RSS

Je, unapenda kuwa mtu wa Mungu?

Je, unataka kuwa mwanamume au mwanamke wa Mungu? Unataka kubarikiwa? Tusikilize neno la Mungu:

“Heri mtu yule… ambaye sheria ya Bwana NDIYO IMPENDEZAVYO, na sheria yake huitafakari MCHANA NA USIKU.” (Zaburi 1:1,2). Je, tunaishi kwa namna kama hiyo? Je, Yesu ni Mwanzo na Mwisho kwetu na tunampenda Yeye na neno lake kuliko yote nyingine? Je, tunakubaliana na Yesu kwamba, “…kinatakiwa kitu kimoja tu” na tumelichagua fungo lililo jema ambalo hataondelewa, kama Mariamu alivyofanya? (Luka 10:42). Je, Neno la Mungu ni thamani kwetu kuliko yote nyingine? Tena tusikilize mtu wa Mungu alilosema katika Zaburi, “…ninayapenda maagizo yako (au tunaweza kusema, ‘neno lako’) KULIKO DHAHABU, naam, dhahabu iliyo safi.” (Zaburi 119:127). Je, haya ni kweli kwetu? Siku hizi wengi wanafundisha juu ya ‘ujasiriamali’ – ni jambo la kuhuzunisha kwamba wengi wanafuata mtazamo huo – wanafuata MAFANIKIO. Wanataka kazi yao ifanikiwe, biashara yao ifanikiwe na kufanikiwa katika kila sehemu ya maisha yao, ingawa Biblia haifundishi ‘yafuate mafanikio’! Biblia inafundisha kwa urahisi sana, “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hayo yote mtazidishiwa.” (Matt.6:33), na kwa msingi, “tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.” Neno la Mungu halichochei moyoni mwa watu wa Mungu uchoyo kwa pesa na vitu; halichochei tamaa kwa vitu, pesa au ‘mafanikio’. Watu wengi siku hizi wanatafuta ‘baraka za nje’ kama watu wa Israeli walivyofanya jangwani na wanapoteza kabisa baraka za kiroho, vile vile watu wa Israeli walivyopoteza! Juu ya ‘ujasiriamali’, Paulo anafundisha, “wale watu wanaotamani kuwa na mali kwa huanguka kwenye majaribu na wamenaswa na tamaa nyingi za kipumbavu, zenye kudhuru, zinazowazamisha watu katika uharibifu na maangamizi.” Kinyume cha hicho anafundisha, “Walakini utauwa pamoja na kuridhika NI FAIDA KUBWA.” (1 Tim.6:9,6). Je, inaonekana vipi kwetu? Je, tunampenda neno la Mungu kuliko dhahabu? Tunashauriwa na neno la Mungu ifuatayo, “Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,…na kama UTAITAFUTA KAMA FEDHA NA KUITAFUTA SANA KAMA HAZINA ILIYOFICHWA, ndipo utakapoelewa kumcha BWANA na kupata maarifa ya Mungu.” (Mithali 2:1,4,5).

Kama nilivyosema, wengi wanatafuta ‘baraka’, baraka’, ‘baraka’ – lakini wanathamani baraka za ‘nje’ (pesa, biashara. ‘kuboresha’ maisha yao, mafanakio) kuliko neno la Mungu, kama vile watu wa Israeli walivyotaka ‘baraka za nje’ kuliko kumfuata Mungu, kwa hiyo Mungu aliwaambia – vile vile anavyotuambia – “Mtu hataishi kwa mkate ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.” (Mtt.4:4). Basi kwa hiyo mtu wa Mungu katika Agano la Kale alikiri, “Nitajifurahisha SANA kwa maagizo yako ambayo NIMEYAPENDA.”. Hata katika shida ilikuwa vile vile; anasema, “Wakuu wakaninena, lakini mtumishi wako ATAZITAFAKARI AMRI ZAKO (au neno lako).” Na tena, “Hiyo ndiyo faraja yangu katika taabu yangu, ya kwamba ahadi yako (neno lako) imenihuisha…Bwana ndiye aliye fungu langu.”. Kwa hiyo anasema, “Neno lako (sheria yako) nalipenda MNO AJABU, ndiyo kutafakari kwangu MCHANA KUTWA!” (Zaburi 119:47, 23, 50, 57, 96). Ushuhuda wetu ni nini sasa? Tukiishi ya namna hiyo – kumpenda Yesu na Neno Lake kuliko yote nyingine – tutakuwa na amani nyingi hata kama hatutafanikiwa katika kila sehemu ya maisha yetu. Kinyume cha hicho, hatakuwa na kitu kutukwaza kwa sababu tunaishi kwa neno la Mungu, kama iliyoandikwa, “Wana amani nyingi waipendayo sheria zako wala hawana la kuwakwaza.” (Zab.119:165).

Sawasawa na Neno la Mungu, siyo wengi wanaomtumikia Bwana Yesu Kristo kweli kweli. Kama ilivyokuwa siku za Paulo, ni vivyo hivyo siku hizi. Paulo anasema juu ya Timotheo, “sina mtu mwingine mwenye nia moja name, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli, MAANA WOTE WANATAFUTA VYAO WENYEWE, sivyo vya Kristo Yesu.” (Wafilipi 2:20,21). Je, tunatafuta nini – ‘baraka’, ‘mafanikio’, ‘ujasiriamali’, cheo, faida yetu, sifa, kutawala kama mabwana, ndoto yangu kuwa mwimbaji au kupiga gitaa katika band moja au ndoto nyingine – au kumpendeza Bwana Yesu katika kila kitu na kuongozwa na neno lake.

Kama tukipenda kuwa mwanamume au mwanamke wa Mungu, lazima tuishi kwa neno la Mungu kweli kweli; tusifuate kundi la watu bali tulifuate shauri la Paulo, “UYATAFAKARI HAYO; ukae katika hayo ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote, Jitunze nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo, maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.” (1 Tim.4:15,16.) Maneno ya ajabu!

“Ninalipenda neno lako KULIKO DHAHABU, naam, dhahabu iliyo safi.”

© David Stamen 2014                           somabiblia.com

KUPAKUA SOMO HILI BONYEZA LINK: Je, unapenda kuwa mtu wa Mungu

 RUDI KWA HOMEPAGE

 

4 responses to “Je, unapenda kuwa mtu wa Mungu?

  1. Pingback: somabiblia
  2. Davith D

    November 16, 2014 at 8:19 pm

    Tukumbuke Kusari Na Kutubu Dhambi Zetu.

     
  3. Yaredi Kyando

    September 4, 2015 at 8:14 am

    Asante mtumishi wa MUNGU ni kweli kabisa hatuwezi lolote pasipo neno la MUNGU

     
  4. Yona

    March 11, 2019 at 4:55 am

    Uko sawa mtumishi wa Mungu

     

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: