RSS

“Sikutamani Fedha wala Dhahabu, wala Mavazi ya Mtu.”

madumla

Mch. GASPER MADUMLA

“Sikutamani Fedha wala Dhahabu, wala Mavazi ya Mtu.”                                                                                                         

Paulo anawaambia wazee wa kanisa kutoka Efeso kwamba, “Sikutamani fedha wala dhahabu, wala mavazi ya mtu.” (Matendo 20:23). Hii inatuonesha kwamba Paulo hakuwa na tamaa juu ya mali ya mtu mwingine katika utumishi wake. Lakini pia Paulo anatufundisha kuwa hakuwa na tamaa ya kujinufaisha binafsi mahali popote katika utumishi wake aliyoitiwa.

Kati ya jambo moja baya katika huduma ya Mungu apewayo mtu ni kutamani fedha, dhahabu au mavazi kutoka kwa watu, ikumbukwe kuwa tamaa inaua huduma kabisa. Ninachokiangalia leo si kazi aliyoifanya Paulo kwa mikono yake na kupata kitu cha kujisaidia na kuwasaidia wale aliokuwa nao, bali ninachokiangalia ni ile namna ya kuishinda tamaa ya fedha katika huduma ya Mungu.

Wapo watumishi wa Mungu wenye kujawa na tamaa za pesa kutoka kwa waamini wao kinyume kabisa na neno la Mungu; watu hawa wameshindwa na tamaa ya kupenda pesa kwa kupindukia. Wakiamini kwamba mapato yote wanayoyakusanya ni sahihi mbele za Mungu kumbe sivyo, kwa maana mapato mengine ni kwa ajili yao ya kujinufaisha tu.

Huduma ya mtu yeyote afanyaye hivi, siku zote haiwezi kuhubiri kweli ya Mungu. Kwa sababu kweli ya Mungu, au Injili halisi haipatikani wala kusimamiwa na fedha wala dhahabu bali injili ya Kristo Yesu husimamiwa na kuongozwa na Roho mtakatifu.

Mfano mwingine huu hapa; Nalimuona mchungaji mmoja ambaye huvaa mavazi makukuu sana, hula kifahari pia na kuwa na gari za kifahari ambazo zote zimetokana na huduma. Kumbe yule mchungaji alikuwa anawalazimisha waamini wake watoe pesa nyingi kwa ajili ya kumpendezesha yeye na mke wake. Sasa kuna kipindi anazidi na kupitiliza michango yake maana hata katika kuhubiri kwake uhubiri kutoa ili ubarikiwe, tena utoe na kujiungamanisha naye kwa pesa sio kwa moyo.

Hakuna hapingae kwamba kutoa ni chanzo cha kubarikiwa, lakini basi iwe kutoa kwa moyo mkunjufu kwa kuelewa lakini sio kutoa kwa kulazimishwa kwa ajili ya matakwa ya mtu binafsi. Cha ajabu kwa mchungaji huyu ni kwamba waamini wake wamefulia yaani hawajafanikiwa kiuchumi hata kidogo.

Karibia wote wana hali ngumu kiuchumi, tena kuna wahitaji kama vile wajane wapo hapo hapo ambao na wao wamekamuliwa vijisenti vyao vya kula ugali na kuvitoa kwa mtumishi ambaye mtumishi huyo kaenda kujinunulia pea ya viatu vya mtoko. Ukiangalia kiundani utagundua kuwa mchungaji huyu alipaswa awasaidie wahitaji katika huduma yake na sio kuwakamua hata hao kwa matakwa yake.

Huduma yoyote ya Ki-Mungu ikiendeshwa katika roho ya tamaa ya kupenda pesa, kamwe haina mafanikio ya kiroho. Mungu wetu hakututuma tufanye huduma iwe biashara za kujinufaisha nafsi zetu, ndio maana haiwezekani huduma ya kweli ya Mungu isimame katika kupenda pesa kupindukia.

Ikiwa wachungaji wakirejea katika misingi ya kanisa la kwanza la akina Petro, watagundua kuwa hawakuwa hivi tulivyo leo. Bali wao walikuwa na vitu vyote shirika kwa utukufu wa Bwana. Leo haiko hivyo, maana wapo watumishi wenye kuwaka tamaa za mali waweze kujilimbikizia huku ndimi zao zinatoa udenda waonapo penye mali. Yaani mimi nakereka jamani!!! Sijui wewe unajisikiaje?

Utakuta mtumishi labda ni muimbaji au mchungaji anapoalikwa kuhudumu basi kitu cha kwanza anaanza kunegosheiti bei/ yaani anaanza kupanga kwamba watamlipa Tsh. ngapi, na akiona hazina maslahi haendi au la! Kama akienda nakwambia ataenda na mistari yake ya kutaka watu wamtolee pesa, na wala mistari hiyo ya Biblia utakuta ilikuwa haielezi kuhusu pesa. Hii ni mbaya sana katika huduma ya Kristo Yesu.

Ifike wakati sasa na wewe uzichunguze roho za watu wa namna hiyo, ili kama ni kujiengua katika huduma zao basi ujiengue maana sio dhambi kuhama huduma ambayo sio sahihi isiyoongozwa na Roho mtakatifu.

Mch. G.Madumla 2014. Dar Es Salaam

 

3 responses to ““Sikutamani Fedha wala Dhahabu, wala Mavazi ya Mtu.”

 1. John wakuchalo.

  March 29, 2017 at 3:23 pm

  Ni,somo zuri.Mungu akubariki.Kiukweli kwa sasa kuna changamoto kubwa katika utumishi.Mfano,hata,katika hili,waweza kushangaa wachungaji woote wana fundisha hivi hivi! lakini!lakini! hawaendi vile wanavyo fundisha.Imefika hatua sasa waamini wanautumia mstari wa biblia,Yesu asemayo,waandishi,na mafarisayo wamekaa katika kiti kilekile cha Musa wanayosema ni ya kweli, yashikeni lakini namuna ya matendo yao msifuate.Maana wao husema bila kutenda wayasemayo.Hii,ni changamoto kubwa zaidi wakati huhu.Mchungaji,uni samehe,simaanishi kwamba wewe hutendi usemayo,bali najaribu kukuonyesha,ni kiasi gani tunavurugwa.Hali,ni mbaya.Tuombe Mungu awape nuru watu wake sawa na rehema zake.Yeye tu! anaweza.

   
 2. JOEL e mweta

  April 14, 2017 at 5:49 pm

  pasta asant kwa kuwa umesimamia kwel hebu mungu naakubariki na aendelee kuku funulia mengi hasa katik nyakt hiz

   
 3. Alex G Hoka

  October 26, 2017 at 5:36 pm

  AMINA BR,MSIRUDI NYUMA,SONGENI MBELE TU,MUNGU AWABARIKI SANA,

   

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: