RSS

Mambo Machafu kwenye Internet

“Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.”

Mto wa uchafu unatiririka toka kwenye mtandao (internet) na kwenye luninga na shetani anautumia ili kuangamiza maisha, hasa kukamata watu wakiwa bado vijana. Ni rahisi sana kwa mtu yeyote siku hizi kuona uchafu wa hali ya juu kwenye mtandao. Picha za ngono (pornography) za kwenye mitandao ni kama dawa za kulevya tu ukishaanza kuzitazama, utataka kufanya hivyo zaidi na zaidi na hutoweza kuacha. Shetani anakuwa amekuweka kifungoni. Ni kama tu watu ambao hawawezi kuacha ulevi muda wote. Hata kama utataka kuacha, hutaweza! Shetani anataka tabia hii iendelee kwa vijana ili kwamba iote mizizi kwao na aweze kuyaharibu maisha yao mapema na afanye  ishindikane kwao kuwa  huru tena – isipokuwa kwa nguvu na wokovu wa Mungu kupitia kwa Yesu. Picha za ngono za kwenye mtandao ni sumu ya  kiroho! Sumu hii haiathiri mwili wako (sio kwa kuanzia) lakini moyo wako, akili na roho! Itaangamiza maisha yako ya kiroho. Zinajaza akili yako na mawazo machafu naa mawazo haya yanapelekea kufanya matendo machafu na dhambi (basi, itaathiri mwili wako!). Sababu nyingine kwa nini picha za ngono mtandaoni ni hatari ni kwamba picha ile unayoiona inaweza kukaa akilini mwako, ikakuchafua hata baada ya kutoka mtandaoni! Sio kitu ambacho tunaweza kucheza nacho kabisa! Si kitu ambacho unaweza kukiangalia kwa ‘mara moja moja’ (hakuna ‘mara moja moja kwenye sumu!) – ama kuziangalia wakati unapokuwa unajisikia kushuka ama kujaribiwa. Hatutakiwi kuziangalia kwa wakati wowote. Hata  mara moja! Kabisa! Hatutakiwi kutembelea tovuti hizo – zitakuchafua. Zitakuua kiroho. Kwa njia ya kuziangalia picha hizi pepo wanaingia maisha yako. Ni kama tu watu wanaotumia madawa ya kulevya, kama utafungwa kwenye picha hizi za ngono ni jambo ambalo haliwezekani kuwa huru tena – isipokuwa kwa kwa neema na nguvu ya Yesu Kristo!

Sababu iliyonifanya kuandika kuhusiana na hili ni kwamba kifungo hiki  ni kama kifungo cha kutumia madawa ya kulevya – hata kama Mungu akikusamehe na kukupa neema ya kuzishinda, vishawishi bado vitakuja, hata vishawishi vikubwa, na utahitajika kukimbilia kwa Bwana kwenye moyo wako wote na kugeukia kwake na kumwamini yeye kwa moyo wako wote ili uwe msafi na huru. Vishawishi si dhambi. Lakini nayasema haya kwa sababu ninafahamu wakati mwingine vijana wanaweza kufikiri vishawishi vinaweza kuwa na nguvu sana na hatuwezi kuvipinga. Hatutakiwi kujisalimisha kwa mawazo haya. Hatutakiwi kuvipa nafasi vishawishi kwa mara nyingine! Neno la Mungu linatufundisha, “jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.” (1 Wakor.10:13).  Amini hivi, chochote kile akili yako ama shetani anachokwambia, amini neno la Mungu, mwamini Mungu. Shetani, ama hata tamaa zako mwenyewe kutaka kustarehe ama kutimilizwa ama raha, zitakupelekea kufikiri kwamba unajaribiwa kuliko kiwango kile unachokiweza. Neno la Mungu linasema kuna neema ya kushinda kwa sababu ya kile Yesu alicokifanya pale msalabani! Kupitia Yesu tumewekwa huru mbali na dhambi hivyo hatuitumikii dhambi tena ama kuiacha dhambi iyatawale maisha yetu:

“..mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;…mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki….Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki..” (Warumi 6:6,18,12,13)

Tunapokuwa tunajaribiwa tunatakiwa kutambua kile kitu Mungu amefanya kwa ajili yetu na kuamini neno lake, “Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.” (1 Yoh.3:8). Na kupitia kwa Kristo tunatakiwa kufisha vishawishi vyetu vinavyotupelekea kutenda dhambi, “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;” (Wakol.3:5).

Hili ni swala muhimu sana. Kama unasoma haya na ulikuwa humjui Yesu Kristo na wokovu wake, na kama unaangalia picha za ngono kwenye mitandao ama huangalii, unahitaji kutubu na kumuomba Kristo akusamehe dhambi zako kama unataka maisha ya kweli sasa na ya milele; na ujue hili, Yesu Kristo ndiye pekee anayeweza kukusafisha na kukufungua toka katika uchafu wako – kwa sababu kama uko kwenye kifungo cha picha za ngono mitandaoni ama la, utakuwa na uchafu kwenye moyo na akili yako. Ama unadhani wewe ni Mkristo lakini unadhani kwamba si vibaya kuangalia picha za ngono mtandaoni, ama dhamira yako haikushitaki unapoziangalia, ama kujisikia vibaya moyoni mwako kwamba kwa namna hiyo unafanya dhambi. Hii inawezekana kabisa kwamba unayo dini na siyo Yesu Kristo. Inawezekana kabisa kwako Ukristo ni kitu cha ‘nje’ tuu na hakipo ‘ndani’! Ama labda umekuwa ukidanganywa na watu wa dini ama makuhani. Umekuwa ukiambiwa ya kuwa kama ukienda kanisani, ukashika sheria fulani na kuamini mambo fulani, basi umeokoka na wewe ni Mkristo. Ama hata umekuwa ukiambiwa kwamba unatakiwa kuungama dhambi zako kwa kuhani basi dhambi zako zitakuwa zimesamehewa na mambo yote yatakuwa sawa! Unahitaji kuendelea kwenda kwa kuhani kila juma na dhambi zako zitakuwa zimesamehewa! Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wanadanganyika na mafundisho haya. Maisha yao hayajabadilikaa kwa ndani. Maisha yao yana tofauti ndogo sana ama hayana tofauti kabisa na watu wengine ambao wanaishi duniani. Kama dhamira yako haikuhukumu, na moyo wako kukosa amani kwa kuangalia picha za ngono mitandaoni, basi Roho wa Mungu hayumo ndani yako. Unahitaji wokovu ambao Kristo pekee ndiye anayeweza kukupa! Dhehebu haliwezi kukuokoa. Dhehebu haliwezi kukusafisha na kukuweka huru mbali na dhambi! Mwana wa Mungu pekee ndiye awezaye kufanya hivyo na unahitaji kuja kwake, na kutubu mbele zake na kutaka msamaha wa kweli toka kwake, kwa kweli kusafishwa moyo wako na kuwekwa huru mbali na dhambi! Unahitaji kupokea Roho ambayo inatoka kwa Mungu ili ikutie nguvu kuishi kama vile ambavyo Yesu aliishi! Mungu huangalia moyo na anajibu maombi yetu endapo tu tutatoa ‘matunda ya toba ya kweli’ – “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, ‘Tunaye baba, ndiye Ibrahimu’ ”. Haitoshi tu kuwa mtu wa dini! Unahitaji kuujua wakovu ambao Yesu anautoa! Yesu alikufa msalabani ili kukata mizizi ya dhambi kwenye maisha yetu na ili tusiitumikie dhambi tena. ( Luka 3:8,9).

Kwa wakristo ni wazi kwamba hatutakiwi kuangalia picha za ngono mitandaoni – hatutakiwi hata kuwa na shauku ya kufanya hivyo. Mzigo uliomo moyoni mwangu ni kukwambia kamwe usitoe nafasi kwa vishawishi kwa kuangalia mambo machafu. Usiiruhusu nafsi yako iangukie katika dhambi hii. Huu sio mchezo. Itayaharibu maisha yako; mzigo wangu uko hasa kwa vijana kwa sababu picha za ngono mitandaoni ni mtego mbaya sana na ni ngumu kutoka nje yake na maisha yote yanaweza kuharibiwa kwa sababu yake! Kimbilia kwa Yesu. Neno la Mungu linasema, “Naye, (Yesu Kristo), aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.” (Waebarania 7:5). Haya ni maneno mazuri ya ahadi. Yesu huokoa KABISA wale wamjiao Mungu kupitia kwake. Na kaka, Yesu anatuombea mimi na wewe bila kuacha! Anaweza kukuokoa toka kwenye dhambi hii ama dhambi nyingine yoyote. Asifiwe Mungu kwa wema na nguvu zake! Ikimbie dhambi na utafute utakatifu (“..ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.) na uatakatifu, kwa sababu kama unavyojua, bila ya utakatifu hatutaweza kumuona Mungu, “Tafuteni KWA BIDII kuwa na …huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao.” (Waebrania 12:14 ) Unaweza kuona ni kwa jinsi gani hili lilivyo la msingi. Shetani anajaribu kukamata waamini na hata wale waliomo kwenye kazi ya Mungu ili aangamize utendakazi wao katika ulimwengu huu na kuharibu maisha yao kama waamini. Mpinge shetani naye atakukimbia – hili ndilo Biblia inatufundisha (Yakobo 4:7).

Mungu alimuonesha Ezekieli kile watu wake,hata viongozi wa dini , walichokuwa wanakifanya kwenye mawazo ya akili zao katika eneo takatifu hekaluni. “Unayaona wanayoyafanya, yaani, haya machukizo makubwa wanayoyafanya nyumba ya Israeli hapa, hata niende zangu mbali na patakatifu pangu?… Ndipo akaniambia, Mwanadamu, toboa sasa katika ukuta huu; nami nilipotoboa, tazama, pana mlango. Akaniambia, Ingia uyaone machukizo mabaya wanayoyafanya hapa. Basi, nikaingia, nikaona; na tazama, kila namna ya wadudu, na wanyama wachukizao, na taswira za vinyago vyote vya nyumba ya Israeli, zimepigwa ukutani pande zote. .. Mwanadamu, umeyaona wanayotenda wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mtu ndani ya vyumba vyake vya sanamu? Maana husema, Bwana hatuoni…” (Ezekieli 8:6-12).

Hiki ndicho Mungu alimuonesha Ezekieli katika maono na bila shaka ndiyo picha ya kile kilichokuwa kinatokea kwenye maisha ya watu wake. Walifikiri kwamba Mungu hakujua kuhusiana na picha walizokuwa wakiziangalia kwa siri, katika vyumba vyenye giza vya mioyo na akili zao. Lakini Mungu anaona ndani yetu, mpaka katika vilindi vyetu. Anataka atusafishe mpaka huko! Anataka atubadilishe huko – katika vilindi vya utu wetu! Kwa nini? Kwa sababu Yesu Kristo alikufa na kumwaga damu yake kufanya mioyo yetu iwe misafi, ili kwamba Roho wa Mungu aishi humo, humo humo, katika vilindi vya maisha yetu ambako hamna mtu mwingine anaweza kupaona, lakini Mungu! Huu ndio wokovu! Huenda ukasema hii haiwezekani. Ndio inaweza isiwezekane kwa mwanadamu. Lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana! Yesu alisema maneno haya ya kushangaza, “Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.”. Mungu anataka  kuishi ndani yetu kwa Roho wake! Yesu alikufa kwa ajili ya hili! Kuongelea siku ya Pentekoste ambapo wanafunzi wangebatizwa katika Roho Mtakatifu, Yesu alisema hivi, “Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.” (Yoh.14:23,20). Hii ndiyo Injili! Hili ndilo agano jipya! Yesu ndani yetu, tumaini la Utukufu! Kama Paulo anavyosema, “Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.” (2 Wakor.13:5)

Unaona, Mungu alimwambia Ezekieli kwamba mawazo yao machafu, kuabudu kwao picha chafu katika mawazo yao kwenye akili zao kulikuwa kunamfukuza yeye mbali toka kwenye makao yake katikati yao! Kama tukiangalia picha chafu na kuziruhusu zitawale kufikiri kwetu , tutamuhuzunisha Roho Mtakatifu wa Mungu (Waefeso 4:30). Tutawezaje kuzaa matunda ya utakatifu kama picha hizi ziko mbele ya macho na mioyo yetu? Tumeona hapo awali kwamba kama tutatafuta wokovu huu lazima tulete matunda ya toba ya kweli – “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba.” Tunatakiwa kuwa halisi na wakweli mbele za Mungu. Yesu mwenyewe anatuonesha ni kwa jinsi gani tunatakiwa kuwa makini katika hili, “Mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” (Mathayo 5:28). Na kama tutaangalia picha za ngono mitandaoni? Unaona kwa jinsi gani hili swala lilivyo zito? Yesu aliweka wazi kwamba hatutakiwi kuzihurumia nafsi zetu! “Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe…” Nafikiri ni wazi kwamba Yesu hakumaanisha  tung’oe macho yetu ama kukata mikono yetu kikweli (kwa sababu kufanya hivyo hakutabadili mioyo yetu!) lakini anaonyesha kwamba inatupasa tusiwe na huruma na nafsi zetu juu ya mambo ya dhambi. Kwa maneno haya Yesu alionesha kwamba tufikiri kuhusiana siyo tu na kuathiri mawazo yetu lakini pia inaweza kupelekea matendo ya dhambi. Muendelezo wa mawazo machafu huleta matendo machafu pia! Kama waamini hatuwezi kucheza na mambo haya; hatuwezi kujiingiza kwenye mambo haya kwa sababu tu tunajisikia kushuka; hatuwezi kuzihurumia nafsi zetu na kujiingiza kwenye vitu ambavyo tunadhani vitatupa anasa ama matulizo! Tunatatikwa kuwa baridi na katili kwa dhambi! Hatuwezi kuota moto wa ‘anasa’, kwa sababu moto huu utatuangamiza!

Tunaambiwa na neno la Mungu, , “Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.” (Mathayo 5:8); “Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.” (1 Tim.1:5). Hili ni Agano Jipya ambalo Mungu ameahidi kutupa mioyo safi. Agano jipya si tu kichwa cha habari kilichopewa kwa sehemu ya pili ya Biblia! Agano jipya ni mpangilio mpya  ambao Mungu ameupanga kati ya nafsi yake na mwanadamu. Kupitia Agano hili anaweza kufanya kitu kwa mwanaume na mwanamke ambacho kitawabadilisha kabisa – angeweza kufanya hiki kupitia kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo mwanae! Amesema angetupa mioyo mipya! “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu…Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda…nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. Nami nitawaokoeni na uchafu wenu wote…” (Ezekiel 36:25-29). Maneno ya ajabu ya neema na ahadi! Na ahadi ni kwako na kwangu katika Kristo!

Sasa nataka kuongea na wale wanaompenda Bwana na wanapambana kuishinda dhambi maishani mwao. Wanataka kumpendeza Bwana lakini mara nyingi wamekuwa wakikatishwa tamaa na kushindwa kwa sababu ya mambo yanayowazidi.  Huenda wamehuzunishwa  kupita kiasi. Huenda unadhani mambo yalioandikwa hapa juu hayawezekani. Huenda unafikiri kuwa wewe u ‘mdhaifu’ kuishi kama vile Mungu anavyotaka. Huenda unadhani umeshindwa mara nyingi sana kuweza kujinasua. Usimuashie shetani aharibu ujasiri wako katika neno la Mungu! Hii ni moja kati ya mbinu kuu za shetani! Kwanza, shetani atakujaribu utende dhambi. Kama akifanikiwa, basi haraka sana atajaribu kukufanya ujisikie ni mshindwaji, kujisikia vibaya kwa ajili ya nafsi yako, kukufanya ufikiri kwamba wewe ni mtu ambaye huwezi kushinda, kwamba siku zote utakuwa wa kushindwa; atakufanya uwaze kwamba Mungu yuko kinyume nawe kwa sababu ya dhambi zako ama umetenda dhambi zisizoweza kusameheka. Atafanya mikono yako ‘ibaki ikining’inia chini’ na ‘magoti yako kuhisi udhaifu’ (Waebrania 12:12). Hii ni moja kati ya mbinu kuu za shetani. Anataka kuumaliza ujasiri wako kwa Mungu na katika neno lake. Anataka kukupeleka gizani ambako utapoteza imani kwa pendo la Mungu kwako, kuondoa imani kwamba Mungu anaweza kufanya kitu kwako! Hisia hizi za kukata tamaa kwa hali ya juu, za kushindwa kabisa, za kukataliwa, za kujichukia mwenyewe – hiyo ni kazi ya shetani! Mawazo anayoyachochea mioyoni mwetu yanatukimbiza mbali na pendo na neema ya Mungu! Hizi ni dalili za kazi yake – anataka kutupeleka kwenye kutokuamini! Na anataka kukuweka katika hali hiyo! Roho Mtakatifu hafanyi hivi maishani mwetu! Ndiyo, Roho wa Mungu anafanya kazi ndani yetu kutushawishi kuhusiana na dhambi zetu, lakini pale anapofanya hivyo anatuchukua kwenye jibu la dhambi zetu, anatuchukua mpaka kwa Yesu; Roho Mtakatifu anamtukuza Yesu katika mioyo yetu (Yoh 16:14) kama mtu atupendaye, Yule ambaye alitufia na ambaye atatusamehe dhambi zetu! Roho wa Mungu ‘hatatukuza’ matatizo yako na kukufanya usimuone Yesu na kufanya tatizo lionekane kama mlima ambao unaubeba mabegani mwako! Kupitia kwa hisia na mawazo ya kushindwa na kukataliwa, shetani atakupeleka mbali na Yesu. Roho Mtakatifu mara zote atakupeleka kwa Yesu! Unaona utofauti, kaka yangu, dada yangu? Tofauti ni kubwa.

Unaona nini kilitokea katika bustani ya Edeni? Shetani aliwaongoza Adamu na Eva kufanya kitendo cha dhambi. Walipotenda dhambi, shetani akazijaza akili zao na kutokuamini! Wakajificha mara moja! Walijawa na mawazo ya hofu, hukumu, kukataliwa kama vile Mungu angekuja na kuwamaliza kabisa! Hii ilikuwa ni kazi ya shetani mioyoni mwao na kwenye akili zao – shetani aliondoa kweli kuhusiana na reheema za Mungu mioyoni mwao, neema ya Mungu, pendo la Mungu, wema wa Mungu na uvumilivu wa Mungu. Shetani aliwafanya wafikiri kwamba Mungu alikuwa kinyume nao! Mawazo haya ndiyo mawazo ambayo shetani anataka kuyapanda kwenye akili zetu wote! Ni mawazo yanayotuchukua mbali na Mungu!

Lakini Mungu anataka tumuendee! Yohana anasema, “…nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi…” (1 Yoh. 2:1). Na hii ni kweli kwa sababu Yesu Kristo alikufa ili kuziangamiza kazi zote za shetani ili kwamba tusitumikishwe na dhambi tena! Lakini Mungu ametupa utoaji kwa ajili yetu, si udhuru kwa dhambi, lakini utoaji kwa msamaha wa dhambi! Yohana anaendelea kwa kusema, “Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu…”. Asifiwe Mungu kwa wema wake na rehema! Kama ukitenda dhambi, usikae hapo ukijisikia vibaya na nafsi yako; usitumie siku nyingi ikijisikia kushindwa ama kukataliwa! Inuka! Jikung’ute mavumbi! Muendee Bana, jinyenyekeze. Achana na dhambi na mgeukie Yesu Kristo! Njoo kwake. Usisite site. Amini neno lake na, “ inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.” (Waebrania 12:12,13). Atakusamehe na kufanya njia kwa ajili yako!

Ndugu kutoka Iringa alisema hivi, “kama unasafiri kutoka kijiji kimoja kwenda kingine na ukaanguka toka kwenye baiskeli yako, utafanya nini? Je, utakaa chini ukilia na kujiskia vibaya kwenye nafsi yako? Je, utalalamika kwa masaa kuhusiana na kushindwa kwako? Hapana! Utanyanyuka na kuendelea! Na kama utaanguka tena, utasimama na kuendelea mpaka utakapofika kijiji ulichokuwa ukikiendea! Kuna ukweli katika hili. Sitaki kumpa mtu yoyote wazo kwamba haijalishi wala haina shida hata kama tutatenda dhambi, ama dhambi siyo kitu muhimu, lakini najaribu kuonyesha mbinu amabayo shetani anaitumia kwetu sote kutufanya tusifikie lengo letu la kujua ukamilifu wa wokovu wa Kristo na ukamilifu wa pendo la Mungu.

Neno la Mungu linasema kwamba Kristo Yesu ‘aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye.’ Mungu akubariki!

© David Stamen 2014                              somabiblia.com

Kupakua somo hili bonyeza link: Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu

RUDI KWA HOMEPAGE

 

7 responses to “Mambo Machafu kwenye Internet

 1. fidel mramba

  November 12, 2016 at 7:34 am

  Nime barikiwa ,Mungu azidi kuji funua kwako kwa ajiliyetu. Shukurani, heshima na utukufu na zika zidi kumrudia Mungu.

   
 2. Jihn wakuchalo

  June 23, 2017 at 10:31 am

  Somo hili linahitaji utulivu mkubwa kulifanya lioane na uhalisia wa namna Mungu alivyo umba viumbe wake mbalimbali.Viumbe woote,kwa asilimia kubwa,Hujaamiana hadharani.Lakini pia viumbe hawa akiwamo mwanadamu kwa asili huzaliana uchi.Na kwa inchi kadhaa hadi sasa mganga mwanamume anaweza kuzalisha wanawake wa,jamaa yake.Kwa wafugaji, ni wengi wanao pandisha mifugo yao mara inapofika joto la kupandishwa,dume.Lakini mtu hafundishi ubaya asijapo uona,ubaya wenyewe.Tuseme swala la picha chafu mtandaoni ni jambo linalo tegemea fikra,na akili ya mtu. Kwani madhara yake hayapo katika picha yenyewe bali yapo katika akili ya mhusika.Kabla hata ya picha, mtu huwa na taswira nzima ya picha hizo akilini mwake mwenyewe.Hili lipo kwa mtu yeyote.Wakati dactari anakimbia filamu chafu, tayari panapo mgonjwa anae sumbuliwa katika maungo yake na anahitaji kuchunguzwa na daktari huyohuyo.Nionavyo watu wafundishwe kuzishinda hisiambaya na wakishakuwa washindi ndani yake watakuwa salama dhidi ya picha chafu na wayaonayo yoote.

   
  • Mwaisanila

   August 30, 2017 at 6:21 am

   Kaka Jihn, ni sheria ya akili kwamba kwa kutazama tunabadilishwa , kwahiyo tatizo lipo kwenye picha yenyewe na sio fikra ; fikra hutegemea kile tu ulicholisha akili hapo kabla, yaani ulishapo akili yako uchafu ndivyo fikra zako zitakavyokuwa chafu,kimoja ni chanzo na kingine ni matokeo. Hata ”mtu mkamilifu na mwelekevu, mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.” Ayubu 1:1 alijua kuwa tatizo ni ile picha yenyewe na fikra ni matokeo tu ndio maana akasema ” Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana? ” Ayubu 31:1
   Yaani Ayubu aliagana na macho yake kwamba hangetazama/hangeangalia, kwa sababu shida sio fikra za Ayubu( mwanzoni) ila shida ni kwamba picha yenyewe ina nguvu haribifu kwa utu wote wa mtu.

    
 3. Maron Mwaisanila

  August 30, 2017 at 6:03 am

  thanks to God for the study, it has been helpful.

   
 4. Reuben

  November 4, 2017 at 8:54 pm

  Umemjibu vyema wakuchalo n’a mimi nakubaliana nawewe

   
 5. Reuben

  November 4, 2017 at 8:56 pm

  Umemjibu vyema wakuchalo n’a mimi nakubaliana nawewe

   

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: