RSS

This slideshow requires JavaScript.

Karibu somabiblia.  Naitwa David Stamen. Hapa unaweza kusikiliza na kusoma jumbe juu ya mafundisho ya Biblia. Pia unaweza kupakua Biblia, kamusi, hadithi na nyimbo kwa Kiswahili, Kiingereza na kimaasai. Yote ni bure. Kusoma  juu ya huduma yangu bonyeza llink ifuatayoHUDUMA YANGU ]  

(FOR THIS PAGE IN ENGLISH: CLICK HERE)

MAPYA KABISA: Bofya somo tu.

VIRUSI VYA KORONA KATIKA MUKTADHA WA KIBIBLIA. MAJANGA YA ASILI NA JINSI YA KUYATAFSIRI.

THE CORONA VIRUS IN BIBLICAL CONTEXT. HOW TO INTERPRET NATURAL DISASTERS.

MASOMO ]  [ JUMBE ZA KUSIKILIZA ] 

[ BIBLIA NA KAMUSI ]  [ HADITHI NA NYIMBO ]

ARTICLES IN ENGLISH

VIDEO: FEDHA YAKO NA IPOTELEE MBALI PAMOJA NAWE!

NIFUATE KWENYE FACEBOOK. UTAPATA MASOMO MAPYA MARA YATAKAPOANDIKWA.

—————————————————-
MAPYA: SEMINA YA VIJANA YA SIKU TANO JUU YA UTAKASO. 2018 DAR ES SALAAM

 1. UTAKASO. SEHEMU 1. SHOKA LIMEKWISHA KUWEKWA PENYE MASHINA.
 2. UTAKASO. SEHEMU 2. MWANAKONDOO AIONDOAYE DHAMBI YA ULIMWENGU.
 3. UTAKASO. SEHEMU 3. NAJITAKASA MWENYEWE.
 4. UTAKASO. SEHEMU 4. MSIUPENDE ULIMWENGU.
 5. UTAKASO. SEHEMU YA 5. KUISHI KWA NENO LA MUNGU

JUU YA HALI YA MAKANISA SIKU HIZI NA WAANDISHI MBALIMBALI  (HAPO CHINI):

 1. KANISA NI NINI?  David Stamen
 2. TURUDI TENA KWENYE KUMHUBIRI KRISTO.   Mch. Carlos Ricky Wilson Kirimbai
 3. INJILI YA MAFANIKIO INAVYOLIANGAMIZA TAIFA   Jackson Malugu (Mhariri wa Mwanzonews)
 4. ‘SIKUTAMANI FEDHA WALA DHAHABU, WALA MAVAZI YA MTU’  Mch. Gasper Madumla
 5. MIMI NAPATA SHIDA SANA. MUNGU TU ANIREHEMU KAMA NAKOSEA. Mch. C.R.W. Kirimbai

MASOMO YAPENDEKAYO YA KUSOMA:

 1. MAMBO YA ZAKA, UTOAJI, SADAKA, FUNGU LA KUMI NA PESA     
 2. VITA VYA KIROHO NA JINSI YA KUOMBA 
 3. MAFUNDISHO JUU YA LAANA
 4. VITA VYA KIROHO NA KUOMBA KWELI KWELI.
 5. TUKUSANYIKE SIKU GANI KATI YA JUMAMOSI NA JUMAPILI?
 6. SABABU YA UMASKINI NA UFUKARA NI NINI?
 7. JE, UNATAFUTA NDOTO ZAKO AU MAPENZI YA MUNGU?
 8. SIRI YA MAFANIKIO – YESU HAKUWA MOTIVATIONAL SPEAKER
 9. MAAGANO YA MUNGU
 10. UZIMA WA MILELE NI NINI? INJILI NI NINI?
 11. HILA NA MBINU ZA SHETANI NA JINSI YA KUZISHINDA. VITA VYA KIROHO KWELI KWELI.

 MASOMO NYINGINE YOTE: BOFYA HAPA

JUMBE ZIPENDEKAZO ZA KUSIKILZA (AUDIO):

 1. UFALME WA MUNGU 1: SHOKA LIMEKWISHA KUWEKWA MIZIZI
 2. UFALME WA MUNGU 2:  KUFANYWA KIUMBE KIPYA – KUFANYWA HAKI YA MUNGU!
 3. YESU ANATOSHA / UNATAKA NINI: SEMINA YA CASFETA
 4. YESU NI NJIA: SEMINA YA CASFETA
 5. USIZOELEE KUWA MKRISTO
 6. ENENDA ZAKO WALA USITENDE DHAMBI TENA
 7. UONGOZI NA WAHUBIRI WA KWELI
 8. CHANGAMOTO KWA VIJANA NA KWA WOTE
 9. SISI TU MANUKATO YA KRISTO
 10. MAFUNDISHO JUU YA MAOMBI

 JUMBE (AUDIO) ZOTE: BONYEZA HAPA

                       BIBLIA NA KAMUSI

 1. BIBLIA KWA KISWAHILI NA KIINGEREZA: DOWNLOAD
 2. DOWNLOAD KAMUSI / DICTIONARIES
 3. DOWNLOAD KIMAASAI AGANO JIPYA AUDIO
 4. DOWNLOAD KISWAHILI AGANO JIPYA AUDIO
 5. SOMA NA SIKILIZA BIBLIA KWA KISWAHILI
 6. SOMA NA SIKILIZA BIBLIA KWA KIINGEREZA
 7. DOWNLOAD / PAKUA OSOTUA NGEJUK : Agano Jipya kwa Kimaasai. 

SOMA OSOTUA NGEJUK KWENYE MTANDAO (INTERNET) Inayo Fahirisi.

 NYIMBO, HADITHI ZA BIBLIA NA JESUS FILM                 

 1. NYIMBO ZA KIMAASAI: SIKILIZA NA DOWNLOAD
 2. NYIMBO KWA KISWAHILI NA KIINGEREZA : SIKILIZA / DOWNLOAD
 3. NYIMBO KWA KISWAHILI NA KIINGEREZA : SIKILIZA / DOWNLOAD 
 4. HADITHI ZA BIBLIA KWA KIMAASAI: SIKILIZA / DOWNLOAD
 5. HADITHI ZA BIBLIA KWA KISWAHILI: SIKILIZA  / DOWNLOAD 
 6. JESUS FILM KISWAHILI: ANGALIA VIDEO NA DOWNLOAD 
 7. JESUS FILM KIMAASAI: ANGALIA VIDEO / DOWNLOAD 

NYIMBO MPYA ZA KISASA

SIKILIZA NYIMBO ZA KIKRISTO KWA MFULULIZO. BONYEZA PICHA HAPO CHINI:

   NIDHAMU ZA MTUMISHI YA MUNGU

“Hata mtu akishindana katika michezo HAPEWI taji, asiposhindana KWA HALALI. Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa KWANZA wa kupata fungu la matunda (au ‘…kuwa wa kwanza KUONJA matunda yale…’). Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.” (2 Tim. 2:5-7).

Ujuzi hautoshi katika huduma. Ujuzi tu hautawatosheleza wasikilizaji. Haifai mkulima kuuza matunda yake kwa wengine pasipo kwanza yeye mwenyewe kuyala matunda ya kazi yake ili atambue kama yanafaa au la! Kama matunda ya maisha yako hayafai, utawafundishaje wengine? Haifai kuwalisha watu wa Mungu na ‘ujuzi’ wangu tu; kuwalisha na fikira na nadharia (ideas and theories) tu pasipo kwanza neno la Mungu kutimizwa katika maisha ya binafsi yangu kwa kadiri ipasavyo! Lazima mimi mwenyewe kwanza niwe ninaishi maisha ya Kristo kadiri ipasavyo. Matunda ya kiroho ambayo ni kupitia Yesu Kristo lazima yatokeze katika maisha yangu kwanza ili nisiwalishe watu wa Mungu na ujuzi tu! Hapo hamna njia ya mkato (short cut) katika huduma ya Bwana – au hata katika maisha ya Mkristo. Yesu mwenyewe alijaribiwa jangwani! Aliongozwa na Roho nyikani hali AMEJAA Roho Mtakatifu ili ajaribiwe na Ibilisi, lakini tutambue kuwa baada ya siku arobaini akarudi Galilaya kwa NGUVU za Roho! Hali kadhalika, lazima sisi sote tupite au kutembea katika njia ya nidhamu ya kiroho na majaribu. Tusiposhindana kwa halali, hatupewi taji. Na maisha hayo ya nidhamu ya kiroho na kimwili hayaishii baada ya muda tu, bali lazima yawe sehemu ya maisha yetu mpaka mwisho, kama Paulo alivyosema,

“Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio WOTE, lakini apokeaye tuzo ni MMOJA? Pigeni mbio NAMNA HIYO, ili MPATE.Na kila ashindanaye katika michezo HUJIZUIA KATIKA YOTE; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika. Hata mimi napiga mbio VIVYO HIVYO, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali NAUTESA mwili wangu na kuutumikisha; ISIWE, nikiisha kuwahubiri wengine, MWENYEWE niwe mtu wa kukataliwa.” (1 Wakor. 9:24-27).

Mtumishi wa Mungu wa dhati, anawalisha watu wa Mungu na neno la Mungu – ila ni lile neno la Mungu ambalo linatokana na uhusiano wake na Mungu! Kimsingi inapaswa lile analolihubiri litokane na maisha yake ya kiroho mbele ya Mungu na nidhamu yake ya kiroho na kimwili – kimsingi analohubiri lisiwe ni jambo la ‘ujuzi’ ambao ameukusanyika kutoka katika vitabu tu au kwenye shule ya Biblia! Hafai kuwajaza watu ujuzi tu! Mtumishi wa Mungu wa kweli amefanywa na Mungu kuwa mhudumu wa Agano Jipya – SIYO WA ANDIKO BALI WA ROHO. (2 Wakor. 3:6). Anahudumia kwa nguvu za Roho, na kwa Roho, sio tu kwa sababu ameshabatizwa na Roho Mtakatifu bali kwa sababu anatembea na Bwana kila siku naye anabadilishwa siku hadi siku kutokana na uhusiano wake na Mungu (2 Wakor.3:18).

Sisemi lile neno analohubiri ni tofauti na mafundisho ya Biblia, hapana, hata kidogo; ila analohubiri limejaribiwa katika maisha ya binafsi yake na kwa hiyo kwake kimsingi siyo jambo la ‘ujuzi’ bali linatokana na uzoefu wake wa dhati MBELE YA BWANA. Mwishoni, ‘kipawa’ au ‘karama’ peke yake havitoshi (Mathayo 7:22,23)! Lazima huduma yetu inatokana na nidhamu ya kiroho, ya kimwili na majaribu vivyo hivyo ilivyokuwa katika maisha ya Kristo Yesu! Kwa hiyo Paulo alimwandikia Timotheo,

“Usiache kuitumia KARAMA ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee. UYATAFAKARI hayo; UKAE katika hayo; ili KUENDELEA KWAKO kuwe DHAHIRI kwa watu wote. JITUNZE nafsi yako, na mafundisho yako. DUMU katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako NA WALE WAKUSIKIAO PIA.”

Na tukumbuke kuwa Daudi aliweza kumshinda kwa uhodari tele Goliathi kwa sababu KWANZA kutokana na uzoefu wake mwenyewe alishamwua simba na dubu – na hayo hayakutokea ‘mbele ya watu’ bali katika maisha yake ya binafsi ‘mbele ya Bwana’! Na Daudi hakutumia mavazi ya Sauli ya vita kumshinda Goliathi, alitumia ustadi na silaha ambazo ALIJIFUNZA MWENYEWE KUTOKANA NA IMANI YAKE KWA MUNGU!

Sisemi ni lazima muumini asubiri miaka mingi kabla ya kufanya huduma, hapana, lakini inapaswa mtumishi wa Mungu awalishe waumini na neno la Mungu litokanalo na uhusiano wake na Mungu na muda wake mbele ya Bwana!  

———————————————————-

Karibu jumbe hizi zote zimeandikwa na zimehuburiwa na mimi, David Stamen. Ninayo hakimiliki kwa zote. Lakini unaweza kupakua au kucopy jumbe hizo kwa ajili ya matumizi yako ya binafsi. Lakini kama ukitaka kuchapisha, kugawa au kutolewa makala au jumbe zangu, unijulishe kabla kuhusu kusudi lako ili nijue juu ya mpango wako. Unapochapa makala yangu, weka jina langu na anwani ya tovuti yangu kama ifuatayo:    © David Stamen somabiblia.com    Siyo halali kuuza makala au jumbe zangu.

KUWASILIANA NAMI, DAVID STAMEN:   kwa email: dsta12@hotmail.co.uk  /  kwa simu: +44 7985653844

 

Tags: , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , , ,