RSS

NAYAHESABU MAMBO YOTE KUWA NI MAVI, ILI NIMPATE KRISTO.

“NAYAHESABU MAMBO YOTE KUWA NI MAVI, ILI NIMPATE KRISTO”

Je, ikoje kwako wewe juu ya jambo kama hilo? Huo ni mtazamo wako kwa dhati?

Nilifundisha juu ya ukweli huo kwa wanachuo kikuu na nilizingatia hata Digrii (Shahada) yangu chini ya kichwa ya mambo ya ‘mavi’. Wengi wao walishtuka. Na baada ya kipindi kile kiongozi wa vijana alinijulisha kuwa wanachuo hawakupenda nitumie lile neno ‘mavi’! Sasa hapo ikawa ni zamu yangu kushtuka! Nilimwambia wanachuo wale baadae kuwa ‘Mavi’ ni neno la kibiblia! Na kwamba alikuwa ni Roho wa Mungu aliye mwongoza Mtume Paulo kulitumia NENO HILO katika muktadha huu! Mungu analitumia neno hilo KWA UTHABITI WA MAKUSUDI HAYA. Yaani, kutuonyesha sisi kuhusu mtazamo au fikra zetu zinavyopaswa kuwa kwa mambo mengine yote ya kidunia pale tunapoyalinganisha na mambo ya kumjua Kristo. Na Paulo aliyahesabu kuwa ni mavi! Na ni nini hasa muktadha wa habari hii katika sura ya Wafilipi sura ya 3. Hapo mtume Paulo alikuwa anaongelea kuhusu MALEZI yake aliyokulia nayo pamoja na ELIMU yake kama Mfarisayo, lakini kisha anaendelea kusema kuwa anayahesabu MAMBO YOTE kuwa kama MAVI ili kwamba AMPATE KRISTO YESU. Je, tunaweza kushuhudia lilelile?

Kuna maneno mengi nyakati hizi za leo yahusuyo mtu kuwa na “malengo”, “goli” au “maono” kwa ajili ya maisha yake, au kuwa na fikra chanya au mtazamo nzuri, na mara nyingi sana watu wasemapo mambo hayo huzungumzia mambo yahusuyo hapa duniani, mambo ya kimwili na mafanikio ya biashara na siyo ya kiroho.

Mtume Paulo anasema, “natenda NENO MOJA tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, NIKIYACHUCHUMILIA yaliyo mbele; NAKAZA MWENDO, niifikilie MEDE YA THAWABU YA MWITO MKUU WA MUNGU KATIKA KRISTO YESU.” (mistari 13,14). Hiyo ndiyo SHAUKU KUBWA ya mtume Paulo, na ndilo lengo lake lenye utukufu! Hiyo ndiyo ‘goli’ yake na ‘mtazamo nzuri’ wake!

Anasema, natenda neno moja TU! Unaona hapo! Jambo MOJA tu ndilo lililokuwa LINASUKUMA maisha yake; alijidhughulisha na GOLI KUU MMOJA; katika maisha yake ALIFILISIWA NA TAMAA KUBWA MNO, ili “amjue YEYE, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, akifananishwa na kufa kwake.” (mstari 10).

Je, hilo ndilo lengo lako? Je, hilo ndilo lengo lako KUU? Je, unayahesabu mambo yote kuwa kama sio kitu kwako, NI KAMA MAVI, ukiyalinganisha na kumjua Kristo? Je, moyo wako unakuambiaje? Kwa hiyo Mungu mwenyewe anatangaza, “Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ANANIFAHAMU MIMI, NA KUNIJUA, ya kuwa mimi ni Bwana.” (Yer.9:23,24).

Je, tunampenda Bwana kuliko mambo mengine yote? Ni nini inayokusukumu katika maisha yako? Unafilisiwa na shauku ya namna gani? Moyo wako unakuambiaje?

Au unafikiri kuwa mambo haya yalikuwa tu kwa ajili ya mitume pekee? Hapana! Ebu basi usikilize mstari unaofuatia baada ya hapo, “Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo.”

Paulo anatuhamasiha na kutuhimiza tuwe na mtazamo uleule ambao alikuwa nao! Huo ndio matazamo unaofaa!

Bwana Yesu alisema ukweli huu, “lakini kinatakiwa KITU KIMOJA TU, na Mariamu AMELICHAGUA fungu lililo jema, ambalo HATAONDOLEWA.” (Luka 10:42). Je, umelichagua fungu lipi kama kipaumbele katika maisha yako? Je, unafilisiwa na mtazamo upi maishani mwako?

Kama unataka kutimiliza kusudi la Mungu kwako hapa duniani na ile ya umilele, basi ndipo inakupasa uwe na mtazamo (attitude) uleule ambao ulikuwemo kwa mtume Paulo. Ukilinganisha na kumjua Yesu Kristo na uweza wake katika maisha yako, basi mambo yote mengine ni kama mavi.

Nilimaliza masomo yangu ya Chuo Kikuu mwaka 1975. Miezi michache tu baadae Digrii (Shahada) yangu ya Chuo Kikuu ilipoletwa nyumbani sikuwepo nyumbani. Rafiki yangu mmoja alinipigia simu akinipasha habari kuwa Cheti changu cha Digrii kimewasili. Nilimwambia yule ndugu kuwa, “Weka hayo mavi kabatini.” Hii ni hadithi ya kweli.

Sasa, mimi siidharau Digrii yangu, hata kidogo. Ninamshukuru Mungu sana kwamba aliniwezesha kufaulu mitihani yangu. Lakini ile Digrii yangu haikumaanisha chochote kwangu binafsi, yaani, haikunifanya mimi nionekane ni mtu wa tofauti na wengine, na wala haikunifanya nijisikie, au hata nianze kufikiri kuwa mimi ni mtu wa maana zaidi kuliko mtu mwingine. Kulinganisha na kule kumjua Yesu, haikumaanisha kitu chochote kile kwangu. Ile digrii haikunibadilisha mimi kwa namna yoyote ile iwayo, wala mimi siwaangalii watu wengine kwa namna ya utofauti eti kwa sababu tu ninayo digrii, kuwadharau watu wengine eti kwa sababu tu ninayo digrii – hii ingekuwa ni dhambi.

Digrii yangu itapita, lakini kumjua Yesu kwa dhati na nguvu ya ufufuo wake ndani yangu ni kitu ambacho hakitapita kamwe. Kumjua Kristo, kumpenda na kumtii yeye ndilo jambo pekee linaloweza kunibadilisha kwa namna inayompendeza Mungu. Nikiyafikiria yale yote ambayo Kristo aliyonifanyia, moyo wangu wenye shukrani utamfikiria Yeye tu, na kumjua yeye kuwa ni hazina kuu niliyonayo ambayo hailinganishwi na kitu chochote cha duniani hapa, iwe ni elimu yangu au cheo ambacho naweza kuwa nacho katikati ya watu wengine!.Mtume Paulo anasema, “Nayahesabu mambo yote kuwa kama mavi.” Je, dhamira yako inashuhudia ukweli huo maishani mwako?

TAFADHALI USINIELEWE VIBAYA. Unaona, mavi nayo yanafaa – mavi hutumika kama mbolea. Hivyo ninazo shukurani mbele zake Mungu kwamba Shahada yangu ya Chuo Kikuu ilinisaidia kupata kazi! Ukweli huo tunaoongelea kwenye somo hili haumaanishi kwamba hatujali wajibu na majkumu ya masomo, ya kazi, ya biashara nkd zetu hapo duniani – hapana, hata kidogo, ni kinyume chake. Aidha, najua wengi wanajitahidi sana waweze kwenda Chuo Kikuu ili wapate kazi nzuri na sisemi chochote dhidi ya hiyo! Lakini kama tukifanya ‘Jambo moja’ kama Paulo alivyofanya, ndipo tutakuwa na uhakika kuwa Mungu atatuongoza katika NYAKATI ZAKE kwa mambo ya hapa duniani yahusuyo kile tunachokwenda kukifanya katika maisha yetu nyakati zijazo. Kwa sababu imeandikwa, “Maana tu KAZI YAKE, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo TOKEA AWALI Mungu aliyatengeneza ILI TUENENDE NAYO.” Na tena, Mungu “ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, SI KWA KADIRI YA MATENDO YETU sisi, BALI KWA KADIRI YA MAKUSUDI YAKE yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele.” (Waefeso 2:10; 2 Tim.1:9).

Ndiyo, Mungu atatuongoza katika maisha yetu kuhusiana na kile tunachosomea na aina ya kazi tutakayoipata. Mambo haya yote ni mazuri na ni ya lazima  – lakini uwe mwangalifu kwamba malengo yako kwa ajili ya mambo hayo yawe yanayotokana na nema yake Mungu itendayo kazi katika maisha yako, ili kwamba usipoteze kusudi lake Mungu mwenyewe katika maisha yako – yote kwa pamoja hapa duniani na hata umilele.

Basi, kwa hiyo, UNAFISILIWA na tamaa YA NAMNA GANI? UNAPATWA NA shauku YA NAMNA GANI? UNASUKUMWA na MALENGO YAPI katika maisha yako? Je, unayahesabu mambo yote kuwa mavi ili upate Kristo? Je, umepatwa na shauku kumjua Yesu na nguvu Yake katika maisha yako KULIKO MAMBO YOTE na goli yote na ndoto zote nyingine? Moyo wako unakuambiaje?

Kama lengo lako na shauku yako kwa ajili ya mambo ya dunia hii vinapita  lengo lako na shauku yako ya kumjua Yesu Kristo, basi jihadharini usipoteze ya ile ya pili PAMOJA NA ILE YA KWANZA! Baraka za dhati za Mungu katika kila sehemu ya maisha yetu zinatokana NA UHUSIANO WETU NA MUNGU – “Utafuteni KWANZA ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.”

© David Stamen 2018

 

Comments are closed.

 
%d bloggers like this: