RSS

Jinsi ya kuepusha Udanganyifu na Mafundisho ya Uongo.

Imeandikwa juu ya watu wa Beroya kwamba, “Watu hawa … walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.” (Matendo 17:11). Tunapaswa kufanya vilevile ili mafundisho mapya ya siku hizi yasitufanye mateka, ili “tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Waefeso 4:14).

Na nikushirikishe kitu fulani chepesi ambacho kilinisaidia mimi kwa kiwango kikubwa kwa miaka mingi. Kama mtu yoyote akifundisha kitu kipya ama tofauti ama hukitambui toka kwenye Biblia, jiulize, ‘Hii imeandikwa wapi kwenye Biblia?’ Kwa mfano, muhubiri mmoja aliwaambia wasikilizaji, ’Kama huna ndoto, huna chochote cha kupigania.’ Haya ni mawazo yaliyo finyu kwa uhakika. Kama ni kweli, ni muhimu kwetu kuelewa hili. Kwa hiyo ni wapi nitayapata kwenye Biblia, zaidi hasa, haya yanapatikana wapi kwenye Agano Jipya? Jibu, haliko popote! Hakuna kitu kama hiki kinachofundishwa na Biblia. Ni ubunifu tu wa msemaji. Basi, ni vema nisiyajali.

Wengine wanafundisha kwamba kama ukiwa na shida katika maisha yako (ya kiroho au nyingine) inawezekana ya kuwa ‘laana’ imeingia kwenye maisha yako! Wanasema kwamba kama mojawapo wa babu yako (hata kama aliishi miaka 500 iliyopita!) alifanya dhambi bila kutubu mbele ya Mungu, ndipo babu huyo hakusamehewa, na dhambi zake zinaipeleka hukumu ya Mungu hata kufikia mpaka maisha yako, na zinampa shetani haki kukutesa na kuzuia maendeleo ya maisha ya kiroho yako! Wapi Bwana Yesu au Mitume wanafundisha mambo haya? Hawataji hata neno moja juu ya hayo! Ni ubinufu tu wa watu wanaotafsiri Agano la Kale vibaya kabisa. Basi, ni vema nisiyajali.

Wengine wanafundisha juu ya ‘siri ya mafanikio’ au ‘ujasiriamali’. Wapi Yesu au Mitume wanafundisha juu ya ‘siri ya mafanikio’. Hamna! Neno ‘mafanikio’ halipo katika mafundisho ya Yeus wala ya mitume! Urahisi na nguvu ya neno la Mungu ni, “Utafuteni KWANZA ufalme wa Mungu…” Bwana asifiwe kwa neno lake la kirahisi (ni rahisi kuelewa kwa wote!) na lenye nguvu! Mafundisho yale ni ubinifu wa watu, na maelfu maelfu ulimwenguni wanawapenda na wanawafuata wahubiri wafundishao juu ya ‘Mafanikio’ na ‘Ujasiriamali’ kwa sababu ya hamu yao kupita kiasi ya kupata pesa, yaani, kwa msingi, kwa sababu ya uchoyo wa mioyo yao! Wanayo hamu kufanikiwa katika biashara yao kuliko kufuata neno la Mungu. Vivyo hivyo Paulo anavyofundisha: “Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.” (1 Tim.6:9,10). Wengine waliofikiri wao ni matajiri walijidanganywa kabisa, sawasawa na maneno ya Yesu: “Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.” (Ufunuo 3:17). Kwa hiyo Paulo aliwaandikia washirika wa Korintho: “Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.” Kumbe, hata wengine waliookoka na huduma ya Paulo walidanganywa na wale ambao walijitukuza huduma zao!. Udanganyifu ulikuwa matokeo ya namna ifuatayo: “Maana yeye ajaye akihubiri Yesu MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho NYINGINE msiyoipokea, au Injili NYINGINE msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!” Kwa hiyo, na tusishangae kama siku hizi vilevile inatokea – watu wanaojidai wao ni nabii au mitume wanahubiri Yesu mwigine na injili nyingine! (2 Wakor.11:4,13,20)

Wengine wananukulu mistari kama Luka 6:38 na Malaki 3:10, nao wanaahidi kama nitoe pesa (kwa ajili ya huduma yao!) ndipo Mungu atanirudishia mara mia moja! Wanasema utoaji wangu ni kama mbegu nami nitavuna mengi baadaye! Hiyo ndiyo dhambi kubwa sana! Sababu kutoa pesa siyo kwamba ili nipate pesa zaidi! Hiyo ni biashara! Je, unataka kufanya biashara na Mungu! ‘Kumbe, nilipe shilling elfu moja tu, nitapata baadaye laki moja!’ Hiyo ni uchoyo, siyo sadaka! Hutoi ili upate! Yesu alisema, “Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume…’. (Mat.6:3). Ndiyo, Mungu atatubariki, lakini sababu ya kutoa pesa kwa ajili ya kazi ya Mungu au kwa maskini, siyo nitapate pesa zaidi! Sababu ya kutoa ni upendo wangu kwake Bwana na kwao watu wake! Bwana Yesu alitoa maisha yake kwa ajili yetu, si kitu kikubwa tutoe sadaka kwa hiari na kwa furaha kwa ajili ya watu Wake bila kutafuta faida kwa ajili yangu! Kwamba Mungu atanibariki ni jambo la wema wake na huruma yake – na Yesu alithibitisha ukweli huo – lakini siyo sababu kutoa pesa. Mamilioni ulimwenguni wanaanguka katika dhambi hiyo, na wanafanya hiyo kwa furaha! “Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnachukuliana na wajinga kwa furaha. Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni.” (2 Wakor.11:19,20). Kama iliyokuwa siku za Paulo vivyo hivyo ni siku hizi. Wapo watu leo wanaotumia huduma kujenga majengo makubwa ya makanisa kwa ajili yao. Wanavaa mavazi mazuri yenye thamani kubwa sana kwa sababu wanadhani kimakosa kwamba hiyo inaonyesha Baraka za Mungu na hiyo ndiyo alama ya maisha ya kiroho yenye mafanikio! Na wanajaribu kushawishi na wengine kufikiri hivyo. Na wengi sana wanawafuata bila kuelewa mafudisho ya Biblia!

Kwakweli, tunaweza kuomba kwa ajili ya ndugu zetu kama Yohana alivyofanya, “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.” Tunaona ‘kufanikiwa’ hapa lina maana kama ‘bariki’ lakini muhimu zaidi ni kwamba Yohana hachochei uchoyo katika moyo wa msomaji! Hatoi wala hafundishi mbinu ili tuwe tajiri! Sisemi lazima kubaki katika umaskini. Hapana. Lakini njia ni ‘Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu…’ na siyo kuchochea uchoyo!

Lakini Mungu apewe sifa kwa ajili ya neno lake! Kwa msingi sihitaji kwenda shule ya Biblia au Chuo Kikuu kuelewa neno la Mungu kwa maisha yangu. Kwa kweli inawezekana yapo mambo yasiyo rahisi kuelewa katika Biblia, LAKINI mambo yale ambayo ni lazima nielewe kwa maisha yangu ya kila siku kama mkristo naweza kusoma na kuelewa kama moyo wangu ni sawa mbele ya Bwana!

“Wakati ule Yesu akajibu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele zako.” (Mat.11:25,26)

“…huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote…” (Yoh.16:13)

“Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote…” (1 Yoh.2:27)

Mistari hii haimaanisha kwamba tunaweza kujitenga na watu au tusiwasikilize wengine wafundishao neno la Mungu, lakini mistari hii ina maana yake kwa ajili ya faida yetu na kwa ajili ya USALAMA wetu wakati wengine wanapohubiri udanganyifu! Mungu apewe sifa sana kwa wema wake na huruma yake kwetu!

© David Stamen 2014                somabiblia.com

Kupakua somo hili bonyeza link: Jinsi ya Kuepusha Udanganyifu na Mafundisho ya Uongo

RUDI KWA HOMEPAGE

 

6 responses to “Jinsi ya kuepusha Udanganyifu na Mafundisho ya Uongo.

  1. Pingback: somabiblia
  2. JAPHET C KAMKONO

    May 22, 2015 at 3:20 pm

    Nimeyapenda sana mafundisho haya,napenda na watu wengine ambao husoma kurasa zangu za blogu yangu wayasome.Mafundisho yenu.Hivyo ninaomba mnipatie RUHUSA/KIBARI ili makala hizi zichapwe kwenye blogu yangu.Lengo kuu ni kufikisha ujumbe kwa watu wengine ambao hawajafika katika ukurasa wenu.MUNGU AWABARIKI KWA KUFUNDISHA NENO LAKE.

     
  3. Anonymous

    November 4, 2015 at 2:45 pm

    nimeelewa

     
  4. Titus Patrick

    December 15, 2015 at 8:56 pm

    ubarikiwe sana kwa mafundisho yenye uzima, kwa kuzidi kuijua kweli ya Mungu itazidi kutuweka huru dhidi ya mafundisho potofu. ubarikiwe sana

     
  5. Jihn wakuchalo

    May 28, 2017 at 5:05 am

    Somo zuri.Ubarikiwe.

     
  6. Anonymous

    February 12, 2020 at 10:46 am

    Nimeelewa sana mungu awabariki sana

     

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: