BALAA AU BARAKA
‘MAMBO YOTE HAYA YAKO KINYUME NAMI.’
Kibinadamu tungeweza kusema kuwa mambo mabaya yamemtokea Yakobo. Alimpoteza mtoto wake mmoja. Na tena akatokewa na ukame wa kutisha. Kisha mwanae mwingine akawa amechukuliwa utumwani. Ndipo alipofikiria kuwa anaweza kuwapoteza wanaawe wote iwapo atawapeleka Misri tena, na kwa huzuni alipiga kelele..
“Yakobo baba yao akawaambia, ‘Mmeniondolea watoto wangu! Yusuphu hayuko, wala Simioni hayuko, na Benjamini mnataka kumchukua nae. MAMBO HAYA YOTE YAMENIPATA MIMI. (Mwanzo 42:36)
‘Mambo yote haya yako kinyume nami.’ Hiyo ilikuwa maana ya maneno yake, na hivyo Biblia ya KJV (Kiingereza) inavyotafsiri mstari huo. Je umewahi kujiliwa namna hii? Ukweli ni kwamba MUNGU MWENYEWE NDIYE ALIYE KUWEMO KATIKA MAZINGIRA HAYO YOTE YA YAKOBO. Mungu alikuwa kazini ilikuletea baraka kubwa Yakobo, pamoja na familia yake yote. Kile ambacho Yakobo alikuwa anakiona kama ni adui, kama ni tishio, kama ni hatari kwake, kumbe ilikuwa ni uhalisia wa mkono wa Mungu mwenyewe katika kumwongoza kuelekea kwenye BARAKA KUBWA. Wakristo wengine wanapoingia katika matatizo huanza kwa urahisi tu kumlaumu shetani, au pale mambo yanapokuwa hayafanyiki kama wanavyopenda yawe. Wanavurugikiwa badala ya kujitoa maisha yao kama dhabihu iliyo hai kwake Mungu katika mazingira yao ili kwamba ipate kuthibitisha kile kilicho chema, chenye kukubalika na mapenzi makamilifu ya Mungu katika maisha yao (Warumi 12:2).
Paulo alitangaza ukweli huo,
“…Kristo yu hai ndani yangu, na uhai nilio nao sasa katika mwili ninao katika imani ya mwana wa Mungu,ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.(Wagalatia 2:20)
Paulo aliishi kwa imani. Kwa imani ya namna gani? Kwa imani katika mwana wa Mungu? Ndiyo, lakini ni zaidi ya hiyo; aliishi siku kwa siku akiamini katika mambo yote kwamba Yesu Kristo alimpenda na akajitoa yeye mwenyewe kwa ajili yake, pasipo kujali chochote kinachoweza kutokea! Hii ni imani ambayo pengine yaweza kuonekana haibadili mazingira yetu mara moja, au pengine haitabadilisha mazingira yetu kabisa, lakini hii ndiyo IMANI INAYOTUBADILISHA SISI WENYEWE katika mazingira yetu! Ni imani inayoushinda ulimwengu. Ni imani inayotufanya sisi kuvumilia katika majaribu na matatizo na hutuleta katika ufahamu halisi kuona kuwa Kristo anaishi ndani yetu, na huyafanya mambo yote yafanye kazi kwa uzuri! Ni imani ambayo hutubadilisha sisi na kumtukuza Mungu. Ni imani inayompendeza Mungu!
Sasa inakuwaje basi baadhi ya waamini wanafikiri mara moja kuwa Mungu hapendezwi nao kwa sababu tu eti mambo yao wakati mwingine hayaendi sawa au kwa sababu wanakutana na shida? Hiyo siyo imani. Hizo ni imani za kishirikina. Bila sababu yoyote tunafikiri kuwa majeshi ya giza fulani yapo kinyume nasi na kwamba yanataka kutuadhibu.Tunapokuwa tunafanya aina hii ya hofu na mitazamo ya hasi, tunakuwa hatumheshimu Mungu.
Paulo alivunjikiwa na jahazi mara tatu. Je hii inamanisha kuwa Mungu alikuwa kinyume naye? Je Mungu alikuwa anamwadhibu? Bibilia iko wazi kwamba jibu lake ni ‘Hapana’. Paulo anasema,
“…twajua yakuwa kaika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema yaani wale walioitwa kwa kusudi lake..”(Warumi 8:28)
Kwa hiyo Paulo aliweza kusema, “Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” (Wafilipi 4:12,13)
Paulo alikutana na matatizo pamoja na majaribu mengi lakini ushuhuda wake na mafundisho yake ni kuwa TUNAJUA kuwa mambo yote hufanya kazi pamoja kwa wema kwa wao wampendao Mungu! Hii ni yenye nguvu. Hii huingia moja kwa moja kwenye mizizi ya mahusiano yetu pamoja na Mungu. Je, kumtumaini Mungu kwetu kuna zama ndani zaidi kuliko yale yanayotutokea au yasiyotutokea? Je, imani ni kumwamini Mungu katika kufanya mambo tu? Ni zaidi ya hapo. Kujaribiwa kwa imani yetu ni kitu cha thamani kuliko hata dhahabu (1 Petro 1:7). Imani ni kumwamini Mungu pale ambapo hakuna chochote kinachotokea, au mambo yanapoonekena kutuendea vibaya. Hii ndiyo imani ya kweli, inaingia ndani zaidi kuliko mazingira ya aina yoyote. Tunashawishika kikamilifu kuhusiana na wema Wake na umaminifu KULIKO MAZINGIRA YOYOTE yanayotufanya tutie shaka pendo lake kwaajili yetu. Hii ndiyo imani. Matokeo ya imani hiyo hiyo katika maisha yako na yangu ni amani kubwa sana na ushupavu mioyoni mwetu wakati tunapokutwa na shida au balaa. Wasikilize watu hawa watutu toka katika Agano la Kale.
“Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto, naye atatuokoa na mkono wako ee mfalme. BASI KAMA SI HIVYO, ujue ee mfalme, SISI HATUTAKUBALI KUITUMIKIA MIUUNGU YAKO wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha, (Danieli 3:17-18).
Ni mistari ya ajabu namna gani hii! Ndiyo tunajua kuwa Mungu aweza kutuokoa sisi kutoka katika moto huu uwakao, wanasema. LAKINI HATA KAMA HATAFANYA HIVYO, haitabadilisha lolote! Tutaendelea kumwabudu Yeye BILA KUJALI KITAKACHOTOKEA. Baadhi ya wakristo wanaanza kumtiliashaka Mungu na pendo lake eti kwa kuwa tu haonyeshi kuingilia mazingira yao. “Yeye ni mwenye nguvu zote, kwa nini hafanyi lolote? Je, ni kweli anatupenda?” Haya ni aina ya mawazo yanayozalishwa na kutokuamini, na yanaungwa mkono na shetaani. Meshak, Shadraki na Abdinego wao hawakusita, wala hawakukaribisha mawazo kama hayo, pasipokujali kilichowatokea wao waliendelea kumwabudu Mungu. Hii haiwezi kutengenezwa au kuiga! Imani hii inatoka ndani kabisa ya moyo wa mtu. Inatokana na kuendelevu wa kumjitoa na kumpenda mwokozi wetu kila siku, kwa ajili ya utukufu wa Mungu! Ndiyo sababu Paulo anasema,
“Wala si hivyo tu, ila na tufurahi katika dhiki pia, tukijua yakuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi, na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo, na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini, na tumaini halitaharishi, kwa maana PENDO LA MUNGU LIMEKWISHA KUMIMINWA NDANI YETU na Roho Mtakatifu tuliye pewa sisi.” (Warumi 5:3-5).
Ni ule uzoefu wa kupita katika matatizo ndio unaotufundisha sisi kuweka mategemeo yetu tumaini letu katika Mungu, na hii hutusababishia sisi kumjua kwa undani zaidi kuwa yeye ni Mwaminifu, Mwema na wakutegemewa! Ni imani hiyo iliyotokana na majaribu hayo, hiyo ni yenye thamani zaidi kuliko dhahabu. Imani hii inamtukuza Mungu na haitoi nafasi kwa shetani.
Ayubu alipokutwa na balaa, je, alimpima au kumhukumu Mungu au upendo wake sawasawa na mambo yale yaliyompata? Hapana. Katika kupoteza mali yake yote na watoto wake wote, alimwabudu na kumtukuza Mungu tu! Tunasoma maneno yafuatayo, “Ndipo Ayubu akainuka…na kuanguka chini, na KUSUJUDIA…akasema, Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.” (Ayubu 1:20,21). Imani hiyo ni ya thamani sana”. Hiyo siyo jambo la ‘kuamini kitu’ tu, bali inatuonyesha kwa wazi ule UHUSIANO Ayubu alio nao na Mungu! Alimwamini Mungu pasipo kujali mazingira; aliamini na kutegemea Uaminifu wa Mungu; hakulaumu tabia ya Mungu, badala yake aliitukuza tabia ya Mungu. Hiyo haitokei kwa ghafla! Sisi tumeitwa tumwamini na kumpenda Mungu kila siku, haijalishi mambo yanayotokea au yasiyotokea – kuishi bila kuona shaka juu ya pendo lake kwako; bila kufikiri Mungu ni kinyume nawe. Badala yake kuwa na hakika juu ya Uaminifu wa Mungu na juu ya tabia Yake.
Mungu aliwaahidi Waisraeli kuwapatia nchi inayo miminika maziwa na asali, na watu wa Mungu walikusudia kufurahia huku wakimwona Mungu akiwafanyia mambo kwa niaba yao, kwa kuwafungulia njia katika bahari ya shamu na kuwashindia dhidi ya Wamisri. Lakini mara tu shida ilipowajia waliangukia katika kutokuamini, na sio tu walimlaumu Musa, bali walimlaumu Mungu mwenyewe kwa kusimama kinyume nao. Wao walimshtaki Mungu hata kusema kuwa Mungu aliwachukia wao na kwamba amewaleta hadi jangwani ili kuwaangamiza humo! (Kumb.1:27) Hapo ndipo kutokuamini kwaweza kutuleta sisi kama tutairuhusu! Je kukoje moyoni mwako?
Kwa sababu ya kutokuamini kwao Waisraeli wengi hawakuweza kuingia katika nchi ile ya ahadi. Walimpima Mungu kwa kujilinganisha na mazingira yao kwa nje. Lakini Mungu amekwisha kuridhia pendo lake kwa ajili yetu, na amelionyesha pendo lake kwa kutukomboa kutoka katika nguvu za adui! Hatupaswi kumpima Mungu kwa mazingira ya nje. Tunapaswa kumtegemea yeye kwa sababu ya kile ambacho amekwisha kukifanya kwa ajili yetu. Na kwa sababu yeye ni Mungu. Mazingira yetu yanayobadilikabadilika, hayambadilishi Yeye! Wala imani yetu katika yeye isibadilike kwa sababu tu eti mazingira yetu ni magumu.
Kama unataka kumpima Mungu kwa kuangalia mazingira yako kwa nje, basi mpime yeye kwa mazingira haya – PALE CALVARI! Kama unataka kufahamu jinsi Mungu anavyojisikia kukuhusu wewe, tazama pale MSALABANI. Mungu alitoa kitu cha thamani zaidi ambacho angeweza kutoa kwa ajili yako – alimtoa mwanae pekee. Alitupenda sisi zaidi hata akamtoa mwanae pekee Yesu Kristo afe pale Calvari!
“Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi” (Warumi 5:8).
Haya ndiyo mazingira yanayoonyesha pendo la Mungu kwa ajili yetu. Ni tukio kubwa zaidi ambalo halijawahi kutokea! Umpime Mungu kwa mazingira hili, yaani ya msalaba, na mazingira mengine yote yawayo katika maisha yako utayaona na macho mapya! Kwa hiyo Paulo anaenda mbali zaidi katika kusema kuwa…
“Kwa maana nayahesabu mateso ya wakati huu wa sasa kuwa si kitu, kama utukufu ule utaofunuliwa kwetu”(Warumi 8:18)
Kila siku maisha yetu yanapaswa kuwa ni dhabihu iliyo hai ya upendo, kutafakari, utii, sifa na kumtegemea Mungu kikamilifu yeye aliyetupenda na ambaye huyafanya mambo yote yafanye kazi kwa wema. Paulo aliishi namna hiyo na hata alidiriki kusema…
“Basi tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu ni nani aliye juu yetu? (Soma Warumi 8:31-37)
Uitazame msalaba ukaone kuwa Mungu ni kwa ajili yako, yupo kazini ka ajili ya kila mazingira, ILI KUKUFANANISHA WEWE NA MIMI KWA SURA YA MWANAE. Hili ni jambo lenye utukufu; hili ni jambo jema lile alilofanya Mungu ndani yetu, yaani, tufananishwe na mfano wa Mwana Wake! Hicho ndicho kinachosemwa katika Warumi 8:29 ambao unafuatia baada ya ule mstari wa 28. Yawezekana unajiuliza, ni jambo gani jema laweza kutoka katika mazingira yenye shida? Jibu la Biblia ni, ‘Yesu Kristo.’ Yesu Kristo ndani yako tumaini lenye utukufu!
Usifikiri kuwa Mungu yu kinyume nawe. Jikabidhi kwake, ujitoe kwake, pasipo masharti. Yeye anakupenda, na kama ilivyo kuwa kwa Yakobo, ni vilevile kwako wewe. Ataendelea kufanya kazi katika maisha yako ili kukuletea baraka timilifu katika Kristo Yesu. Mungu hayupo pale ili kutimiza matarajio na ndoto zetu za binafsi, au hata mipango yetu. (Utatambua na kujua mapenzi YAKE kwa ajili ya maisha yako ikiwa unafuata agizo la neno la Mungu katika Warumin 12:1,2). Yeye hufanya kazi ili kutubariki katika Kristo Yesu. Kwa vyovyote shetani yupo kazini, na hufanya mambo kujaribu kuangamiza kazi za Mungu, na kuwanyanganya watu wa Mungu ule urithi wao ulimo katika Kristo Yesu. Lakini wewe utaweza tu kuelewa nini ni nini katika maisha yako, na katika mazingira yako pale tu utakapojitoa maisha yako kama dhabihu iliyo hai kikamilifu na pasipo malalamiko au masharti kwa Mungu kila siku! Vinginevyo unaweza kujikuta wewe mwenyewew ukipambana kinyume na Mungu, huku ukifikiria labda ni shetani katika mazingira yako, kama vile ilivyo kuwa kwa Yakobo.
Yusufu mwana wa Yakobo alipitia katika kuushuhudia uovu mwingi kinyume naye, na mazingira ambayo kwa uhakika yalikuwa magumu na yasiyo ya haki – alichukiwa na hatimaye akauzwa utumwani na ndugu zake yeye mwenyewe, alisingizwa na mke wa bosi wake, pasipo haki akatupwa gerezani, lakini mwisho wa hayo yote, yeye alisema nini?
“nanyi kweli mlikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa kama ilivyo leo.” (Mwanzo 50:20).
Ni maneno ya ajabu ya jinsi gani! Hakuna uchungu. Hakuna malalamiko. Yusufu aligundua mkono wa Mungu katika mazingira yake yote. Na wewe? Sio mambo yote yaliyomtokea Yusufu yakuwa sawa; mambo yasiyo kweli yalimtokea Yusufu. Alipitia katika mambo ya mateso, alivumilia na kuwa mnyenyekevu, lakini alikabidhi maisha yake na roho yake kwa Mungu katika mambo yote na akamwabudu Mungu. Hakupambana au kufanyia ushawishi katika mazingira yake ili kupata kile alichotaka apate. Mungu alifanya kazi kwa niaba yake ili kumletea utimilifu wa baraka.
Basi na Mungu afanye hivyo katika maisha yetu yote.
© David Stamen 2014 somabiblia.com