RSS

VITA VYA KIROHO : ROHO ZITAWALAZO MAENEO

(Kupakua makala hiyo bonyeza:  Vita vya Kiroho )

Katika makala hii tutaangalia mafundisho yanayohusiana na kile wanachokiita “Roho za Kimaeneo”. Kulingana na mafundisho hayo, wanadai kuna roho chafu maalum ambazo zinatawala jamii, vijiji, miji, jiji au hata nchi nzima. Hiyo ina maana kwamba, roho hizo zinatawala katika eneo zima kulingana na jiografia ya eneo lenyewe; na hivyo huitwa “Roho za Maeneo”. Inaendelea kufundishwa zaidi kwamba eti hizi roho za maeneo zanao uwezo na mamlaka ya kuwabana watu katika giza, vifungo na dhambi kulingana na jiografia ya eneo lao. Kimsingi, zaidi ya hilo, hawa wanaohamasisha mafundisho hayo, wanatuambia kwamba hizi roho za maeneo zinao uwezo wa kushikilia jamii ndogo au miji kiasi kwamba Injili peke yake haiwezi kufaa, kupata kuingia wala kupendwa au kuenea katika eneo hilo hadi hapo hizi roho za kimaeneo zitakapotambulikana na kisha zikafungwa, zikazidiwa nguvu pamoja na kukemewa kwa njia ya maombi. Wanafundisha kwamba watu hawawezi kumjia Bwana, wakaokolewa na kukombolewa kutoka katika dhambi, giza, pamoja na vifungo mbalimbali, kwa idadi kubwa mpaka kwanza hapo tutakapotambua na kisha kuzifunga na kukemea nguvu za roho hizo za kimaeneo. Hivyo ndivyo wanavyosema na kuwafundisha watu.

Hiki ndicho kidokezo cha mafundisho yao kwa lugha rahisi kadiri iwezekanavyo, na nina hakika kwamba utakubali kuwa ikiwa mafundisho haya ni ya kweli, basi ni ya umuhimu mkubwa. Kuenea kwa Injili pamoja na kuokolewa kwa watu kunategemea ufahamu na matumizi ya mafundisho haya, ikiwa mafundisho hayo ni ya kweli! Jambo hili haliwezi kuwa swala la jinsi mtu aonavyo au tafsiri ya kibinafsi, kwa sababu litaathiri ufahamu wetu kuhusiana na jinsi Injili ilivyo, pamoja na lile alilolifanya Yesu pale Kalvari.

Kama ilivyo katika zile makala nyingine zilizopita, napenda kwanza niangalie yale ambayo Maandiko yanavyosema na kufundisha. Kwa hivyo, kwa muda huu, hatutaangalia Maandiko ambayo watu wanadhani wamepata kuyaona mambo hayo yakifundishwa. Jambo hili ni la msingi na lenye uzito mkubwa kiasi kwamba hatuwezi kuyaachia kwenye ubunifu au hisia za kibinadamu tu. Tunachotafuta ni maandiko ambayo mambo haya yanafundishwa dhahiri na kutajwa bayana.

Mambo haya yanafundishwa wapi ndani ya Agano Jipya?

Kwa jibu la urahisi na la ujumla kuhusiana na habari hiyo hapo juu ni – “Hakuna popote!” Hatuyapati mahala popote katika Agano jipya, mafundisho haya yahusuyo kutambua na kuzifunga roho za kieneo!

Yesu hakutumia au kufundisha mbinu hii.

Hakuna mahali popote tunaposoma kuwa Yesu aliibainisha roho iliyokuwa ikitawala eneo, kijiji au mji, na kisha akaifunga na kuikemea kabla hajaanza kuhubiri na kufanya miujiza mahali hapo.

Hakuna mahali popote ambapo Yesu aliwafundisha mitume wake au mtu mwingine yeyote kwamba Neno la Mungu linaweza kuwa na nguvu na mafanikio katika eneo fulani ikiwa kwanza utaibainisha roho ya lile eneo na kuifunga na kuzishinda nguvu zake kwa njia ya maombi. Kamwe hatusomi popote Yesu akiitumia au kuifundisha mbinu hii.

 Mitume hawakutumia au kufundisha mbinu hii.

Hakuna mahali popote pale katika Injili au kwenye Matendo ya Mitume ambapo tunasoma habari za mitume au mtu mwingine yoyote yule akitumia mbinu za jinsi hiyo katika kuineza Injili. Mtume Paulo alitembelea miji mingi sana ambamo kulikuwa na zinaa ya kutisha, mambo ya kimwili, uchawi pamoja na dhambi. Hakuna popote pale ambapo tunasoma juu yake akizitambua kwanza roho hizo katika miji hiyo ili aone ni aina gani ya roho za kimaeneo zinazotawala katika miji, wala hatusomi mahala popote pale na kuona akiomba juu ya roho za aina hiyo ili kwamba kazi ya Injili ipate kustawi.

Hakuna mahali popote pale ndani ya maandishi yao kwa makanisa au kwa watu binafsi, ambapo mitume hawa wamepata kutaja tu mbinu za jinsi hiyo, licha ya kuzifundisha. Yapo mahusia mbalimbali kwa ajili ya kuomba katika Agano Jipya. Lakini hakuna mahali popote pale ambapo mitume wanaelekeza kuwa roho za kimaeneo zina uwezo juu ya watu katika baadhi ya maeneo na kwamba watu hawana budi kuomba dhidi ya roho hizo na kuzivunja nguvu zake, ili kwamba Injili ipate kustawi na ili wanawake na wanaume wapate kuokolewa.

Hayapo mafundisho ya jinsi hiyo ndani ya Agano Jipya. Kwa msingi huu pekee, tunaweza, kwa usalama kabisa, kuyakataa mafundisho ya jinsi hii.

Lakini sasa, mtindo wa jinsi hii haufudishwi kwenye Agano la Kale wala hatuna hata mfano mmoja katika Agano la Kale, unaoelezea juu ya mtu yeyote anayezitambua roho za kimaeneo na kufunga nguvu zake kabla kazi ya Bwana haijakamilishwa ipasavyo. Kwa kweli, waandishi hao wa kisasa wanarejea katika maandishi fulani fulani ya Agano la Kale, na tutakwenda kuangalia maandishi hayo baadaye, lakini hata hivyo, hakuna hata andiko moja linalounga mkono mtindo huo na mbinu zao zinazoenezwa na waandishi hao.

Jukumu la Uongo

Wanawezaje walimu hawa wa siku hizi kusema, “Lazima uzitumie mbinu hizi ili kuhakikisha mafanikio ya uInjilisti katika ulimwengu”, wakati ambapo maandiko hayatushauri kufanya hivyo? Wanaweka jukumu juu ya watu we Mungu wakati ambapo maandiko hayaweki jukumu la jinsi hiyo. Kwa maneno mengine, wao huongezea maneno yao juu ya Neno la Mungu – na wakizitumia mamlaka zao juu ya watu wa Mungu, mamlaka ambazo hazitokani na Mungu. Hili ni jambo la hatari sana. Ni jambo moja kusema kuwa, kwa sababu maandiko hayawazuii kuzitumia mbinu hizo, kwa hivyo wao wanajisikia uhuru kuzitumia. (Hata hivyo, hoja hii si ya msingi, kwa sababu mafundisho yao yanagusa kweli za msingi za Injili na ufanisi katika kuenezwa kwake, hivyo wanapaswa kuonyesha kwa uhakika mambo hayo yanafundishwa wapi katika maandiko, kabla hawajafundisha na kuzitumia kanuni hizo). Lakini kwa kweli wanafundisha kanuni zao za lazima kwa ajili ya kueneza Injili. Huo ni udanganyifu na unaweza kuwapelekea watu wa Mungu, kutumbukia katika kuchanganyikiwa, vifungo pamoja na hatari iwapo watapokea na kuyafuata mafundisho ya jinsi hii.

Ikiwa mbinu hizi za kuzitambua na kuzifunga roho za kimaeneo ni za lazima kwa ajili ya kuleta mafanikio ya uenezaji wa Injili, kwa nini basi Yesu pamoja na mitume wake hawakufundisha wala kutufunulia mambo hayo? Tunaelezwa na hawa walimu wa kisasa kwamba maombezi dhidi ya mamlaka na uweza juu ya maeneo ya kijiografia, yanahitajika sana kabla Injili haijapenya katika maeneo hayo. Je, mitume walikuwa ni wajinga juu ya mbinu hizo? Au labda walishindwa kutufunulia kile kilicho cha lazima kwa ajili ya uenezi wa Injili, na kwa ajili ya wokovu wa nafsi za watu? Je kanisa litakuwa limeondolewa ukweli huu wa lazima kwa muda wa miaka 2000? Hapana! Kanisa halijanyimwa ukweli huu wa lazima, na bado Injili imeendelea kuenea muda wote huo kwa karne zote hizo, kama Yesu alivyosema Injili haina budi kuenea, hata bila kanisa kufundisha au kuzitumia mbinu hizo ambazo hawa walimu wa kisasa wamezibuni. Kutokea muda wa Matendo ya Mitume hadi kufikia siku hii ya leo, kumekuwepo na uamsho, maelfu ya watu wamerejea kwa Bwana kwa idadi kubwa, nao wameokolewa kutokana na dhambi, giza na vifungo vya shetani pasipo hata kujulikana kwa mbinu hizo, kufundishwa wala kuzitumia!

