RSS

Wewe ni Mfungwa wa nini?

Mtume Paulo alikwepo gerezani wakati alipoandika barua kwao watakatifu waliopo Efeso. Katika sura 4 mstari 1 anajiita ‘mfungwa katika Kristo Yesu.” Hakusema yeye ni mfungwa wa serikali, au mfungwa wa Kaisari, au mfungwa wa mazingira yake, au mfungwa wa shetani! Alikiri ukweli uliomo moyoni mwake, yaani, yeye ndiye mfungwa wa Kristo Yesu! Huo ndio mtazamo wa kiroho! Hakujali vifungo vyake, hakujali gereza, hakujali mazingira yake; ni kama alitangaza kwa watu wote, “Mimi ni mfungwa wa Bwana! Mazingira haidhuru kwangu!”

Sasa, ndugu yangu, kijiji sio gereza lako! Wewe sio mfungwa wa kijiji chako, au wa ndoa yako, au wa kazi yako, au wa mazingira yako, au wa wivu ya ndugu zako! Bwana asifiwe! Anatupa neema zaidi! Huwezi kusema, ‘Mazingira haya, au upungufu wa jambo hili, au mtu yule, au ndugu huyo vinanizuia kukua kiroho, zinanizuia nisiendelee mbele katika Bwana.’ Hapana! Siyo kweli! Kama wakristo, sisi tu wafungwa wa Bwana tu – tumtumikie Yesu katika kila mazingira – kuishi kijijini au kutoka, tufanye kama wafungwa wa Bwana kama Yeye anavyopenda – kadiri ya mapenzi Yake, siyo ya kwangu.

‘Yupo mtu fulani mgumu kazini kwangu anayezuia maisha ya kiroho!’ Hiyo siyo kweli. Kazi yako siyo gereza lako, na kama mfungwa wa Bwana unapswa kumwonyesha yule neema na msamaha na usiwe mfungwa wa uchungu au ugumu au hasira moyoni mwako, kwa sababu ‘Mungu huwapinga wajukuzao bali huwapa neema wanyenyekevu.’ Kama Paulo anavyosema sehemu ile ile katika Waefeso sura ya nne, “Basi, mimi niliye MFUNGWA WA BWANA, nawasihi mwenende kama inavyostahili WITO WENU mlioitiwa. iweni WANYENYEKEVU kabisa na WAPOLE, mkiwa WAVUMILIVU, mkichukuliana KWA UPENDO.” Hiyo ilikuwa nia au ‘mtazamo’ wa Paulo! Wengine (hasa mjini) wanatafuta ‘mtazamo’ mzuri ili waboreshe maisha yao au kufikia lengo lao wapate ‘mafanikio’! Lakini nia ya Paulo ilikuwa “Mimi niliye mfungwa wa Bwana – sina mapenzi yangu ya binafsi, sina malengo yangu ya binafsi; namtumikia Bwana, natafuta mapenzi Yake tu, na goali (malengo) yangu ndiyo, ‘nimjue Yeye na uweza wakufufuka kwake, na ushirika wa mateso Yake.’ Mambo nyingine yote ni ‘mavi’ kwangu!” Nia ya Paulo ilikuwa kuhesabu mambo yote kama ‘mavi’ ili apate Kristo! Sasa, lengo (goali) la Paulo ni lengo letu? Na tunahesabu yote kama ‘mavi’ ili tupate Kristo? Hatupo kanisani sasa! Huwezi kusema ‘Amen’ kwa mdomo mbele ya watu. Upo peke yako, jibu kwa kweli moyoni mwako.

Au labda yote siyo ‘mavi’ kwako, na mafundisho ya ulimwengu wa biashara na wahubiri wahamasishaji (‘motivational speakers’) watokao Magharibi/Ulaya wafundishao juu ya ‘mafanikio’ yanayokuvuta. Mafundisho haya ya kibinadamu na filosofia ya ulimwengu huo yameingiza makanisani na yanaharibu maisha ya kiroho ya weeeengi.

Usinielewe vibaya. Sisemi hatuwezi kufanya kazi kwa bidii au kuweka mipango juu ya kazi yetu. Haya ni vizuri, lakini na tumtumikie Bwana Yesu kiasi cha kutokuruhusu cho chote kutuchukua MATEKA, hata kama ni jambo ‘nzuri’! Umjue Bwana Yesu ni lengo lako kiasi cha kutokujali jambo lo lote lile kutawala katika maisha yako au katika mawazo yako – siyo pesa, wala cheo, wala sifa ya watu, wala biashara, wala malalamiko juu ya mazingira yako! Kama Paulo alivyosema, “Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vitu vyote vyenye faida. Vitu vyote ni halali kwangu,” lakini SITATAWALIWA NA KITU CHO CHOTE.” 1 Wakor.6:12.

Ndoa yako siyo gereza lako! Kama unayo shida hiyo, ni nafasi kukua katika neema na upendo wa Mungu. Sisemi hivyo cha kiurahisi! Maisha ni maisha (life is real) na tunapaswa kila siku kuchagua tuwe mfungwa wa hasira na uchungu au ugumu wa moyo, au kuchagua tuwe mfungwa wa Bwana, yaani, SINA UHURU, sina haki kukasirika mpaka usiku, sina haki kuruhusu uchungu, ugumu, chuki, wivu au kutokusamehe ziingize moyo wangu! Mimi ndimi mfungwa wa Bwana! Nimewekwa huru kumpenda jirani yangu! “Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.” (Wafil.1:21). Hiyo ndiyo Injili yenye nguvu ya Mungu kubadilisha maisha yetu tuwekwa uhuru kweli kweli!

“Aaaaah, kama mazingira yangu yangekuwa tofauti!” Amke ndugu! Usijidanganye! Usilalamike, badala yake, “itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.”

Je, unataka kuoa au kuolewa? Kumbuka, wewe ni ‘mfungwa wa Bwana’ ili usifanye mapenzi yako bali mapenzi ya Mungu! Ndugu yangu, dada yangu, ‘umngoje Bwana’. Usitafute njia ya mkato (‘short cut’) kwa kuwa unafikiri umesubiri kupita kiasi! Usimjalie Shetani kukushawishi kwamba huwezi kupinga au kukataa anasa ya dhambi! Usimjalie kuharibu maisha yako duniani na kwa milele! Umngoje Bwana kwa moyo wako wote. Ujimtoe maisha yako kabisa! Kwa wakati mzuri atakubariki! Ni jambo la kuhuzunishwa sana kwamba wengi wanaanguka mahali hapa. Mimi nilioa kwa umri wa miaka thelathini na tano, na Mungu alinitunza kwa neema na nguvu Yake mpaka wakati ule ule, na mpaka sasa hivi pia! Ndiyo, pengine ni lazima ufe, kama tulivyoona, “Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.” Maisha siyo mchezo! Kama hatuchukii nafsi yetu wenyewe, hatuwezi kuwa wanafunzi wa Yesu! Umngoje Bwana!

Kama wewe na mimi ni wafungwa wa Bwana, tupo uhuru! Tupo uhuru kumtumikia Yeye kwa neema, unyenyekevu na upendo katika mazingira yote. Kwa hiyo Paulo anasema, “Furahini katika Bwana sikuzote! Paulo alisema, “Naweza kuyafanya mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu.” Je, aliweza kufanya nini kwa nguvu ya Bwana? Anatueleza kwa wazi! “Kwa maana nimejifunza kuridhika katika hali yo yote. Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa na vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika  kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wa kuwa na vingi na wakati wa kupungukiwa. Naweza kuyafanya mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu” (Wafil.4:11,12). Siku hizi wengi wanakimbilia ‘manafikio’! Paulo alimfuata Yesu na kwa hiyo aliridhika katika hali yo yote! Na mimi, na wewe? Faida kubwa ni nini? Tena Paulo anatuambia, “Lakini utauwa na kuridhika ni faida kubwa.” Mungu apewe sifa kwa mafundisho wazi kabisa! Usiwe mfungwa wa ‘mafanikio’!

Tunaimba, “Yesu unatosha.” Ni kweli? Unataka nini? Unatafuta nini? Maisha yanatuongoza tuchague kila siku. Ndugu, tuchague ile iliyo bora! Na tuwe mfungwa wa Bwana!

© David Stamen 2015            somabiblia.com

Kupakua somo hili bonyeza link:  Wewe ni Mfungwa wa nini

Unaweza kusikiliza jumbe wa audio juu ya hayo kwa kubonyeza HAPA

RUDI KWA HOMEPAGE

 

2 responses to “Wewe ni Mfungwa wa nini?

  1. Pingback: somabiblia
  2. Anonymous

    April 21, 2020 at 6:28 am

    Nimebarikiwa

     

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: