UTOAJI NA KIKIUMI / JAMBO LA UNYONYAJI
KUSIKILIZA, BONYEZA JINA LA JUMBE HAPO CHINI. UKURASA MWINGINE UTAFUNGUA, NA JUMBE UTAANZA.
JUMBE USIPOANZA, BONYEZA MSHALE WA KUSHOTO ( WA KWANZA > ).
KUDOWNLOAD / KUPAKUA JUMBE, KUBONYEZA MSHALE WA MWISHO ∇.
UTOAJI NA KIKUMI / JAMBO LA UNYONYAJI
NAFTAL OBONDO KISSIRI
August 24, 2014 at 8:02 am
naomba kuelimishwa zaidi kuhusu maana halisi ya kikumi
dsta12
August 24, 2014 at 4:00 pm
Unaweza kusoma makala juu ya Huduma na Pesa hapa:
https://somabiblia.com/je-unataka-kubarikiwa-na-kuwa-mtu-mwenye-mafanikio/
Au kusikiliza jumbe juu ya: Pesa: Sadaka au Biashara hapa:
Nategemea itakusaidia kwa kiasi!
robeson
August 2, 2015 at 7:48 pm
mungu ni msaada wetu
ELIYA WILLIAM
August 11, 2015 at 11:27 am
nime elewa jambo fulani
elly mdeka
May 10, 2016 at 10:57 pm
Tupo pamoja,nami ni mjumbe wa habari hizo hizo.sasa nahubiri habari hizo kupitia huduma urejesho na upatanisho.ningependa kuwa pamoja nanyi
dsta12
May 11, 2016 at 12:39 pm
Mpendwa Elly,
Nafurahia maneno yako, Elly, kwani siyo wengi wanaokubali na jumbe zangu! Sasa, je, unaweza kuniambia unahudumia sehemu gani ya Tanzania na kunieleza zaidi juu yako na jinsi tunavyoweza kuwa pamoja. Kwa neema ya Mungu mimi nitakuja Tanzania tarehe 20 Mai mwezi huo na nitakaa Dar Es Salaam kwa kama wiki mbili, baada ya hapo nitakwenda Morogoro kwa wiki moja. Je, unayo facebook page?
Wako katika Yesu Kristo,
David
Thobias Laizer Laizer
May 31, 2016 at 7:40 am
Haleluya haleluya namshukuru Mungu wangu kwa kunipa uzima siku ya leo maana sio kwa nguvu zangu kuwepo leo
pia namshukuru Mungu kwa kunipa kibali nguvu na urejesho kutoka dhambini sasahivi nahubiri Injili yake MWOKOZI bila woga wala wasi wasi ye yote
namshukuru pia Mungu kwakunipa ukumbusho kuhusu tovuti hizi. maana nimda mrefu sijatembelea kujifunza nk lakini week hii nimeanza kutembelea kujifunza nk
Devid nakupa ukweli sio kwamba watu hawaikubali Injili yako wanaikibali sana lakini misingi za makanisa zetu ulimwenguni hazijengwi KIROHO zinajengwa kimwili ndio maana unaona kuuondoa ktk kile wanachoamini ni vigumu mnoo
nimejaribu kufuatilia masomo haya kwa njia ya sauti nimeanza kuielewa lengo lako nanamuomba Mungu sana siku moja tukutane tunene neno la UZIMA uso kwa uso unajua ktk bara letu la Africa watu weupe wametunyonya sana ndio maana tukiwaona kwa vyovyote vile tunawapenda midomoni tunawatii kimwili tunawapa tabasamu la nyuso zetu ili tupate walicho nacho lakini mioyoni mwetu hatuwataki kwasababu tu ya tabu na shida unyonyaji wao waliouonyesha huko mwanzo
wskatuona sisi waafrica km wapumbavu wasio na akili nk wakatunyonya km kope ndio maana watu kuamini Injili yako ningumu kwa sababu tu ya ngozi yako lakini nasema km mjumbe wa Kristo ipo siku wataikibali unajua siku hizi makanisa mengi ni biashara wapo kimaslai ya kiuchumi sio kuponya faida kwanza ndio maana tumekuwa waoga na watumishi wa ng`ambo mm nakuambia ukweli sio kwamba hatutaki Injili au sio kwamba hatuikubali tunaikubali ila tumevunjwa moyo na wanadamu mtu anakuja anapokelewa baada ya mda anaanza kuonyesha ufisi wake kuwanyanyapaa wenyeji alowakuta
kisa tu ametoka mbali hiyo ndio ukweli kutoka Africa sio mawazo yangu lakini chunguza utapata Jibu lake misingi ya mwanzo ya mtu mweupe iliharibu misingi ya sasa haijali anakuja kwa njia gani ni sawa namtumwa wa dhambi za dunia Yesu KRISTO akamwokoa nilazima ajipe mda wakuvunja misingi ya mwanzo iliokuwa ikimuharibia uhusiano yake na Mungu wale waliokuwa wanamjua hawamwamini haraka wataanza kumchunguza kwanza je amebadilika kweli au ni uzushi tu Mungu awe pamoja nawe
Kanuni Kayombo
August 23, 2016 at 12:13 pm
Naitwa Pastor kanuni Kayombo city harvest international dar esalam Tanzania nimebarikiwa sana na somo lako naamini kwa sasa Kanisa limeanza kupona ,karibu sana kanisani kwangu ili uweze kufundisha masomo yako na tu ujenge mwili wa Kristo pamoja
Projestus Benezeth
March 17, 2020 at 12:49 pm
Amen, nimebarikiwa sana juu ya kile nilichokitafuta muda mrefu.