RSS

VIRUSI VYA KORONA KATIKA MUKTADHA WA KIBIBLIA

VIRUSI VYA KORONA KATIKA MUKTADHA WA KIBIBLIA.

1  WAKRISTO WA AGANO JIPYA WALIFANYAJE WALIPOKABILIANA NA JANGA?              
2  MAJANGA MENGINE                                                                                                                  
3  INJILI NA HUDUMA YA UPATANISHO .            
4  KUHUBIRI INJILI.                                                                                                                         
5  CHINI YA AGANO LA KALE.                                                                                                       
6  MAELEZO ZAIDI KUHUSU MAJANGA NA HUKUMU.                                                             
7  KUHUSU KAZI YA SHETANI.                                                                                                      
8  MITAZAMO AMBAYO BADO INANBAKI KUTOKA KWA UTAMADUNI WA UCHAWI.                      
9  MAJANGA YA ASILI NA JINSI YA KUYATAFSIRI.                                                                    
10 JINSI TUNAVYOPASWA KABILIANA NA MAMBO HAYO – USHUHUDA WETU.                 
11   NENO LA MWISHO.      

Kwa sababu ya kuchanganyikiwa na hata kuwa na hofu iliyosababishwa na mafundisho ya uongo kuhusu virusi vya korona, nimejitahidi katika somo hili kutoa muktadha wa kibiblia nikitumaini kwamba utakupatia ufahamu wa mambo ya kibiblia yahusuyo mada hii. Ili kupata manufaa halisi ya somo hili, ningependa kumtia moyo msomaji ili avumilie kuisoma makala yote.

  1. WAKRISTO WA AGANO JIPYA WALIFANYAJE WALIPOKABILIANA NA JANGA?

Katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 11 tunasoma kwamba Wakristo walisafiri hadi Antiokia kuyakimbia mateso yaliyosababishwa na Wayahudi wasioamini. (Mdo 11:19). Katika sura hiyo tunaambiwa kwamba nabii Agabo toka Jerusalem alifika katika kanisa la Antiokia na kutabiri kwamba njaa kubwa ingekuja dunia nzima. Hapa tunaona hali ya mateso ya kanisa ambavyo ingefuatiwa na njaa kubwa mno. Sasa tunaweza kujifunza ni kwa jinsi gani wale waumini WA AGANO JIPYA walivyoshughulisha na matukio mawili hayo. Je, walikuwa na mtazamo wa namna gani?

Agabo, Paulo na Barnaba walikuwa ni Wayahudi waliojua vema ule uhusiano kati ya majanga asili na hukumu ya Mungu katika historia ya Israeli CHINI YA AGANO LA KALE. Sasa watu hawa walikuwa wanafundisha Wakristo wapya habari za Yesu Kristo na Agano Jipya huko Antiokia.

Waliyafanyaje hayo? Je, walisema ya kwamba ile njaa ilikuwa ni hukumu ya Mungu, hivyo waliwaongoza watu wajishushe, wakiri na kutubu kwa ajili ya dhambi za mji wa Antiokia, kwamba hapo ndipo Mungu angeiponya nchi; au wakiri na kutubu kwa ajili ya dhambi za nchi ya Syria, kwa sababu Antiokia ilikuwa sehemu ya nchi hii? Jibu lake ni ‘Hapana’, hawakufanya hivyo. Je, walifundisha waumini wapya kwamba njaa ile ilitokana na Ibilisi ndio maana Mungu aliwaambia juu ya janga hili ili wangeweza kuomba dhidi ya ibilisi? Jibu ni ‘Hapana’, hawakufanya hivyo. Hakuna neno hata moja linalohusu mambo haya katika mstari huo ya Matendo sura ya 11. Zaidi ya hayo, baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo hatuna mfano wala mafundisho ya Agano Jipya yanayoeleza kwamba waumini wanakiri au kuomba kwa ajili ya dhambi za nchi wanayokaa. Hii ni muhimu kwetu kuelewa.

Kifo cha Yesu msalabani kilibadilisha kila kitu.

Hivyo fikra zetu na msimamo wetu lazima vibadilike. Hatuishi katika Agano la Kale kwa sasa. Mahusiano ya Mungu na ulimwengu huu yamebadilika, hivyo yatupasa kujua haya mabadiliko yaliyoletwa na injili ili tusiishi ama kufikiri kama tungali katika Agano la Kale.

Utakumbuka kwamba Katika Agano la Kale Mungu alituma manabii kutabiri juu ya watu wake Israeli kwa sababu ya ibada za sanamu na dhambi zao, hivyo Mungu aliwaonya kuhusu hukumu yake juu yao endapo wangeendelea na dhambi zao. Lakini sasa tunasoma nini katika Agano Jipya? Agabo alipotabiri kuhusu njaa ambayo ingekuja dunia nzima, Wakristo walifanyaje? Je, walijiuliza kwamba ile ilikuwa ni ishara ya Mungu kuhukumu ulimwengu kwa sababu ya dhambi zao, au ilikuwa ni ishara ya ghadhabu ya Mungu kwa watu wake, yaani Wakristo, kwa sababu ya dhambi zao? Je, walitafuta tafuta kujua kama njaa ile ilitoka kwa ibilisi, au kwa Mungu? Hapana.

Wangeweza kujiuliza maswali mengi mno juu ya kile kilichotabiriwa kiasi cha kuchanganyikiwa na kujawa na hofu na mahangaiko moyoni kwa KUJARIBU KUBASHIRI kiachotokea. Maswali hayo yanaweza kuzunguka kichwani na moyoni mwa mtu mpaka kichwa chake kimechanganyika na moyo wake umehangaika. Hiyo siyo namna ya kuishi. Hali hiyo haitokani na maisha ya kiroho.

Kwa maswali yote haya hakika hakuna awezaye kuomba! Maombi ni lazima yawe ya kiimani, na imani huja kwa neno la Mungu (Warumi10:17). Maombi yetu hayapaswi kuwa ya KUBAHATISHA juu ya tukio la namna hiyo. Maombi yetu hayapaswi kutokana na hofu, au machanganyiko vichwani vyetu kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, au ushirikina – je, janga hilo linatokana na hukumu ya Mungu juu ya nchi, au juu ya waumini; je, tunapaswa kujinyenyeza; au je, ni kazi ya Shetani ambayo tunapaswa kuomba dhidi yake, nkd, nkd?

Ninajiuliza kwamba masaa mengi yamepotea katika maombi kwa sababu watu huomba si kwa sababu ya mambo yaliyofunuliwa kwao na Mungu, au kwa sababu wamechunguza Biblia inachofundisha, bali ni matokeo ya hisia tu – maombi yao yanatokana na hofu au na tamaa janga hilo liondolewe tu. Baadhi ya watu wanajisumbua sana kichwani na moyoni kwa sababu huwaza moja kwa moja kuwa kama janga inaendelea, inamaanisha Ibilisi anashinda, na hivyo yapasa kumzuia kwa maombi yetu. Hivyo maafa yasipoondoka huchanganyikiwa na kudhani ya kwamba Mungu hayupo kazini, au Ibilisi ameshinda! Hivyo hupoteza amani na furaha katika Bwana. Haya yote ni matokea ya kuomba pasipo kufikiri hasa ni nini Biblia inafundisha, na ni nini Biblia haifundishi.

Haya mawazo yote ni kama kujaribu kunyakua kitu gizani. Siyo imani, siyo kuenenda katika ufahamu na hekima; haileti nuru, haileti pumziko na amani katika moyo na fikra. Fikra za namna hizo ni za kibinadamu tu, zitokanazo na hofu na kukosa imani ya kweli katika Mungu.

Sasa hii inaturudisha kwa Wakristo wa Antiokia. Utakumbuka kuwa walipitia katika mateso, na sasa walikuwa wanakaribia kuingia katika kipindi kigumu cha njaa. Hivi walisumbuliwa na hayo maswali ambayo tumeyaona hapo juu? Jibu la wazi ni, ‘Hapana’. Hatusomi kitu kama hiki. Paulo, Barnaba, Agabo na wengine huko Antiokia walikuwa Wayahudi kwa kuzaliwa na walijua vizuri sana ni kwa jinsi gani Mungu alivyokuwa ameshughulika na taifa la Israeli, lakini hawakulichukulia jambo lile KANA KWAMBA WALIKUWA CHINI YA AGANO LA KALE. Tunaona kuwa hapakuwa na maombi ya toba wala ya kukiri dhambi. Sasa walifanya nini kuhusu hiyo njaa iliyokaribia kubomoa dunia? Walichofanya ni hiki: walikumbuka ya kwamba waumini wengi wa kikristo huko Uyahudi walikuwa maskini na walikuwa chini ya mateso, wakagundua kuwa walikuwa katika hatari ya kuangamia kwa njaa. Hivyo walianza kuchangisha fedha na kuzituma Uyahudi ili kusaidia Wakristo maskini. Hivyo ndivyo walivyofanya. Katika tukio hilo hatusomi kwamba kuna jambo lingine lililofanyika. Walichanga fedha na kuzipeleka kusaidia Wakristo maskini ilikuwa ndiyo wazo na mtazamo wao tu!

Kumbe! Hamna hofu. Hamna machaganyiko. Hamna malalamiko kana kwamba Mungu hayupo kazini na Ibilisi sasa anatawala! Hamna. Hawakujisumbua na kujitesa na fikra na maswali mbalimbali yasiyofaa na yasiyoongoza po pote. Kutokana na moyo wa upendo, mara moja waliamua kuwasaidia waumini maskini – hiyo tu. Bwana asifiwe!

Sijui kama walimwomba Mungu awafunulie sababu ya kiroho ya janga lakini ni wazi hawakuwa na maarifa ya namna hayo kwani hatusomi kitu cho chote juu ya hicho. Waliendelea kuishi wakimtegemea Mungu tu na kuwahurumia waumini waliopatwa na mateso. Na wewe, na mimi?

Umeona? Fikra zao zilikuwa zimebadilika kwa sabau Kalvari imebadilisha kila kitu. Na kama tutakavyona hapo chini, uhusiano kati ya Mungu umebadilika kabisa. Hawakuwa tena chini ya Agano la Kale. Yesu alikufa ili kuwakomboa na kuwaleta ili wawe na uhusiano naye. Wao walitambua kwamba Mungu aliruhusu hiyo njaa, hivyo waliamua kushughulika na jambo hilo kwa kuwasaidia waumini wa kikristo walioathirika. Mungu hakusema neno lolote isipokuwa kwamba ingetokea njaa, hivyo hawakuhitaji KUBASHIRI kile alichokuwa akifanya Mungu na sababu chake. Ukitafuta tafuta jibu au maelezo wakati Mungu mwenyewe hasemi kitu zaidi, utazunguka gizani tu moyoni mwako na utajisumbua na kujitesa.

Ni wazi tunapenda kuuliza, ‘kwa nini’? Lakini katika kitabu cha Matendo sura ya kwanza wanafunzi walimwuliza Yesu, “Bwana, wakati huu ndipo utakapowarudishia Israel ufalme”. Yesu alitoa jibu gani? Alisema, “Si kazi yenu kujua nyakati wala majira Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.” Kwa maneno mengine, walipaswa kuridhika kuwa hawakuwa na uwezo wa kujua baadhi ya mambo! Wakristo wa Antiokia waliridhika kwa kutokujua mambo yote, hivyo hawakujisumbua vichwani mwao kwa sababu Mungu hakudhihirisha sababu ya kiroho ya janga lile. Badala yake, walilichukulia kwa moyo wa huruma na upendo kwa waumini waliokuwa wakiteseka nao walitengeneza nia ya kuwasaidia. Bwana asifiwe!

Waumini wa Antiokia hawakujisumbua na kuhangaika juu ya maswali ya hukumu ya Mungu au mashambulio ya Shetani.

Hebu na tutambue ya kuwa Wakristo wa Antiokia walielewa na kukubali kwamba njaa iliyotarajiwa kuja dunia ingeathiri waumuni na kufanya maisha yawe magumu, kwao na kwa watu wengine. Walitambua hivyo bila ya manung’uniko kwamba Wakristo wangepita katika kipindi kigumu sawa na watu wengine wasioamini kwa sababu majanga ya asili. Hivyo Wakristo wa Antiokia walichukua hatua ya kusaidia waumini wa Uyahudi waepukane na njaa. Hapakuwa na maombi ya dhidi ya ibilisi, hapakuwa na kutubu dhambi za ulimwengu au nchi. Walichukua hatua kivitendo kusaidia waumini wengine kwa kuwakinga na athari za njaa ambayo ingetokea. Na kama una rasilimali fedha, ndivyo unavyofanya sasa? Ndivyo unavyochukua hatua katika hali hii ya virusi vya corona? Ndilo wazo lako la kuu na la kwanza kusaidia ndugu wa kike na wa kiume katika Kristo ambao wamepoteza kazi, au wanakabiliwa na njaa? Tunasoma Biblia zetu? Tunapenda kufundishwa na kulishwa na neno la Mungu?

Matendo ya Mitume 11 ni mfano mzuri wa kile walichofanya Wakristo walipokabiliwa na maafa. Japokuwa si mafundisho ya moja kwa moja, hata hivyo yanaweza kutusaidia kupata ufahamu wa fikra za Wakristo wa Agano Jipya juu ya kukabiliana na maafa.

  1. MAJANGA MENGINE

Kama muda wa miaka 5 lilikuwa na ukame na mafuriko vilivyosababisha ugumu wa maisha kwa walio wengi kama si kila mmoja nchini Tanzania. Zaidi ya hayo, karibu watu millioni 5 hadi 10 huugua malaria kwa mwaka, kati ya hao 80,000 wanafariki. Hili linawaathiri watu wote. Hii haina tofauti na ugonjwa wa virusi vya corona, ambavyo huathiri watu. Je, wahubiri walituambia tumkemee ibilisi ili kwamba malaria iweze kutoweka nchini Tanzania – au wanaenda kulala wanatundika chandalua juu ya vitanda vyao? Je, wahubiri wanaita watu wakiri dhambi za taifa na kutubu ili kwamba isiwepo njaa tena, na mafuriko yanayoharibu mazao Tanzania? Kama ni hapana, kwa nini? Najua virusi vya corona vinaadhiri kila mmoja wetu kijamii kwa namna ambayo hayo matatizo mengine yaliyotajwa hapo juu hayawezi, lakini kwa nini watu wamechagua kukiri dhambi za taifa kwa ajili ya janga moja tu na si mengine? Hili halina jibu. Halina hata sababu ya msingi wa kibiblia. Mpendwa msomaji, jambo hili halina msingi wa kibiblia unapoanza kutubu kwa ajili ya dhambi za nchi kila yanapotokea majanga, kana kwamba sisi ni taifa la Israeli chini ya Agano la Kale. Haya ni majira ya neema Injili.

Mungu hatumii nabii kila mara katika nchi kuwaambia ya kuwa ataleta janga la aina fulani wasipotubu kama ilivyokuwa kwa Israeli chini ya Agano la Kale. Bali Mungu anaongea kupitia mwanawe, kupitia katika Injili. Hivi ndivyo anavyoongea. Mungu ametoa Mwanawe ili watu wenyewe watubu kupitia kuhubiri kwa Habari Njema ya Yesu Kristo!

Kati ya mwaka 1918 na 1920 kulitokea janga la kimataifa. Liliitwa mafua ya kihispania. Dunia nzima waliathirika watu 500 millioni, na watu 50 millioni walikufa. Janga hilo lilikuja na kupita. Hivyo na janga hilo lililokuja, nalo inaonekana litapita. Hatuwezi kutarajia kwamba tutabaki bila kuguswa na mambo kama hayo, lakini naandika juu ya tumaini tulilonalo kwa Mungu katika sehemu nyingine ya somo hili.

  1. INJILI NA HUDUMA YA UPATANISHO . KAZI YA MUNGU KUPITIA MSALABA.

Katika sehemu nyingine ya somo hilo nitaonyesha wazi kuwa hata Waisraeli, kama watu wa Mungu, hawakukiri ama kutubu kwa ajili ya dhambi za taifa lingine. Hili halijulikani katika Biblia, na hasa ni muhimu kwetu kuelewa hili katika muktadha wa kile alichofanya Mungu kupitia Yesu Kristo msalabani.

Tunasoma hayo katika 2 Wakorintho 5:19, “Yaani Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho” Yesu alikuwa mwana kondoo wa Mungu achukuaye dhambi za ulimwengu (Yohana 1:29) kwa kifo chake msalabani! Na Yohana anatwambia katika waraka wake wa kwanza, “Naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.” (1Yohana 2:2). Na tunasoma nini katika waraka wa Warumi? Neno la Mungu linasema hivi, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi…Kwa maana ikiwa TULIPOKUWA ADUI tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.” (Warumi 5:8-10). Mistari hiyo inatueleza kuwa Yesu ametwaa msamaha wa dhambi kwa watu wote alipokufa msalabani – na alifanya hivyo wanadamu walipokuwa bado ni wenye dhambi na ni maadui. Amekwisha kufanya hivyo. Imekwisha!

Kama hii ni neema ya Mungu kwa wenye dhambi, sasa mbona unakiri na kutubu dhambi za watu wa nchini mwako? Unataka kuongeza sala zako katika kazi aliyoimaliza Kristo pale Kalvari? Unadhani kazi yake pale msalabani haitoshelezi kuleta msamaha kwa wenye dhambi? Unadhani maombi yako yatafanikiwa kuliko mauti ya Kristo? Unadhani Kristo hakuteseka vya kutosha kiasi cha kupata neema, rehema na masamaha kwa kila mwanaune na mwanamke? Hivi ndivyo unavyodhani? Ndiyo, hakika hivi ndivyo unavyodhani kama unajaribu kutubu kwa ajili ya dhambi za nchi yako. Sala zako ziko kinyume na Injili ya Yesu Kristo. Au kwa upande mwingine, unadhani neno la Mungu siyo la kweli? Kwa upendo wake na wema wake amewasamehe wanaume na wanawake walipokuwa wangali na maadui zake. Unadhani Mungu alighadhabika na kuchoka, na sasa analeta majanga mbali mbali katika nchi yako kwa sababu wenye dhambi hawakutubu? Unadhani ya kuwa msingi wa toba kwa sasa ni Injili ya Yesu Kristo, au ni hofu na hukumu ya pigo la majanga ya asili? Unadhani Mungu amebadili fikra zake kuhusu Kalvari bila ya kutuambia? Hapana!

Hivi hujasoma ya kuwa, “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika mwana..”(Waebrania 1:1,2). Mungu anasema nasi siku hizi katika mwana, kupitia yale ambayo mwana ametenda msalabani, kupitia Injili ya Yesu Kristo. Na kwa sababu ya kumwaga damu yake akamtuma Roho Mtakatifu, na ni Roho wa Mungu ambaye ATAWAHAKIKISHIA WANAUME NA WANAWAKE HABARI YA “DHAMBI, HAKI NA HUKUMU”(Yohana 16:7-11). Je! Unafikiria kwamba huduma ya Roho Mtakatifu imekoma na kwamba Wakristo katika nchi yako wanahitaji kukiri na kutubu dhambi za wasioamini badala ya wenye dhambi wenyewe kutubu? Au unadhani Kristo aliteswa hadi kufa msalabani kusamehe wenye dhambi za walimwengu walipokuwa adui yake, na baadaye akatuma mapigo kwa sababu ana hasira ya dhambi zao? Mungu hajawabadili ghafla mawazo yake! Ni Roho wa Mungu ndiye anayewahakikishia habari ya dhambi kwa njia ya mahubiri ya Injili.

Injili maana yake ni “habari njema” ya kusamehewa dhambi. Je, unaeneza “habari mbaya”. Kama unakiri na kutubu dhambi za nchi yako, basi unatoa ujumbe kwamba Mungu ametuma ugonjwa huu kwa sababu ana hasira kwa sababu ya dhambi zao – kwa jinsi hiyo ina maana kwamba sala zako zitaondoa dhambi zao, kwa sababu kile alichofanya Kristo Kalvari hakikutosha kuwa ondoleo la dhambi zao!

Na ukumbuke kuwa virusi vya corona ni vya ulimwengu mzima, je utaomba kwa ajili ya dhambi za ulimwengu mzima, ili kusamehewa, kana kwamba Yesu hakufa!

  1. KUHUBIRI INJILI.

Sasa ni nini kilichobaki kwa mwenye dhambi kufanya? Kilichobaki kwa mwenye dhambi kufanya ni KUAMINI Injili na kutubu mwenyewe dhambi zake. Msamaha umekwisha tolewa bure na Mungu kwa watu wote kupitia Kristo. Ndiyo maana Kristo anasema, “Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye”. (Yohana 3:17). Hii ndiyo habari njema! Hivi ndivyo tunapaswa tuwahubirie wanaume na wanawake! Kama Paulo anavyosema, “…tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, NI MIZURI KAMA NINI MIGUU YAO WAHUBIRIO HABARI YA MEMA.” (Warumi 10:14-15). Kanisa linapaswa kuutangazia ulimwengu ya kuwa Kristo alikwisha kufa kwa msamaha wa dhambi. Ni kwa kuhubiri Injili ambako kutaongoza wanaume na wanawake kwenye toba majira haya.

Bwana Yesu alisema, “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.” (Mathayo 28:18). Huu ndio ukweli tunaopaswa kuuelewa na kuuishi kwao. Yesu amepewa mamlaka yote – mbinguni na duniani! Je, huu ndio ufahamu wetu tukizingatia kile kinachotokea ulimwenguni hivi sasa? Katika Zaburi tunaelezwa maneno hayo, “Semeni katika mataifa, BWANA ametamalaki.” (Zaburi 96:10). Huu ni ujumbe, kwamba – Bwana anatamalaki! Huu ujumbe ni kwa moyo wako, kwa ufahamu wako, na kwa nchi zote – Bwana anatamalaki. Tena neno la Mungu linatangaza kuwa, “Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.” (Zaburi 47:8). Chochote kinachotokea ulimwenguni, huu ndio ukweli. Ibilisi hatawali juu yote. Ibilisi anaweza tu kupofusha mioyo ya wasioamini (2 Wakorintho 4:4) na kufanya kazi katika maisha ya wenye dhambi (Waefeso 2:1,2), lakini ni Mungu ambaye juu ya yote na anayetawala. Unaamini hivyo? Unaamini ukweli huu moyoni mwako kadiri unavyoenenda siku hadi siku? Usiishi kwa kufikiri kwamba nguvu fulani imetia laani katika maisha yako au katika nchi unapoishi kwa sababu ya covid-19! Huu ni ushirikina, siyo imani. Usiishi kwa hofu ya kile kinachoweza kutokea. Ukiishi kwa hofu, utapatwa na madhara makubwa kuliko yale ya virusi! Yatupasa kumwamini Mungu na neno lake. Nazungumzia hili zaidi mwisho wa somo hili

  1. CHINI YA AGANO LA KALE.

Kwa sababu ya mchanganyiko unaosababishwa na kushindwa kutofautisha Agano la Kale na Agano Jipya, hebu tuzingatie mambo yalivyokuwa katika Agano la Kale. Ni wazi kwamba chini ya Agano la Kale Israeli kamwe hawakuambiwa kukiri ama kutubu kwa ajili ya dhambi za taifa lolote la kipagani. Hapana mfano wa jinsi hii wala maelekezo ya Mungu ya kufanya hivyo. Na huu ni ukweli katika Maagano yote mawili, yaani la Kale na Jipya. Wakati Wayahudi wakiwa mateka Babeli, hawakukiri ama kutubu kwa ajili ya dhambi za Babeli. Wakristo walipokuwa Roma hawakuingia katika mambo ya kukiri ama kutubu dhambi za dola ya Kirumi. Kufanya jambo la namna hii ni kufanya jambo ambalo halikuamriwa na Mungu, jambo ambalo halina mfano wake katika Biblia. Baadhi ya watu hufanya hivyo siku hizi, lakini haileti matokeo kwa sababu hakuna kusudi la Mungu ndani yake, na kufanya hivyo kwa sasa ni kutokuelewa Injili na matokeo ya kifo cha Kristo pale msalabani.

Kwa huzuni na uchungu wa majanga asilia waumini wengine wanaanza kumuomba Mungu asamehe dhambi za nchi yao, lakini hii itakuwa ni kuongozwa na hisia, wala siyo neno la Mungu. Pasipo kufikiri Biblia inafundisha nini hasa, watu hufikiria jinsi Israeli walivyokiri na kutubu dhambi zao, na OVYOOVYO kulichukulia hali hiyo katika mazingira ya sasa. Kama tulivyoona, Israeli kamwe haikukiri ama kutubu kwa ajili ya dhambi za taifa lingine la kipagani, ambalo halikuwa na uhusiano wa Agano na Mungu.

Yona alipoenda Ninawi, hakulazimika kukiri na kutubu dhambi zao! Bali ALIHUBIRI NENO LA MUNGU kwao, na walipokwisha kusikia neno la Mungu WALITUBU WENYEWE DHAMBI ZAO. Hivyo kama unataka kuona watu wakiokolewa na kubarikiwa, hubiri neno la Mungu, hubiri Injili ya Yesu Kristo.

Kama unataka toba kwa watu wa nchi yako, basi wahubirie Injili, na uombe Mungu alete watenda kazi kwa ajili ya mavuno hayo!

Watu wa Israeli walijihusisha na kutubu dhambi walizozitenda wenyewe, wala siyo dhambi za watu wengine ama mataifa mengine. Ni muhimu kwetu kuelewa muktadha wake. Kwanza, wakati Mungu anawaongoza Israeli kuelekea nchi ya ahadi, ALITANGULIA KUWAONYA kupitia kwa Musa kuhusu ADHABU ambayo wao, au taifa lao, wangepata endapo wangemgeuzia kisigo maagano na kutumikia miungu mingine (Kumb. 28), na katika Mambo ya Walawi 26 Mungu anafafanua kwamba hukumu yake kwao ni kurejeza mioyo yao kwake. Na endapo kwa hukumu ya awali wasigelitubu, Mungu angeleta hukumu zaidi juu yao.

Na katika kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati sura ya 6 na 7, Sulemani anachukua wazo hili kumuuliza Mungu kama angelisamehe kama wangejishusha mbele za Mungu na Madhabahu yake huko Yerusalemu kwa kukiri na kutubu dhambi zao – na Mungu angesikia sala yake.

La pili, wakati Israeli walipomgeuzia kisogo Mungu, Mungu aliwatumia manabii kuwaeleza wazi kuwa wametenda dhambi na kwamba hukumu ilikuwa juu yao. Hivyo Israeli hawakuachwa pasipo kujua Mungu alikuwa anafanya nini, na kwa sababu gani alifanya hivyo. Hivyo Israel hawakuhitaji KUBAHATISHA ili kujua kwa nini kulikuwa na hukumu. Mungu aliweka wazi kwa kuwaonya Israeli kabla hayajawakuta, na hata wakati yalipowakuta, Mungu aliweka wazi kwa nini yalitokea.

Na hivi ndivyo Mungu anavyofanya na anavyosema siku hizi katika Agano Jipya? Hapana, haitokei kwa njia hii.

Na tutambue kuwa Israeli haikuachwa gizani kuhusu hukumu ya Mungu. Yote tuliyoyaeleza yanaihusu Israel kama taifa chini ya Agano la Kale. Lakini hata ilipokuwa chini ya Agano la Kale, Israeli kamwe haikufunzwa kukiri ama kuomba kwa ajili ya dhambi za mataifa ya wapagani, ama kuambiwa wafanye hivyo kwa ajili ya taifa lolote walikoishi. Hakuna mfano wala maelezo kutoka kwa Mungu ya kufanya hayo. Huu ni ukweli, katika Agano la Kale na Agano Jipya.

Katika Agano Jipya, wale ambao sasa wamezaliwa mara ya pili kwa Roho wa Mungu wamekuwa maskani ya Mungu katika Roho (Waefeso 2:22). Tumekuwa hekalu la Mungu (1 Wakorintho 3:16) na tumekuwa warithi wa Mungu (Warumi 8:17; Wagalatia 4:7). Yesu ametukomboa kwa damu yake, watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa (Ufunuo 5:9). Sisi ni kanisa lake, mwili wake, na yeye ni kichwa cha kanisa lake! Hili kanisa lake linajumuisha watu wote aliowakomboa ulimwenguni kote na haliwakilishwi na taifa la duniani. Kwa damu yake Kristo Yesu alitukomboa kutoka katika laana ya Torati (Wagalatia 3:13).

Huwezi kuingiza Agano la Kale ndani ya Agano Jipya kana kwamba Yesu hakufa! Hakuna chochote katika Agano Jipya kinachoonyesha kwamba Mungu angekemea au kuhukumu watu wake, dhambi zao, kupitia majanga ya asili. Lakini kumbuka kanisa ni la ulimwengu mzima. Ni makosa makubwa na si kibiblia kufikiri eti wewe ni mkristo unayeishi katika nchi fulani, kwamba Mungu atakwenda kushughulika na nchi yako kama alivyofanya kwa Israeli! Hakuna kinachoonyesha kuwa Mungu alifanya hayo kwa taifa lolote la kipagani. Hakuna chochote katika Agano Jipya cha kutuwezesha kufikiri hayo. Zaidi ya hayo Israeli iliwakilisha watu wa Mungu kama taifa moja. Wakristo katika taifa lolote wanaweza kujikuta kwenye nchi iliyojaa watu wasioamini. Huwezi kulinganisha wala kuchanganya Agano la Kale na Agano Jipya.

Hili ni tatizo lililomsumbua kwa mfululizo Paulo, tatizo la walimu wa uongo waliojaribu kurudisha nyuma Wakristo katika Agano la Kale kwa kufikiria njia za kutenda mambo!

  1. MAELEZO ZAIDI KUHUSU MAJANGA NA HUKUMU.

Wote tunafahamu kwamba Mungu alileta mafuriko kama hukumu kwa ulimwengu siku za Nuhu, na pia alituma moto kuteketeza Sodoma na Gomora. Katika matukio hayo Mungu aliwajulisha watumishi wake kabla hayajatokea (Nuhu na Ibrahimu).

Hukumu nazo zilitangazwa na manabii mbali mbali (kama Amosi, Obadia, Nahumu nk) dhidi ya mikoa na nchi ambazo ziliitendea Israeli ukatili. Pia tunajua kuwa Yesu Kristo alitabiri kuangushwa kwa mji wa Yerusalemu kwa sababu Wayahudi walimkataa kuwa Masihi wao. Hili lilitokea mwaka 70 BK.

Hata hivyo, WAKATI HUO Injili inahubiriwa huko hakuwa na mfano wa kufahamika wala sauti ya Mungu haikusikika kurudia habari hiyo. Ilikwisha kusemwa na Kristo na maandiko matakatifu. Kristo alituambia kwamba kutakuwa na “matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni” (Luka 21:11), na kwamba TUSITISHWE NA MAMBO HAYO. Tunajua kuwa kabla ya kurudi kwa Bwana: “kutakuwa ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa yakishangaa, kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake……Hapo ndipo watakapomwona mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.” (Luka 21:25, 27).

Hukumu yao wasioamini haikawii wala uvunjifu wao hausinzii. (2 Petro 2:3). Tunajua kuwa, “…wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika na uweza wake; katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasitii injili ya Bwana wetu Yesu Kristo;…yeye atakapokuja kutukuzwa katikati ya watakatifu wake…” (2 Wathesalonike 1:7,10). Na twajua ya kuwa, “mbingu na nchi zimewekwa akiba kwa moto hata siku ya hukumu na kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.” (2 Petro 3:7). Kitabu cha Ufunuo kinatueleza pia kuhusu hukumu na hasira ya Mungu itakayomwagwa juu ya dunia.

Ujumbe wa msingi nyakati hizi za kuhubiri Injili na za kanisa, ni kwamba hukumu ijayo ni juu yao waliokataa Injili ya Yesu Kristo. Imekwisha tabiriwa na kutamkwa na Mungu. Hivyo kuona kila majanga ya asili kuwa ni hukumu ya moja kwa moja kutoka kwa Mungu dhidi ya dhambi za nchi fulani na dhambi yake haina uthibitisho wa kibiblia. Inavuruga ujumbe wa Injili na kile alichosema Mungu kuhusu hukumu ijayo.

Hivyo tunapaswa kukumbuka kwamba, “Bwana haikawii kutimiza ahadi yake,…bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba. (2 Petro 3:9)

Kwa sasa bado tumo katika nyakati za kuhubiriwa kwa Injili, hivyo tusidharau uzuri na rehema za Mungu zinamuongoza mtu kwenye toba, kama Paulo asemavyo, “Au waudharau wingi wa wema wake na ustahamili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu? (Warumi 2:4).

Mwisho, kama tulivyokwisha ona, Mungu akitaka kuihukumu nchi ambayo siyo Israeli, mara nyingi hutangaza hukumu yake wazi wazi mapema. Mungu hajawahi kuipiga nchi KWA HUKUMU YA GIZANI – bila kupata onyo ya mapema kutoka kwa Mungu. Mungu ni nuru, na HUONGEA KWA WAZI WAZI NA KWA HAKI kuhusu hukumu zake, kwa watu wake na kwa mataifa. Tusichukulie kana kwamba Mungu hatendi haki kuliko alivyokuwa kabla ya kumtuma mwanawe kufa Kalvari! Tusimfanye Mungu kana kwamba siyo mwadilifu kwa kupendekeza kuwa ataleta hukumu ghafla kwa taifa bila kutoa maelezo yoyote. Lakini kama tulivyokwisha ona, muktadha huu unailenga Israeli chini ya Agano la Kale tu. Na mambo hayo hayana mfano wake katika Agano jipya.

  1. KUHUSU KAZI YA SHETANI.

Tunapaswa kujua pia kuwa katika Agano la Kale hakuna majanga ya asili yaliyoipata Israeli yanayoweza kuhusishwa na Ibilisi. Mungu mwenyewe aliwaambia Israeli kwamba ndiye Yeye atakayepeleka juu yao njaa nkd kama wakianza kuitumikia sanamu. Shetani hatajwi kuwa chanzo cha majanga ya asili – si katika Agano la Kale wala Agano jipya. Je, waweza kuwa na mfano mmoja wa Biblia ambapo shetani anatajwa kuwa chanzo cha majanga ya asili ambayo yameathiri nchi fulani, ama ulimwengu? Kwenye 1 Mambo ya Nyakati 21:1-21, Shetani alimshawishi Daudi kuwahesabu Israeli – kwa maneno mengine, alimjaribu Daudi kutegemea nguvu ya kibinadamu badala ya kumtegemea Mungu. Lakini ndiye Mungu aliyetuma hukumu dhidi ya Israel na siyo Shetani!

Lakini yako mambo ambayo shetani anahusika na maandiko yako wazi juu ya hilo – lakini hapana anapodaiwa kuhusika na majanga asilia katika nchi yoyote au duniani. Hivyo unapoomba dhidi ya majanga ya asili kwa sababu unaamini kuwa ni kazi ya ibilisi, nani kakwambia ni kazi ya ibilisi? Kama majanga yanaruhusiwa na Mungu kwa makusudi yake, basi utakuwa unaomba ukipingana na kile alichoruhusu Mungu. Hiki ndicho unachotaka kufanya? Na kama utawaambia watu au kuwafundisha kuwa majanga ya asili ni kazi ya ibilisi, na kama sivyo, je, wataka kumpa umaarufu na nguvu asizostahili? Wataka kuwatia hofu watu, na kufanya ionekane kuwa ibilisi anazo nguvu za ushindi kuliko Mungu – hasa unapopita muda mrefu bila janga kutoweka?

Katika maisha haya ni nadra kupata au kutokupata kabisa sababu za kiroho za kwa nini mambo fulani hutokea. Hili ni jaribu kubwa la kiroho – hasa yanapokuja mateso tusiyojua sababu yake. Katika hali isiyo ya kawaida maandiko yanatupa ufahamu wa sababu za kiroho kwa nini Ayubu aliteseka kwa maumivu sana. Sasa, tunajua kuwa Ayubu aliteswa vikali na Ibilisi, lakini neno la Mungu linaweka wazi kuwa hili lilitokea kwa sababu Mungu aliliruhusu; aidha, tunatambua kuwa Mungu aliruhusu hili KWA MAKUSUDI YAKE!

Makusudi gani ya Mungu?  Kwanza, kuwaonyesha watu wote, na falme, mamlaka na wakuu wa giza hili katika ulimwengu wa roho kuwa mtu anampenda Mungu kuliko kitu chochote. (Waefeso 3:10). La pili, ni kuimarisha imani ya muumini ili amfahamu Mungu kwa kina, na kuwa na uhusiano wa karibu naye. (Ayubu 42:5).

Haya yote yanampa Mungu utukufu.

Kumbuka Bwana anasema nini kwa waumini wa Kanisa la Smirna dhidi ya yule ambaye Bwana hamtuhumu, isipokuwa anawashauri akisema, “usiogope mambo yatakayokupata; tazama huyo ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.” (Ufunuo 2:10).

Tunaona wazi tena, Mungu akiruhusu ibilisi kufanya mambo ambayo yatatimiza kusudi la Mungu. Sasa ni kwa kiasi gani Mungu anaruhusu Ibilisi avuruge nguvu za asili na hata kusababisha majanga, siwezi kusema kwa sababu maandiko yenyewe hayasemi. Je, Ibilisi ndiye aliyesababisha tufani katika Ziwa la Galilaya Yesu alipokuwa amelala katika mashua? Kama ndiye ama siye, Yesu aliituliza tufani, na wanafunzi hawakuwa tena hatarini. Lakini tunafahamu kuwa Mtume Paulo aliharibikiwa na meli mara tatu na bado Mungu alimuokoa. Inastaajabisha kuona kwamba hata kama Ibilisi anaonekana kuwa nyuma ya matukio mabaya yanayochafua uasili wa dunia, lakini Biblia haimtaji yeye kuwa chanzo chake.

  1. MITAZAMO AMBAYO BADO INANBAKI KUTOKA KWA UTAMADUNI WA UCHAWI.

Tatizo kubwa ni kuwa baadhi ya Wakristo wanajaribu kubahatisha Mungu anafanya nini. Wanajaribu kutafsiri matukio kana kwamba hawawezi kuishi pasipo kujua sababu, kwa nini mambo haya yanatokea. Baadhi ya mambo haya chimbuko lake ni uchawi, yanatokana na utamaduni wa uchawi – watu bado wana fikra za kichawi. Baadhi ya watu hufikiri kwa njia hii: Mambo mabaya yanayotokea katika mazingira yako. Lazima yawe ya kichawi, ni nguvu za ibilisi. Kuna aliyetia laana juu yako kupitia kwa wachawi. Hivyo huogopa. Unatafuta hirizi au nguvu zaidi za kiroho ili kudhibiti na kuangusha nguvu za pepo wabaya. Usipofanikiwa kuondoa hiyo hali mbaya, ina maana kuwa yule mwovu na nguvu za giza amekushinda na hauko salama. Pasipo kugundua hili, huu ni msingi wa fikra za Wakristo kadhaa. Huu ni ushirikina. Siyo mambo ya kibiblia. Ngoja nikupe mfano rahisi. Mama mmoja wa kikristo alifika kazini, na mtu mmoja akamsemesha hivi: “Mbona una huzuni na mashaka leo?” Yule mama mkristo akajibu. “Oh, kuna jambo baya limenitokea, nina hakika ni Mungu ananihukumu.” Hii ni hadithi ya kweli. Hizi siyo fikra za Biblia. Hii inatokana na mtazamo wa kishirikina. Alijuaje ya kuwa Mungu alikuwa akimwadhibu? Hakujua! Anabahatisha tu! Mungu hakuongea naye juu ya dhambi fulani yake. Tatizo la fikra zake ni kuwa alifasiri hali mbaya iliyomfika kuwa ni hukumu ya Mungu kwake. Hakumwendea Mungu na kumngoja. Hakuzingatia neno la Mungu katika Maandiko. Kama jambo baya likimkuta, hii ni hukumu ya Mungu, na adhabu! Hiyo ni mantiki ya giza! Hivyo ndivyo alivyodhani. Kufikiri mara moja namna hii ni kutembea gizani, ni ushirikina. Na ndivyo watu wengi wanavyofikiri – kwa kweli pasipo kuja kwa Mungu, pasipo kumngoja, na kuzingatia neno lake.

Na hivi ndivyo watu wengi wanavyochukulia hii hali ya sasa – pasipo kujua au kisikia lolote toka kwa Mungu, wao MARA huamini kuwa majanga ni ya ibilisi, ama wanahitaji toba kwa kuwa ni hukumu ya Mungu! Kuna wahubiri wengi ambao hawasaidii katika hali kama hii. Kinyume chake wao wanachockea fikra hizo za ushirikina bila kujali Biblia inasemaje.

Ni picha mbaya kiasi gani tunayoona tunapodhani kuwa Mungu ni kama mtu aliyejificha kwenye ukingo gizani ambapo hatuwezi kumwona, na anaweza kuruka ghafla akatoka na kutupiga, kisha haraka akaruka tena kujificha gizani bila ya maelezo yoyote! Hivyo bila sababu ya kufanya hivyo tukadhani, tukaanza kufikiri kuwa anatuhukumu tokea mbali katika ukingo wa giza, kisha tunaanza kutubu kwa hofu….lakini tunatubu kwa lipi? Watu wengine wanafikiri vivyo hivyo moyoni mwao, yaani, wanafikiri Mungu anafanana na tabia ya namna hiyo na matendo ya namna hiyo! Hili ni giza, huu ni ushirikina. Huyu siyo Mungu wetu.

Nikifanya lililo baya Mungu anaweza kunihakikisha kwa habari ya kosa au dhambi yangu kwa neno lake, au kwa Roho matakatifu dhamirini mwangu. Yeye ni Baba yangu. Ni Baba yako kama umekombolewa kwa damu ya mwana Kondoo. Na tuenende katika nuru ya neno lake, na siyo katika giza la ujinga na ushirikina.

Hebu na tujikumbushe ya kwamba Wakristo katika Matendo ya Mitume 11 hawakufanya hivi hata mara moja. Ufahamu wao ulikuwa tofauti. Walikubali ukweli kwamba njaa ilikuwa inakuja, na ilionekana kwamba Mungu aliwaambia kuhusu hili hivyo waliweza kutoa michango kwa waumini maskini wa Uyahudi. Ni ukweli wa kibiblia kwamba kutakuwa na majanga ya asili bila maelezo maalumu ya hukumu yake wala dhambi za taifa husika.

  1. MAJANGA YA ASILI NA JINSI YA KUYATAFSIRI.

Nataka kuangalia Biblia inasema nini kuhusu majanga ya asili yanayotokea duniani, ili kuona kuwa tunaweza kupata ufahamu wa kutusaidia. Kwanza kabisa nanukuu Yesu alisema nini katika Mathayo 24:14: “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Ndiyo maana nimesema tumo katika wakati wa neema ya habari njema. Habari njema itahubiriwa katika ulimwengu wote kabla ya huo mwisho. Tunachojali hapa ni haya matukio asilia ya hapa duniani kabla ya huo mwisho, na siyo hayo yatakayotokea Yesu atakaporudi, na hukumu ambayo wote wataiona wakati ule.

Sasa tuangalie zaidi katika Mathayo sura ya 24. Wanafunzi walimuuliza Yesu kuhusu dalili za kuja kwake na za mwisho wa duniani, na hivi ndivyo Yesu alivyosema, “Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; ANGALIENI MSITISHWE; maana hayo HAYANA BUDI kutukia; lakini ULE MWISHO BADO. KWA MAANA taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na tauni na matetemeko ya nchi mahali mahali.Haya yote ndiyo MWANZO WA UTUNGU” (Mathayo 24:6-8). Jambo la kwanza muhimu tuliloona ni kuwa Yesu anayataja haya majanga kwa kusema kuwa “hayo HAYANA BUDI kutukia”. Hatoi sababu wala kufafanua kwa nini yatatokea, isipokuwa anasema, ‘hayana budi kutukia’. (Biblia ya Swahili SUV imekosa kuweka neno ‘tauni’ katika mstari wa 7 lakini lipo kwenye Luka 21:11, na karibu maandiko yote ya Kigiriki yanalo neno ‘tauni’ katika Mathayo 24:7).

Fahamu kuwa mstari wa saba unahusiana na mstari wa sita, kama unavyoona mstari wa saba unaanza na neno, “kwa maana”, ukionyesha kuwa kuna mwendelezo wa matukio kati ya mstari wa sita na saba. Kuongezea kwa habari ya vita, kutakuwa na njaa na magonjwa au tauni na matetemeko seheme mbali mbali! Yesu alitutabiria hayo, lakini pasipo bila kufafanua kwamba yatatokea kama hukumu mahsusi kwa watu mahsusi. Basi sisi tusibuni sababu wala kubahatisha sababu!

Ni nini ujumbe wa Yesu kwako ama kwangu kuhusu haya majanga? Hapa kuna jambo la pili muhimu kufahamu. Alisema kwamba, “angalieni msitishwe”. Umesoma neno hili? Yesu anatueleza kuwa vita na majanga vitakapotokea yatupasa tuangalie. Tuangalie nini? Angalieni MSITISHWE NA MAMBO HAYO! Je, huu ndio mtazamo wako juu ya baa za namna hiyo zinapotokea? Kama siyo, kwa nini siyo? Au je, huu ndio ufahamu ulio nao leo kuwa inapotokea tauni kufikirii mara moja kuwa ni hukumu ya Mungu juu ya nchi, au ibilisi amechukua nafasi kushinda makusudi ya Mungu? Je, huu ndio matazamo wako na fikra zako? Je, unapenda kumwamini na kumtii Yesu au wataka kufuata hisia zako au baadhi ya wahubiri ambao hawafundishi kusudi lote la Mungu ( Matendo ya Mitume 20:27) Yesu amepewa nguvu zote za mbinguni na duniani, na ametwambia mapema kuwa mambo haya yatatokea hivyo tusihangaike mioyoni mwetu! Jina lake litukuzwe!

Jambo la tatu muhimu kujua ni kuwa tunapoongea juu ya matukio yote haya, Yesu anasema, ‘mwisho bado’. Hii ina maana gani? Ina maana kuwa hazungumzii kipindi cha muda mfupi ambapo mambo haya yanatokea. Ana maana gani anaposema kuwa mambo hayo ni ‘mwanzo wa utungu’. Yaweza kuwa na maana kwamba aina hii ya ‘utungu’ yaweza kuongezeka kadiri tunavyokaribia mwisho. Au ukiangalia mstari unayofuata, baada ya mstari wa saba, Yesu anazungumzia mateso ya waumini na dhiki itakayowapata. Kwa maneno mengine majanga asili ni mojawapo ya hiyo ‘dhiki’ na yanafuatiwa na mambo yatakayoleta dhiki kwa waumini kwa sababu ya mateso na kusalitiwa.

Haijalishi ni kwa jinsi gani unafasiri maelezo haya ya ‘mwanzo wa utungu’, muhimu ni kuwa Yeye aliye juu ya yote anatueleza mapema kuwa mambo haya yatatokea. Hakuna cha kushangaza kwa Mungu. Mungu hajapoteza uwezo wake. Anafanya mambo yote kwa makusudi yake na kwa mapenzi yake. Ukweli huu utatufariji na kututia moyo.

Watu wanaokiri na kutubu kwa ajili ya dhambi za nchi wanazoishi kwa sababu ya majanga ya asili, wanapuuza ushuhuda wa maandiko ya neno la Mungu. Nakushauri usome maandiko tuliyorejea katika somo hili ili yapate kukuongoza. Yataleta nuru na uzima nafsini mwako.

Mwisho katika somo hili la majanga ya asili yanayoelezwa hapa, napenda kuleta wazo katika baadhi ya mistari ya Biblia yenye kuleta maana ya pamoja. Haya ni mawazo yangu nataka nikushirikishe kama yanaweza kukufaa.

Adamu alipotenda dhambi iliadhirika dunia nzima (Mwanzo 3:17,18). Mambo hayako sawa kabisa katika dunia hii!

Kuvunjika kwa uhusiano wa Mungu na mwanadamu kunaakisiwa katika mabadiliko ya nje ya dunia.

Kwa mfano, kulikuwa na njaa katika Agano la kale ambayo haikuhusiana na hukumu za Mungu juu ya dhambi yoyote (Mwanzo12, 26 na 41). Tumekwishataja jinsi Yesu alivyosema kuhusu majanga ya asili kama ‘utungu’, na utungu huo utakuwepo hadi mwisho. Neno hili ‘utungu’ katika lugha ya asili ya Kiyunani ni sawa na “maumivu machungu”, hasa uchungu wa mwanamke anapojifungua mtoto – kama ilivyotumika katika 1 Wathesalonike 5:3 wakati Paulo anazungumzia uharibifu wa ghafla utakaoikumba dunia siku ya mwisho. Anasema, “Wakati wasemapo kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo, kama vile UTUNGU umjiavyo MWENYE MIMBA, wala hakika hawataokolewa.” Neno hili ‘utungu’ katika mstari huu ni sawa na lilivyotumika katika Mathayo 24:8 – tofauti ya hapa limetumika kama kitenzi na siyo nomino. Na katika Wagalatia 4:19 Paulo anaelezea juu ya maombi yake kwa Wagalatia tena anatumia neno hili kama kitenzi linalokuwa na maana ya ‘kuvumilia uchungu kama anayejifungua’. Paulo anasema, “Vitoto vyangu, ambao kwamba NAWAONEA UTUNGU tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.” Alikuwa na hofu juu ya Wagalatia WALIORUDISHWA NYUMA NA MTAZAMO WA FIKRA ZA AGANO LA KALE na kukaribia kupoteza imani ya kweli katika Kristo. Anasema anawaombea tena akilinganisha maombi yake na utungu wa kuzaa! Hivyo neno hili, ‘utungu’ linapotumika, hutumika kueeleza uchungu unaovumiliwa ili kupata kilicho bora. Utungu una kusudi litarajiwalo mwisho.

Na tunakutana na neno hili tena katika Waraka kwa Warumi,

“Kwa maana viumbe vyote (au ‘kiumbe chote’) pia vinatazamia KWA SHAUKU NYINGI KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU…kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa KATIKA UTUMWA WA UHARIBIFU, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote (au ‘kiumbe chote’) pia vinaugua pamoja, navyo VINA UTUNGU PAMOJA HATA SASA.” (Warumi 8:19-22). Tunaweza kutafsiri kwa maneno ‘viumbe vyote’ au ‘kiumbe chote’. Sasasawa na lugha ya Kigiriki, tafsiri zote mbili ni sawa.

Paulo anasema kuwa viumbe vyote (kiumbe chote) viko chini ya vifungo na uharibifu. Hii inatukumbusha kitabu cha Mwanzo 3:17,18, ambacho nimeinukuu hapo juu – na kutokana na kifungo vinaugua navyo vina utungu hata sasa. Lakini kwa nini vina utungu na kuugua – ni kwa lengo gani? Na matarajio gani? Paulo anatueleza kuwa uumbaji UNASUBIRI UFUNUO WA KWELI NA MWISHO WA MWANA WA MUNGU ILI KUTOLEWA KATIKA UHARIBIFU NA VIFUNGO. Akirejea wakati wa mwisho kama tunavyoweza kuona tukisoma mstari ya 23 hadi 25 wa Warumi 8.

Mistari hiyo ya waraka kwa Warumi siyo rahisi kuelewa na kufasiri, watu wana mitazamo tofauti juu ufasiri wao. Siyo kwamba naomba ukubaliane nami kuhusu kifungu hiki cha Warumi, lakini natumaini kuwa utaona ni kwa jinsi gani kifungu hiki kinaendana na mistari nyingine katika Biblia. Ukubali ama usikubali na ninachosema kuhusu kifungu hicho cha Warumi, japokuwa tumeona kwenye vifungu vingine kuwa Biblia inatupa picha jinsi dunia inavyougua kwa uharibifu. Kuna mambo hayako sawa katika dunia. Tunajua kuwa yalitokea mabadiliko ambayo ni matokeo ya dhambi ya Adamu. Sasa dunia ina utungu.

Inawezekana kabisa ishara nyingi za huo ‘utungu’ zinaweza kuwa majanga ya asili ambayo Yesu ameyaeleza katika Mathayo 24.

Kutokana na mistari hiyo na nyingineyo tuliyoona, itakuwa wazi kuwa kuanza maombi kwa ajili ya dhambi za nchi tunazoishi, ama kuomba dhidi ya ibilisi kila yatokeapo majanga ya asili ni jambo lisilo na msingi wa kibiblia nyakati hizi za neema ya Injili.

Kama ilivyoonyeshwa hapo juu, majanga ya asili ama “huzuni” ambayo Yesu anaizungumzia katika Mathayo 24 inaweza kuongezeka kadri tunavyo karibia siku ya kurudi kwake. Zaidi ya hayo, wangepata mabaya kuliko. Hivyo kuna haja kubwa kwetu tuwe na shina na msingi katika neno la Mungu, kiasi kwamba tusiwe na mchanganyiko, kukata tamaa na kuogopa, kiasi kwamba hatudanganyiki na kufanywa mateka wa kila mhubiri wa uongo anayejiita nabii.

Bila shaka siku hizi kutakuwa na wahubiri wanaodai kwamba Mungu ametuma ujumbe kwa kanisa. Tayari nimesikia wahubiri wawili ambao wanasema Mungu amewapa ujumbe kwa kanisa kuhusu virusi vya corona na hukumu zingine zitakazokuja. Lakini hawasemi mambo sawa! Tukumbuke kwamba wakati wanafunzi walimuuliza Yesu juu ya nyakati za mwisho, jambo la kwanza Yesu alilosema ni, “JIHADHARINi, MTU ASIWADANGANYE…” (Mathayo 24: 4). Yesu alikuwa akituonya kwamba kutakuwa na wadanganyifu wengi ambao watajaribu kupotosha watu na madai wanayojifanyia wenyewe na juu ya mambo yatakayotokea (Mathayo 24: 23,24).

Tunajua kwamba kabla tu ya Bwana kurudia mambo makubwa yatatokea ambayo yataathiri dunia nzima na wote wanaoishi ndani yake, na Yesu alisema kuwa isipokuwa siku hizo zilifupishwa, hakuna mwili ambao utaokolewa. Vitu hivyo havijakuwa lengo la somo hili kwa sababu siku hizo bado ziko mbele yetu na inawezekana zisiwe mbali sana.

Msomaji wangu mpendwa, ujumbe wa Yesu ulikuwaje kwetu kuhusu siku za mwisho? Jambo la muhimu alilokuambia wewe na mimi ni, “IWENI TAYARI, kwa kuwa katika saa kama vile hamfikirii Mwana wa Adam atakuja … Basi kesheni, na muombe kila wakati …” (Mathayo 24:44; Luka 21:36). Usiruhusu wahubiri wakukoseshe hisia zako na ujaze mawazo yako juu ya vitu vitakavyokuja! Kilicho muhimu ni kwamba wewe na mimi tunaishi kila siku katika uhusiano wa karibu na Yesu Kristo, ili wakati atakapokuja uwe tayari kukutana naye!

  1. JINSI TUNAVYOPASWA KABILIANA NA MAMBO HAYO – USHUHUDA WETU.

Sasa ningependa kuongelea ni jinsi gani sisi kama Wakristo siku hizi tunapaswa kukabiliana au kushughulisha na hali hii ya virusi vya corona. Tunawezaje kuwa katika hali hii? Kwanza kabisa tunapaswa kutofautiana na mtazamo wa kidunia. Kama watu wa Mungu tunapaswa kufahamu kuwa tunapitia mambo mengi yale yale wanayopitia watu wengine. Inakuwa hivyo. Kama isingelikuwa hivyo, Mungu angewezaje kuonyesha ulimwengu na enzi zote na mamlaka kwamba amefanya maajabu ndani yetu, hata kutufanya tuwe tofauti na wale wanaotuzunguka? Mengi yanatokea kwetu, lakini hayatutii uchungu, ugumu au hofu na mahangaiko. Kama watu wa Mungu, tunapaswa kutofautiana na watu wengine wasioamini katika mtazamo wetu na jinsi tunavyoshughulisha na mambo hayo.

Kinachomtukuza Mungu ni imani yetu kwake – hili ni jambo muhimu kuliko yote. Ukitaka kujua likupasalo kufanya basi mtumaini Mungu, Baba yako, moja kwa moja.

Bwana alisema , “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na Mimi”. (Yohana 14:1). Unamwamini Mungu kwa namna hii? Unamwamini yeye katika hali hii ya sasa, kiasi kwamba huna majonzi na mahangaiko moyoni? Unayo amani kwa sababu unafuata neno la Mungu lisemalo kwamba, “mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.” (1Petro 5:7). Tuna ahadi kubwa kiasi gani katika neno la Mungu: “Aketiye mahali pa siri pake aliye juu atakaa katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.” (Zaburi 91:1,2). Je, umeketi mahali pa siri pake Mungu unapoyatoa maisha yako kwake? Ninajuaje kama namtumaini Mungu? Unajua kwa ile amani akupayo: “Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.” (Isaya26:3).

Imani yetu ambayo ni matokeo ya hivyo amani ni ya dhamani zaidi kwa Mungu kuliko dhahabu, hata kama inajaribiwa kwa moto. (1Petro1:6,7). Uhusiano wako na Mungu ni wa muhimu zaidi kuliko mambo yote mengine. Endapo hali hii ya virusi vya corona inakufanya uhangaike kiasi cha kuchanganyikiwa na kupoteza amani na furaha katika Bwana, tayari umeshindwa katika vita, na utapoteza jambo muhimu katika maisha yako ambalo ni uhusiano wako wa karibu na Mungu. Kwa kadiri ya imani yetu kwa Mungu na uhusiano wetu na Mungu ulivyo, woga, au kuogopa kitu chochote ni tishio kubwa kuliko virusi vya corona. Tukitekwa na woga majira haya, basi virusi vya corona tayari vimetupiga, mbali na tahadhari zote tulizochukua kujikinga na ugonjwa huo.

MUNGU HAKUTUITA ILI KUJUA AU KUELEWA KILA KITU, wala kujua chanzo cha kila kitu. ALITUITA ILI TUMTUMAINI YEYE KABISA, hasa tusipoelewa yanayotokea. Hii ndiyo imani iliyo ya kweli na ya dhamani mbele za Mungu. Hebu na tukumbuke ni jinsi gani linatuagiza: “Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako” (Mithali 3:5,6). Usitegemee akili zako! Hizi ni mistari ya ajabu sana na zitayaongoza moyo wako na maisha yako – na ya kwangu pia. Kataa kuongozwa na kutawala na akili yako ili upate majibu ya kila kitu. Mtumaini Bwana. Ndiyo wote tuna maswali, lakini hatuachilii akili zetu zituongoze ama kutusumbua eti kwa sababu hatujui chanzo cha yanayotokea!

Kama nilivyosema, kumtumaini Mungu na kuwa na amani moyoni si jambo la kujitakia baraka, bali ndilo jambo linalomtukuza Mungu.

Kama wewe ni mtoto wa Mungu, unajua kuwa uhai wako umefichwa ndani ya Kristo katika Mungu? (Wakolosai 3:3). Ni kweli ya ajabu gani hii! Ni mambo makuu kiasi gani Mungu ametutendea kupitia kufa na kufufuka kwa mwanawe! Tunajua na kuelewa kama watoto wa Mungu kwamba maisha yetu yamo mikononi mwa Mungu (Zaburi 31:15). Kama umekombolewa na Yesu Kristo, wewe ni WAKE, na yeye ni mwamba wako na ngome, makao yako na usalama wako. (Zaburi 18:2; Wakolosai 3:3; Warumi 835-39; 1 Petro 3:13). Kuyapata haya maishani huhitaji sala ndefu. Kupata usalama huu katika kipindi hiki ya corona virusi huhitaji kukimbia kwenda mhubiri fulani ili upate usalama huo kupitia sala ndefu yake! Haya ni mambo ambayo Mungu mwenyewe tayari ametenda kwa ajili yetu kupitia Yesu Kristo. Baraka hizo za amani na furaha kimsingi lazima kutokana na uhusiano wako na Mungu. Endelea kushika neno la Mungu, na kumwamini yeye. Huhitaji mhubiri wa kuomba kwa sauti kuu, kwa nusu saa, ili upate amani na usalama katika Kristo. Tayari haya ni mambo ya kweli kwa Kristo, na ndani yake.

Tunapaswa kuishi kwa imani kwa neno la Mungu, wala SIYO KWA MSISIMKO WA MAHUBIRI yanayoamsha hisia katika mikutano. Lakini mhubiri na awajaze watu wa Mungu na neno la Mungu kwa wakati huu. Tunahitaji kuwa na tumaini na imani ISIYOTOKANA NA HISIA ZILIZOAMSHWA KWA KITAMBO KIDOGO NDANI YA MIKUTANONI, bali iwe tuamini na imani inayotoka kwa kumwamini Mungu na neno lake siku hadi siku. Inatupasa kuishi kwa imani, wala si kwa hofu au kwa hisia.

Unaamini hivi hata kama janga hili lisipoondoka haraka? Au unaamini kwamba sasa ibilisi ametawala na ameshinda kwa sababu janga linazidi kuenea? Kama hivi ndivyo, basi mawazo yako siyo sahihi. Maandiko yanasemaje, “Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake (Yesu)…ila twamwona Yesu …amevikwa taji ya utukufu na heshima” (Waebrania 2:8,9). Je, hivi ndivyo uonavyo kwa macho ya rohoni, kwamba Yesu amevikwa taji la utukufu na heshima? Je, hii ni kweli ambayo mioyo yetu inaikumbatia na ambayo inatutia moyo na kutupa amani mioyoni mwetu? Mungu na mwanawe wako katika kiti cha enzi – hakuna mwingine. Litukuzwe jina lake!

Na Isaya anatangaza yafuatyo: “Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye HABARI NJEMA, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye AUTANGAZAYE WOKOVU, Auambiaye Sayuni, MUNGU WAKO ANAMILIKI!” Huu ndio ujumbe wetu kwa wengine na kupitia huo pia tunaweza kuwatiana moyo sisi kwa sisi!. Na Paulo anathibitisha hiyo anaposema, “Simameni, hali mmefungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani.” (Waefeso 6:14,15).

Mioyoni mwetu tunapaswa kuishi maisha juu sana na wala siyo haya yanayotuzunguka – tuishi kumuona yeye asiyeonekana kwa macho. Paulo anasemaje kuhusu magumu tunayoyapita katika maisha haya? Anasema hivi: “Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, BALI VISIVYOONEKANA. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele”.(2 Wakorintho 4: 17,18). Kama unatazama na kuishi kwa mambo yanayoonekana utakata tamaa, kuhuzunika na kuchanganyikiwa. Tunapaswa kuwa na mtazamo sahihi na kuishi kwa mambo yasiyoonekana, tukimtazama Yesu.

Yesu ametuambia kwamba tusiwaogope hao wauao mwili kisha hawawezi kufanya kiingine zaidi. Alisema kwamba Mungu pekee ndiye tunayepaswa kumwogopa, kwa sababu ana uwezo wa kuangamiza mwili na roho (Luka 12:4,5). Mstari wa 4 inaonekana mahsusu ikizungumzia mateso, lakini pia ndio ukweli kwa ujumla. Hatupaswi kumwogopa Ibilisi bali kumpinga na mashauri yake. Hatupaswi kuogopa kile ambacho mwanadamu anaweza kututenda. Hatupaswi kuishi na hofu ya virusi vya corona. Tunapaswa “kuogopa Mungu.” Kuogopa Mungu, maana yake ni kumwamini, kumheshimu na kutii neno lake kuliko kitu kingine chochote. Hofu ya Mungu inatuongoza kujiepusha na uovu, na ndio mwanzo wa hekima, na ufahamu; lakini pia inatupatia ujasiri wa kweli, na kuwa salama ndani ya Mungu (Zaburi 111:10; Mithali 8:13; 14:26; 16:6). Hii siyo hofu inayotufanya tujifiche mbali na Mungu katika miti kama Adam na Eva walivyofanya, kwa sababu tunadhani Mungu anataka kutuhukumu muda wowote. Hapana. Kuogopa Bwana ni unyenyekevu, kuyatoa maisha yetu kwa Mungu tukimheshimu yeye na neno lake kuliko vyote. Huku kumwogopa Bwana ndio chemchemi ya uzima (Mithali 14:27)!

Ngoja niseme ya kwa kwamba hakuna chochote ninachoandika kumshawishi mtu amjaribu Mungu. Nina maana gani hapa? Maana yangu ni hii, kwamba Ibilisi alinukuu maandiko kumjaribu Yesu ili ajitupe chini toka juu ya hekalu (Luka 4:9-12). Ibilisi alijaribu kumwambia Yesu kwamba hapaswi kuogopa hatari yoyote kama yeye ndiye mwana wa Mungu, hivyo alimjaribu Yesu ili ajirushe. Yesu alikataa. Aidha, tunasoma katika Yohana 7:1 kuwa Yesu hakutaka kutembea Uyahudi. Kwa nini? Kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua. Unaona? Katika mambo aliyoyafanya Yesu alijali hali ya mazingira yake – isipokuwa kwa kusudi maalumu Mungu huzizuia ili kutimiza mapenzi yake. Mungu hakufanya kimiujiza kila mara ili kumlinda kutokana na hatari ya mazingira yake. Mara kwa mara Yesu alitembea katika muktadha wa mazingira ya wakati husika. Hii inatufundisha nini? Inatufundisha kwamba hatupaswi kuongozwa kwa kujiaminisha katika dini za uongo ambazo moja kwa moja kufikiri kuwa, “Mimi ni mtoto wa Mungu, sihitaji kuogopa hatari hii ama ile, Mungu atanilinda kwa lolote nifanyalo.” Hii inawakilisha majaribu ya Ibilisi. Yesu alipojaribiwa na Shetani ajitupe chini toka juu ya hekalu alijibu, “imeandkiwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Vivyo hivyo tunapaswa kuishi sawasawa na neno la Mungu na siyo kwa imani feki.

Ukiniuliza ‘imani feki’ ni nini, na nikueleze kwa mfano ufuatao: Kama mtu fulani (haijalishi ni nani) akidai na kufundisha kama usipokwenda kanisani kwa sababu ya corona virusi huna imani ya dhati, unakosea sana! Sasa kama ukienda kanisani kwa sababu ya maneno ya yule mtu ili uonekane una  imani ya kweli kwa Bwana, ndipo imani yako ni batili. Imani yako haitokani na uhusiano wako na Mungu bali inatokana na maneno au fundisho la mtu anayetaka kukuaminisha imani kadiri ya mawazo yake. Kwenda kanisani haimanishi unayo imani ya kweli. Unapaswa kuishi sawasawa na imani uliyo nayo mwenyewe mbele ya Mungu, na ndipo ukienda kanisani (au usipoenda) utakuwa na amani inayotokana na Mungu mwenyewe. Usishi sawasawa na sheria ya mtu.

Siwezi, na sitaweza kutoa mwongozo kwamba ufanye hiki au usifanye kile kipindi hiki cha virusi vya corona. Bali ninakushirikisha ukweli wa kibiblia na kanuni zitakazotuongoza katika kufikiri na kutenda. Maamuzi tunayopaswa kufanya kila siku siyo mepesi, hivyo tunapaswa kuenenda kwa unyenyekevu mbele ya Mungu na kwa kuomba hekima na neema.

  1. NENO LA MWISHO

Ni nini matokeo makubwa ya mtu aliyeingia katika Agano la Jipya? Kulingana na neno la Mungu, ni kwamba wote tunapaswa kumjua Mungu, kuanzia mdogo hadi mkubwa (Waebrania 8:8-11). Mungu atukuzwe! Ndiyo maana nimeandika somo hili. Watu wanaibiwa ufahamu wa neno la Mungu, kwa hao wahubiri na manabii wasiolisha kundi kwa neno la Mungu. Badala yake, WANAAMSHA HISIA ZA WATU kwa kuhubiri kwa sauti kubwa na kujaza mioyo na akili za wasikilizaji toleo lililoharibika la mawazo ya Agano la Kale linalowaingiza gizani.

Yesu Kristo alikufa kwa ajili yetu ili kutuleta katika uhusiano wake na yeye na Baba! Uzima wa milele ni kumjua Mungu (Yohana 17:3). Yatupasa kumjua alivyo. Yatupasa kuijua amani, faraja na furaha ya kumjua Mungu. Amina.

© David Stamen  2020.        somabiblia.com

 

Comments are closed.

 
%d bloggers like this: