RSS

JUU YA MAFUNDISHO YA WAADVENTISTA WASABATO

HAPA UTAWEZA KUSOMA JUU YA MAFUNDISHO NA HISTORIA YA WASABATO NA KULINGANISHA NA MAFUNDISHO YA BIBLIA NA INJILI YA KWELI.

BOFYA SOMO UPENDALO:

*ORODHA YA MAFUNDISHO MAKUU YA UONGO YA WAADVENTISTA*

KUHUSU YA MAFUNDISHO YA WASABATO: TUKUSANYIKE SIKU GANI?

HISTORIA YA WASABATO NA MAFUNDISHO YAO.

MISTARI YA MSINGI

KUSUDI LA MAAGANO LA MUNGU

INJILI YA YESU KRISTO

ARTICLES IN ENGLISH:

LIST OF THE MAIN FALSE TEACHINGS OF SDA

HISTORY AND ERRORS OF THE TEACHINGS OF THE SDA

IS SDA A CULT

TESTIMONIES OF PASTORS AND OTHERS WHO CAME OUT OF SDA PLUS VIDEOS CONFRONTING SDA TEACHING.

TO READ AN EXCELLENT INTRODUCTION TO SDA TEACHING AND OTHER MATERIAL , CLICK ON THE LINK OR IMAGE:

EXADVENTIST.COM     

YOU CAN FIND MORE TEACHINGS BY CLICKING ON THE LINK BELOW:

UNAWEZA KUPATA MAFUNDISHO MENGI ZAIDI YA KUSOMA NA KUSIKILIZA KWENYE:

www.kuomba.com

                                             KWA MAWASILAANO / CONTACT TEL.:  (+255) 0672215533

MASWALI NA MAJIBU 12 JUU YA MAFUNDISHO YA WASABATO

Niliuliza maswali 12 kwenye Facebook group ‘Mjadala wa Biblia baina ya Wasabato, Wakatholiki, Waprotestant na Walokole’ (2017). Hapo chini ni majibu (na maelezo kwenye p.10) ya Msabato Allen John (administrator mmoja wa FB Group hiyo) juu ya mafundisho ya Wasabato:

 1. William Miller, Hiram Edson na Ellen White walitazamia Yesu atarudi duniani Oktoba 22 1844.

Jibu – Ni KWELI.

 1. Watu hawa watatu (pamoja na wengine) walikata tamaa sana baada ya hiyo haikutokea.

Jibu – NI KWELI

 1. Muda mfupi sana baada ya hapo Hiram Edson alisema iliwekwa dhahiri kwake kwamba sio kuwa ilimbidi Yesu kurudi duniani Oktoba 22, 1884, lakini siku hiyo Kristo alitoka patakatifu mbinguni na kuingia patakatifu pa patakatifu ili kufanya kazi iliyo takatifu zaidi.

Jibu – Ni KWELI.

 1. Ellen White alifundisha vile vile, yaani, Oktoba 22, 1884 Kristo alitoka patakatifu mbinguni na kuingia patakatifu pa patakatifu ili kufanya kazi iliyo takatifu zaidi.

Jibu – NI KWELI

 1. Ellen White alifundisha dhambi za waumini zimehamishwa kwenye vitabu vilivyopo patakatifu pa patakatifu. Kwa hiyo ni lazima kusafisha patakatifu pa patakatifu.

Jibu- NI KWELI lakini ni Dhambi za Waumini waliotubu.

 1. Ellen White alifundisha Yesu alianza kazi ya “Hukumu ya Uchunguzi” (Inestigative Judgement) tarehe Oktoba 22, 1884 mbinguni ili ‘kusafisha’ patakatifu pa patakatifu.

Jibu – NI KWELI

 1. Kazi ya “Hukumu ya Uchunguzi” ni kazi ya kuchunguza maisha ya waamini (kwa kusoma vitabu) na kuamua ni nani anastahili kwa sababu ya kutubu kwake kwa kweli na kukua katika neema!

Jibu – NI KWELI

 1. Kazi hiyo ya “Hukumu ya Uchunguzi” inaendelea mpaka sasa.

Jibu – NI KWELI

 1. Baada ya kumaliza kazi hiyo ya “Hukumu ya Uchunguzi”, Yesu atarudi duniani.

Jibu – NI KWELI

 1. “Kila mtu atahukumiwa kulingana na nuru aliyopewa na KAMA ULISIKIA UKWELI na kwa kusudi UKAPUUZA HAKIKA HAUWEZI KUOKOLEWA. Mpaka kufika nyakati za Mwisho kabisa kabla ya Yesu kuonekana injili itahubiriwa kwa nguvu na kila mtu atasikia ukweli juu ya Sabato. WALE WATAKAOPUUZA NA KUIKATAA NURU KWA KUSUDI HAWATAOKOLEWA.” (Allan John).

 

 1. Ellen White alifundisha juu ya hukumu ya Mungu wenye dhambi na wasioamini hawatateseka kwa milele.

Jibu – NI KWELI

 1. Ellen White alidai kupitia ndoto yake aliingia patakatifu pa patakatifu na aliona amri kumi zimeandikwa kwenye mbao mbili na zilikuwa ziking’aa sana, na moja ilikuwa iking’aa zaidi, na ndio inayozungumzia Sabato, yaani, amri ya nne.

Jibu – NI KWELI

Sawasawa na mfundisho ya wasabato, ni sawa kusema SHARTI mmoja ya kuokolewa ni lazima ushike sabato baada ya kusikia mafundisho yao. Ukikataa kwa kusudi kuyashika mpaka mwisho (baada ya kuyasikia), hutaokolewa, hata kama unadai wewe ni mkristo. Hapo tunaweza kuona utimilifu wa undanganyifu wao.

 

Comments are closed.

 
%d bloggers like this: