haki katika mazungumzo yote na majadiliano yote na wengine? Je, ni hitaji kubwa la tabia yako kushinda kila jadiliano na wengine? Faida ya ujuzi ni nini? “Ujuzi huleta majivuno, bali upendo hujenga.” (1 Wakor.8:1). Ujuzi wetu siyo sababu tujiinue juu ya wengine na kuwakemea kama wangekuwa wajinga. Ipo njia nyingine, “Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo.” (Waefeso 4:15). Haya pamoja na, “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.” (Wakol.4:6). Ndiyo, tuhubiri Injili ya Yesu Kristo kwa hodari; tutangaze Ukweli kwa wazi, bila kuwaogopa watu, bila kutafuta kuwapendeza watu, lakini inaleta faida tu kama tukifanya hivyo sawasawa nia na tabia ya Yesu Kristo aliyejinyenyekeza!
Maji siyo kama mawe, siyo ndiyo jamani? Maji hayawezi kukujeruhi. Kama maji yanakutana na jiwe, maji hayapigani na jiwe – yanaendelea kutiririka mbele tu na kuzunguka mkingamo kwa urahisi bila kubadilisha tabia yake! Tabia yake ni ‘laini’ na upole – ni kama Upendo ambao “huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo haujivuni; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya.” (1 Wakor.13:4,5). Wengine wanaweza kuonekana watu wazuri sana – mpaka watakapochukizwa na kitu au mtu fulani, ndipo jihadhari! Wanabadilika kwa ghafula! Paka anaweza kujionyesha awe upole na mwenye urafiki – huoni makucha! Lakini mara moja paka atakapochukizwa au kukasirika, utaona makucha na atakuumiza! Upole na urafiki zimetoweka kwa ghafla. Yakobo anatuonya, “Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.” (3:10). Lakini maji ya uzima ni kama “hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.” (Yak.3:17). Bwana asifiwe! Hakuna Mwingine kama Yesu! Tunampenda kwa sababu Yeye ni tofauti na watu wote; tunampenda kwa ajili ya tabia Yake! Yeye ni Mwana wa Mungu! Na Yeye alikufa ili kutupa maji ya Uzima yawe ndani yetu! (Yoh.7:38).
Maji yanatiririka tiririka kutafuta tafuta mahali pa chini kabisa! Maji yanatelemka telemka kabisa mpaka hayawezi kushuka zaidi! Mahali hapo hapo yapo maji mengi! Kama ilivyo bondeni! Maji ya uzima mengi – kila wakati! Mahali pa juu sana labda itanyesha mvua pale lakini patakauka kwa haraka. Bali mahali pa chini kabisa pana maji mengi wakati wote – maji ya uzima!
Roho ya shetani inasema, “Nitapanda JUU hadi mbinguni, nitakiinua kiti changu cha enzi JUU ya nyota za Mungu, nitaketi nimetawazwa JUU ya mlima wa kusanyiko, kwenye vimo vya JUU sana vya mlima Mtakatifu.” (isaya 14:13,14).
Yesu Kristo anasema, “Njoni kwangu…Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.” (Matayo 11:29).
Watu wanaoishi ‘mahali pa chini’ hawachukizwi na wengine, hawadharau wengine kwa sababu wanaishi na Yule amabye “hutujalia sisi neema iliyozidi.” (Yakobo 4:6). Kama ukitaka kupanda juu au kujiinua (kama mlima) juu ya wengine, ujue, “Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.” Tupo wapi? Tunaishi wapi?
Ujue, “Kila bonde litajazwa / litainuliwa, kila mlima na kilima kitashushwa…” (Luka 3:5; Isaya 40:4).
Lazima tuchague. Tunaweza kuihishi naye aliyesema,
“Kwa maana hili ndilo asemalo aliye juu, Yeye aliyeinuliwa sana, Yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: ‘Ninaishi mimi mahali palipoinuka tena palipo patakatifu, tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na mwenye roho ya unyenyekevu, ili kuhuisha roho za wanyenyekevu…” (Isaya 57:15).
“Mtu huyu ndiye ninayemthamini: Yeye ambaye ni mnyenyekevu na mwenye roho yenye toba atetemekaye asikiapo neno langu.” (Isaya 66:2).
Kuishi ya nama hiyo, tutabarikiwa sana na tutakuwa baraka kwa wengine! Tutakuwa “manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea.” (Wakor.2:15). Mungu apewe sifa sana kwa neema Yake kuu!
© David Stamen 2015
Kupakua ujumbe huo, bonyeza link hiyo: Tabia ya Maji ya Uzima
tumsifu mmari
June 12, 2015 at 10:06 pm
Huduma hii tunayofanya ni ya kristo hivyo tunapwaswa kunyenyekea san kibur ni ushindi kwa shetani