Kutamani “matokeo” kupita kiasi.

Lakini moja ya kusudio lao kuu hawa wahubiri na walimu wa kisasa ni kuona “matokeo”. Mmoja wa viongozi wa kanisa ambaye anaamini katika kutumia kanuni hizo amesikika akisema kuwa iwapo kanisa lake halitaongezeka kutoka washirika 1000 hadi kufikia washiriki 2000 ndani ya miaka miwili, basi hapo itakuwa ni kutokana na kushindwa kwao katika kujaribu kwa makini kufanya hivyo. Kwa maneno mengine, iwapo tutazitumia mbinu halisi basi tutegemee kanisani washirika kuongezeka mara mbili zaidi ndani ya miaka miwili! Watu hawa wanalifanya kanisa kuwa kana kwamba ni aina fulani ya biashara ambapo tunapaswa kuzitafuta kanuni bora zaidi ili kutoa matokeo na kufikia malengo. Hata makanisa mengi kwa sasa yameanza kutoa “maelezo ya umisheni” pamoja na malengo yao kwa ajili ya mafanikio yao. Mtindo wa aina hii kwa kazi ya Mungu, umeazimwa moja kwa moja kutoka kwa ulimwengu wa kibiashara. Hii yote inamdhalilisha Yesu Kristo ambaye ndiye kichwa cha kanisa lake ambaye ndiye aliyetuonyesha kwa neno lake jinsi itupasavyo kujishughulisha wenyewe. Mmoja wao amesema kwa uwazi kabisa kwamba wanavutiwa zaidi na yale “yanayofanya kazi” ( yaani, yanayoleta mafanikio au matokeo ) kuliko “yale yaliyo ya kweli”. Kwa hiyo basi, tayari wameanza kujenga msingi wa udanganyifu wao. Katika kujiondoa kwao kutoka katika miongozo iliyo sahihi ya Neno la Mungu, wao wamekuwa wakijiweka wazi kwa udanganyifu wa shetani; kadiri wanavyoendelea na kuzitumia mbinu na kanuni zinazoweza kuwaletea matokeo ya haraka na yenye kuvutia.

Yesu anaomba kwa Baba akisema “Neno lako ni kweli”, Yohana17:17. Sasa kama watu wa Mungu, sote tunatamani na kuomba kwamba Injili iweze kufikia na kuokoa nafsi za watu wengi watuzungukao na ulimwenguni kote. Lakini watu wa Mungu, maombi yetu, kazi zetu, pamoja na mafundisho yetu lazima yawe kulingana na neno la Mungu, ambako ndiyo kweli. Hamu yetu ya “kuona matokeo” isituongoze kuelekea kwenye kuikataa au kujitenga na Neno la Mungu kama lilivyofunuliwa katika maandiko; au kuanzisha mbinu zetu wenyewe au mtindo wa fikra kwa ajili tu ya kujipatia kile kinachoonekana kuwa ni “matokeo” ya haraka. Mengi ya mafundisho hayo ya kisasa yanasukumwa na mawazo ya “mafanikio” yakikusudia kutafuta kitu fulani “kinachofanya kazi” na hiyo ni “Mafanikio”. Hawa walimu wa kisasa wanaendelea kubuni mawazo mapya pamoja na mitindo ya kufundisha. Hakuna hata mmoja anayeweza kujihoji mwenyewe kuwa inakuwaje kila baada ya miaka michache kunahitajika “mitindo” mipya, katika mtazamo wa Kitheolojia – hii ni upepo mpya wa imani! Wala hakuna hata mmoja anayeweza kuuliza, kulitokea nini na ule upepo wa imani uliopita? Au kutambua kwamba kanisa halihitaji mtindo mpya katika mafundisho yake ya Imani isipokuwa ni marejeo kwa yale ambayo tayari yamefunuliwa vizuri katika maandiko. Ikiwa tutakuwa waaminifu, tutapaswa kuungama kwamba, mafundisho hayo mengi ambayo yanaendeshwa na wazo la mafanikio ni matokeo yanayotujia moja kwa moja kutoka kwenye mila za kibiashara za Marekani (U.S.A); mahala ambako kila kitu kinategemea malengo, matokeo pamoja na mafanikio. Na Wakristo zaidi sana huko Marekani wameazima akili hizo au wamechukua mtazamo na silka kutoka kwa ulimwengu na wameuingiza kanisani, umewapelekea kwenye ubunifu wa mafundisho na matendo ya kutatanisha.( Bila shaka, mimi sisemi kwamba, wazo la roho za kimaeneo linakuja kutoka kwenye desturi za kibiashara, lakini huu msukumo kwa ajili ya mafanikio – ambao umewapelekea Wakristo hawa kutumbukia katika ubunifu na udanganyifu).

Mwandishi na mwalimu ambaye ni mmoja wa waenezaji wakuu wa mafundisho haya anaelezea juu ya jambo ambalo nimeligusia hapo juu, kuhusiana na kukosekana kwa maandiko yanayounga mkono mafundisho haya. Katika utangulizi wa kitabu chake alichokiandika yeye mwenyewe kiitwacho “Territorial Spirits” (“Roho za Kimaeneo”; Sovereign World Ltd. Ó1991 C.P.Wagner), amesema kuwa, amewahi kutazama kwenye vitabu 100 huko kwenye seminari ya theolojia ambavyo vimezungumzia kuhusiana na somo la malaika na mapepo, ili aweze kugundua mafundisho yahusuyo roho za kimaeneo. Anaendelea kueleza kuwa, siku za leo ipo haja kubwa sana ya kufanya utafiti kwa ajili ya somo hilo. Lakini kwa nini tufanye utafiti? Je utafiti wa kwenye Biblia hautoshi? Je hatuna Biblia? Neno la Mungu halitoshi kutuelekeza kuhusiana na jambo kama hili la msingi? Kwa dhahiri kabisa sivyo hivyo, kwa kuwa yeye hawaaliki watu wafanye utafiti katika Biblia. Ijapokuwa kwa hakika anajaribu kutafuta ushahidi kwa ajili ya mafundisho hayo kwenye maandiko, kama tutakavyoweza kuona hapo baadaye, yeye anaenda sehemu nyingine ili kuona iwapo anaweza kupata uthibitisho kwa ajili ya ubunifu huu wa kigeni. Lakini anatuambia kwamba ni vitabu vitano tu kati ya 100 vilivyotaja kuhusiana na somo hilo la roho za kimaeneo, na kati ya hivyo vitabu vitano, ni vitatu tu ambavyo angalau vinasema chochote kinachoweza kusaidia. Lakini hakuna chochote kati ya vitabu hivyo ambacho kilistahili kujumuishwa katika kitabu chake. Hii haishangazi kwa vile mafundisho hayo hayamo pia katika Biblia – na mpaka sasa hakuna hata mmoja ambaye amebuni au kuyatumia kwa jinsi hiyo, kwa kadri nifahamuvyo. Kwa hiyo, katika kitabu chake hicho anajumuisha michango kutoka hasa kwa waandishi wa siku za leo ambao wanaoeneza mawazo ya jinsi hiyo. Wagner alikuwa anafanya utafiti juu ya kanuni za ukuaji wa kanisa na maombi, alipowafikia viongozi wa kanisa fulani ambao walikuwa wakifanya aina hii ya maombezi dhidi ya roho za kimaeneo. Hapo, ilimpelekea kuingia ndani zaidi ya mafunzo yake juu ya somo hili. Kama tulivyokwisha kuona katika makala nyingine iliyopita, watu hao wanapofanya utafiti wao hawaanzi kwa kusoma Biblia, isipokuwa wao huanza kwa kutegemea uzoefu wao wenyewe na “mafunuo ya kiroho” wanayoyapokea. Ndipo hutafuta maandiko ambayo huyalazimisha au kuyafanya yaunge mkono “mafunuo” waliyopokea. Nasi tutatazama maandiko hayo hapo baadaye. Lakini napaswa kusema kuwa, hata hao viongozi wa makanisa – ambao waliiamini imani hiyo ya kigeni, hawakubaliani wao kwa wao kuhusiana na mafundisho haya, na namna ambayo yanapaswa kutumiwa. Kwa vile hayaungwi mkono na maandiko ya Neno la Mungu, basi haishangazi kuona kwamba mmoja wa waenezaji wa mawazo haya ameamua kusema kwamba kwa kuwa Mungu ni mwenye enzi, basi anafunua mbinu mpya na bora kwa ajili ya uInjilisti wa ulimwengu mzima. Wanachomaanisha ni kwamba Mungu anaufunua kwao ufunuo huu usiopatikana katika Biblia, na hivyo wanajihesabia wenyewe mamlaka ya kitume! Yote hii inaonyesha jinsi wanavyoiacha imani, kwa vile wanayainua mafununuo yao na uzoefu wao juu ya neno la Mungu.

Hebu sasa tuyatazame kwa karibu yale yanayofundishwa na waandishi hawa wa kisasa kuhusu vita vya kiroho.

Mafundisho yao juu ya Vita vya Kiroho.

Wanaigawa vita ya kiroho katika ngazi tatu. Kwanza, kuna kile wakiitacho mapambano ya “ngazi ya chini”, ambayo wanamaanisha kutumia mamlaka ambayo Mungu amelipatia kanisa lake kuwatoa mapepo toka kwa mtu mmoja mmoja. Hii imetolewa mfano wake vizuri katika Injili na Matendo ya Mitume na hivyo siyo jambo lenye kuleta hoja kwetu. Aina ya pili inaitwa mapambano ya “ngazi ya kishirikina” ambavyo wanamaanisha kuwa ni kukabiliana na kuzifunga roho za uchawi, dini ya kishetani, ibada za sanamu, na kadhalika, mambo ambayo kwa kawaida yanaleta athari zake ovu kupitia kwa mtu fulani binafsi. Ngazi ya “juu” ya mapambano ya kiroho inaitwa mapambano ya “kimkakati” au ya “kwenye anga za juu” ambapo maombezi yanahitajika ili kuzitambua na kuzifunga roho mbaya za ngazi za juu, au mamlaka na nguvu, ambazo zinatawala katika maeneo makubwa ya kijografia.

Hizi ngazi mbili za mwisho ni mambo ya kukisia na ubunifu wa hawa waandishi wa kisasa, kama tutakavyoweza kuona. Ile ngazi ya pili haina umaarufu mkubwa na inaingiliana kwa kiasi fulani na ile ya tatu. Kwa hiyo nitazungumza kidogo juu ya ngazi hii ya pili, tutakapoangalia vifungu vinavyohusiana nayo. Lakini ni ngazi ile ya tatu ambayo mafundisho yao yanakazia, kwa hiyo kwa upana zaidi tutakuwa tunatazama ngazi ya mwisho, kwa vile ndiyo hasa inayowakilisha udanganyifu na hatari kubwa.

Ni namna gani roho hizi mbaya zinatambulikana na watu kukabiliana nazo? Sawa, kwa wale ambao wanaamini kuwa wameitwa ili kuhusika na aina hii ya vita, wanatumia muda wao mwingi katika maombi kutafuta kutambua kwa njia za karama za kiroho na “upambanuzi”, jina au aina ya roho (moja au zaidi ya moja) iliyoshikilia eneo fulani – inaweza ikawa ni roho ya kiburi, uchoyo, tamaa mbaya au uchafu, ndipo tena wanakabiliana nayo katika vita vya maombi na kuzifunga nguvu zake – hii inaweza ikachukua siku kadhaa au wiki kadhaa. Ili kutambua ni roho gani inatawala juu ya mji, wanafundisha pia haja ya kile wanachokiita kuwa ni “kutengeneza ramani za kiroho”, kazi ambayo inahusisha uchunguzi wa historia ya mji – hali ya mji huo kidini, kijamii na kikabila, na historia ya nyuma, hali kadhalika kuhusu matendo maovu yaliyofanywa katika mji huo, au kufanywa na mji huo, au yaliyofanywa dhidi ya mji huo – kurudi nyuma miaka zaidi ya mia au kama si elfu na zaidi! Inafundishwa kwamba tendo hili litatusaidia sana kuzitambua ni roho chafu za jinsi gani zinazoshikilia mji kwa nguvu sana ili kwamba tuweze kuomba kwa ufanisi dhidi yake na kisha kuzifunga nguvu zake! Nilishughulikia juu ya hoja hii ya kiushirikina katika ile makala yangu ya kwanza.

Baadhi ya hawa wahubiri wa kisasa wanasema kwamba hawataweza kuhubiri Injili katika eneo lolote lile hadi kwanza wawe wametambua roho mbaya zinazotawala na wakazifunga nguvu zake. Lakini sasa Yesu hakutumia mtindo huu katika mji wowote aliouendea. Hatusomi chochote kuhusiana na mtume Petro au Paulo akishiriki katika aina hii ya “vita vya kiroho” kabla hajautembelea mji wowote ule; au kuhubiri Injili hapo. Hatusomi chochote kile kuhusiana na mtume Paulo kuzifunga roho za uzinzi, uchoyo au tamaa mbaya kule kwenye miji ya Efeso au Korintho kabla hajaanza kazi yenye nguvu hapo. Wala hatusomi popote kwamba katika nyaraka zao kuwa mitume hao waliwasihi watakatifu kuomba dhidi ya roho za kimaeneo, kama hawa waandishi na wahubiri wa kisasa wanavyotutaka sisi tufanye!

Makosa Mawili ya Kimsingi

Fundisho hilo siyo tu kwamba ni nyongeza kwa Maandiko, bali kwa kweli linaielezea vibaya na kuidhoofisha kazi yote ya Kristo pale Kalvari na jinsi Injili ilivyo. Na tutaanza kwa kuyatazama makosa mawili ya kimsingi ambayo mafundisho hayo yanawatumbukiza watu ndani yake.

Kwanza, fundisho hili linakanusha au kupunguza ushindi mkamilifu ambao Yesu aliutimiza pale msalabani. Mafundisho yenyewe hauyakiri kikweli ushindi halisi ambao Kristo ameupata dhidi ya nguvu zote katika ulimwengu wa roho, kwa niaba ya kanisa lake, kadhalika na kwa ajili ya wanadamu, wala hawa walimu hawaheshimu kikweli na kujali mamlaka zote na haki ambazo Mungu anazo za kuwaelekezea watu wake na kujenga kanisa lake.

Kabla ya pale Kalvari, Yesu mwenyewe alikuwa akitembea huko na huko akihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu. Hali kadhalika aliwatuma mitume pamoja na wanafunzi kuhubiri Injili ya ufalme wa Mungu na kuwatoa watu mapepo na kuwaponya wagonjwa. Akiwa amepokea msamaha na ushindi juu ya majeshi ya uovu pale msalabani, Kristo aliita, akatuma na akawatumia mitume vile vile na watu wengine katika kulijenga kanisa lake. Tunajua kuwa watu wengi waliokolewa kupitia mahubiri ya mtume Petro. Filipo alitumwa na Mungu kuwageuza wengi watokane na dhambi na uchawi. Matendo 8. Na katika ile Matendo 11:19-21, tunasoma kuwa, “… mkono wa Bwana ukawa pamoja nao, wao … waliohubiri Yesu ni Bwana kwa mataifa na watu wengi wakaongezeka upande wa Bwana”. Mtume Paulo aliitwa na Mungu, Matendo 26:13-18; katika ile Matendo 13:2 mtume Paulo alitumwa na Mungu. Watu hawa wote walihubiri neno la Mungu kwa watu wengine, wakikiri kile ambacho Kristo amekifanya pale Kalvari na watu wengi walimgeukia Bwana. Mitume waliwakomboa waume kwa wake pia kutokana na roho za uovu na waliyakemea mapepo yaliyokuwa yakitenda kazi ndani ya mtu mmoja mmoja. Matendo 13:8-11; 16:18; 19:12. Hayo yote yalitokea pasipo hata kupata mafundisho yahusuyo na pasipo matumizi ya mtindo huu wa kisasa ambao unaitwa “mapambano ya kimkakati”

Hebu niseme hapa kwamba inapaswa iwe wazi kwetu, kwamba sio mahubiri yoyote na kila mahubiri huwa na ufanisi. Mtume Paulo alikuwa makini katika kumhubiri Kristo, lakini yeye alijikabidhi mwenyewe kwa ndugu zake pamoja na kwa kanisa, naye alikuwa tayari kurejea nyumbani kwake katika mji wa Tarso, Matendo 9:26-31. Baadaye tunamkuta kama mmoja wa manabii na walimu huko Antiokia, Matendo 13:1. Paulo hakuhubiri tu mahali popote pale kulingana na mipango yake na ubunifu wake, bali akiwa na ushirika na Mungu na akimtii Roho na kanisa, Paulo aliitwa na Mungu kuihubiri Injili, Matendo 13:1, na alielekezwa na Roho maeneo ya kwenda na maeneo ya kutokwenda, Matendo 16:6 – 10. Hivyo mtume Paulo anasema katika Warumi 10:14 – 15. “…basi wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikiaje pasipo mhubiri? Tena wahubirije wasipopelekwa?” Mtume Paulo pamoja na wenzake walikuwa makini sana kuhusiana na wito huu wa kimungu – 1 Kor. 9:16,17 na alikuwa makini zaidi pia kuwa angeweza kufanya kazi vizuri tu kulingana na wito wake, 2 Kor. 10:13-18.

Ikiwa tutaenda mbali na wito wa Kimungu na karama; ikiwa tutaenda mbali na muda wa Kimungu katika maisha yetu; ikiwa tutaenda mbali na Neno la Mungu – basi tusitegemee kupata matunda ambayo Mungu anayategemea kutoka kwetu. Tunapaswa kuwa watumishi wa Mungu, hii ina maana kwamba tunatakiwa kufanya yale tu anayoyasema na kujikabidhi kwenye maelekezo yake na muda wake katika maisha yetu. Hatutakiwi pia kwenda mbali zaidi ya karama na wito wetu. Hii inaweza kuwa pengine ndiyo sababu wengine wanaenda pasipo kupelekwa? Inaweza kuwa ndiyo sababu kwamba wanapata mafanikio kidogo au hawaoni mafanikio kabisa kutokana na mahubiri yao. Juhudi ya jinsi hii ya wahubiri wasio na subira wanatafuta sasa kutunga au kubuni mtindo fulani au mbinu ambazo zitaifanya kazi yao iweze kufanya kazi vizuri na kuleta “mafanikio”! Inaweza ikawa ndiyo sababu wanaenda mbali zaidi ya yale ambayo yanafundishwa na Maandiko ili kwamba wapate haya? Ninafikiri kuwa mambo hayo pia yanachangia katika jambo hili lote la UInjilisti wenye mafanikio pamoja na kushughulikia “mbinu mpya”. Hii yote haimaanishi kuwa ikiwa tumetumwa na Mungu, basi siku zote tutaona ‘matokeo makubwa’, bali ikiwa tuna shauku ya kumtumikia Mungu na kumzalia matunda na kiukweli kupeleka Neno lake kwa watu, basi tutaenenda kwa kufuata Neno lake na Roho wake.

Kama tusomavyo Injili na Matendo ya Mitume, tunaona kwamba watu wa Mungu walihubiri na kushuhudia juu ya kifo chake na ufufuo katika utii wa amri zake na maongozi yake au kwa kadiri fursa zilipojitokeza. Ijapokuwa walifahamu kuwa Kristo ameangamiza mamlaka na uwezo, haina maana yoyote, kama tusomavyo katika habari zao, kwa watu wa Mungu kuchukua UInjilisti “katika mikono yao wenyewe” na kujaribu kuifanya kazi ya Mungu kwa ajili yake. Mitume hawakufanya mambo kwa kukisia pale walipokuwa wakilitumia neno la Bwana au walipotumia uwezo na mamlaka ambazo aliwapatia. Walimtii Mungu na Mungu aliwarejesha wengi kwake na akadhihirisha nguvu zake kuu. Na Mungu aliupata utukufu! Hayo yote yalitendeka pasipo hata kuzitambua au kuzifunga roho za kimaeneo! Hawakujaribu kuongezea chochote kile juu ya yale ambayo Mungu alisema na kuyafanya ili kuufanya uInjilisti uwe wenye mafanikio zaidi! Lakini hawa walimu wa kisasa pamoja na wahubiri wanathubutu kuonyesha kwa mafundisho yao, kwamba yale ambayo Kristo aliyafanya pale msalabani hayakutosha. Ndiyo, wanatangaza kwamba Kristo alipata ushindi pale msalabani, lakini inaonekana kana kwamba hakuzivunja mamlaka na enzi vya kutosha kwa ajili yao, kwa sababu wahubiri hawa wanaamini kuwa roho chafu bado zina haki kisheria kuwashikilia watu katika giza na kifungo na kuwa Injili haiwezi kupenya katika eneo linalotawaliwa na roho hizo. Wanafundisha kuwa mtu anahitajika kwanza kufanya “vita vya kiroho” ana kwa ana na mamlaka hizo pamoja na nguvu hizo kwa maombi, hadi kuzishinda nguvu zake kupitia maombi kwanza, kabla Mungu hajazirejesha roho za watu kwake! Mawazo ya aina hii kwa hakika ni ya jamii ya kiushirika tu na yenye milki ya ulozi zaidi kuliko kuwa na mawazo ya kimaandiko. Mtazamo huu juu ya aina hii ya roho ya kimaeneo pamoja na uwezo wao pamoja na aina hii ya kuzingatia katika maombi dhidi ya roho ya uovu, hayapatikani katika maandiko ya neno la Mungu. Mtazamo huu unaweza kumtukuza ibilisi kwa namna itakayowanyima watu wa Mungu ufahamu wa kweli na nguvu ya Kristo ndani ya watakatifu wake na kupitia kanisa lake. Inawafanya watu wamfikirie shetani zaidi badala ya kuweka mawazo yao kwa Kristo, na kwa jinsi hiyo wanampatia shetani uwezo zaidi na utukufu na kuwanyang’anya watakatifu ile imani yao ya kweli katika Mungu. Maandiko yanasema kwamba, “Ijapokuwa hatujayaona mambo yote yakitiishwa chini ya nyayo zake, lakini tunamwona Kristo.” Amina! Lakini sasa, badala yake walimu hawa wa kisasa wanatutaka sisi tuyaone mapepo! Ni mafundisho madhaifu na manyonge kama vile yenyewe yalivyo si ya kibiblia. Na hao walioyahamasisha mafundisho hayo ndio huwa wa kwanza kukubali katika vitabu vyao kwamba watu wameharibiwa walipokuwa wanajaribu kutumia mbinu hizo. Mafundisho hayo ni kashfa dhidi ya mamlaka ya Mungu na shambulizi dhidi ya ushindi kamili wa Kristo alioupata pale Kalvari, ambao ndio unaomruhusu kulijenga kanisa lake kulingana uradhi wa mapenzi yake mwenyewe. Katika uweza ambao Mungu aliutumia katika kumfufua Kristo kutoka katika wafu. (Efe 1: 19-23)!

Ndiyo tunatambua kile kinachofundishwa na maandiko, kwamba mfalme wa uweza wa anga ni ile roho itendayo kazi sasa katika wana wa uasi; Efe 2:2. Shetani huzungukazunguka kama simba angurumaye akiwafunga wengi kuyatenda mapenzi yake na hafanyi lolote isipokuwa ni kuua, kunyang’anya na kuharibu. Yeye hudanganya na kuwafunga wengi katika vifungo. Mambo hayo pamoja na mengineyo yanafundishwa ndani ya maandiko, na wala hiyo sio hoja yetu tena hapa. Nami sisemi hapa kwamba hatuwezi kuomba kwa Mungu, kuhusiana na mambo ya aina hii; wakati ambapo tunajua hali na watu ambao wanahitaji neema ya Mungu, rehema pamoja na wokovu wake. Lakini linapokuja jambo la uenezi wa Injili na jinsi inavyoenezwa na kubadilisha maisha ya watu, ndipo tunaweza kusema kuwa mafundisho hayo ya kisasa yameenda nje ya maandiko, na yametumbukia katika kasoro na udanganyifu – yanawafanya watu wawe shabaha ya roho za udanganyifu. Wanakubali kuwa Kristo amepata ushindi pale kalvari dhidi ya shetani, lakini bado wanaamini kwamba wanatakiwa pia wapate ushindi zaidi juu ya roho zinazotawala ju ya maeneo yote yanayokaliwa na watu.

Ni nini kinaipatia roho hizo za kimaeneo haki ya kisheria kukamata mamlaka za aina hii juu ya watu, kiasi kwamba hata iifanye Injili isiwe yenye mafanikio katikati yao? Haya ati wanasema ni zile dhambi zilizopita za jumuia hiyo au mkoa na ile laana iliyowekwa juu yake kwa sababu ya dhambi hizo! Napenda niwaambie ukweli, wanachokifanya hawa walimu wa kisasa ni kuzijaza akili za watu wa Mungu mambo yasiyo ya kiInjili yenye ushirikina mtupu na yenye kasoro nyingi. Kristo amezichukua dhambi za ulimwengu mzima na amelipia gharama kubwa isiyohesabika ili kufanya hayo. Kristo ni mwenye mamlaka zote za juu – ni Mkuu. Shetani anaweza tu akaenda pale ambapo Mungu amemruhusu kwenda. Sawa, maandiko yanakiri kuwa ipo haja ya maombi, kuhubiri, uInjilisti, kazi pamoja na ukombozi wa mtu mmoja mmoja kutokana na mapepo; lakini kadiri ya haja ya kuihubiri Injili inavyohusika, bado maandiko hayakiri kwamba kuna haja ya toleo lingine zaidi ya lile alilolinunua tayari Kristo pale msalabani kwa ajili ya ulimwengu wala maandiko hayakiri kwamba “dhambi zile za kihistoria” zilizopita za maeneo ndizo zinaipatia roho za kimaeneo haki ya kisheria kuzuia Injili; wala pia maandiko hayakiri kuwa ipo haja ya watakatifu kujiingiza moja kwa moja katika makubaliano ya kiroho na hizo roho za kimaeneo kana kwamba roho hizo zinahitajika kufungwa kabla ya Injili kufanyika na kuenezwa kwa mafanikio yanayopaswa ( tafadhali angalia makala yangu ya kwanza ambamo jambo hili limeelezwa kwa undani zaidi ).

Wakati mtume Paulo alipokuwa Athene, hawakupatikana watu wengi waliomgeukia Mungu lakini pamoja na hali hiyo, si Paulo mwenyewe wala si maandiko ya Neno la Mungu yanapohesabu hali hiyo ya watu kutoipokea Injili kuwa ilisababishwa na nguvu kuu na mamlaka au haki ya roho za uovu kupinga Injili au kazi ya Mungu. Mtume Paulo hakuianza kuzishughulikia roho za kimaeneo katika maombi kwa sababu ya kuonyesha “upungufu wa mafanikio” katika huduma yake. Mtume Paulo alikuwa na ufahamu mkubwa zaidi na mafunuo kuliko hawa walimu wa kisasa, lakini yeye hakukimbilia kwenye “mbinu za kiwango cha kimkakati” ili kuzishinda “roho ya kuabudu sanamu” ambazo zilidhaniwa “kutawala” katika mji wa Athene, katika jitihada yake ya kuushinda upungufu huu wa mwitikio katikati ya watu. Unaona, hawa walimu wa kisasa wao wanasema kwamba, watu kwa kweli hawapo huru kuitikia Injili hadi hapo tutakapokuwa tumezifunga roho za kimaeneo! Mmoja wa waandishi, kwa kweli anapendekeza kuwa roho za kimaeneo zinazotawala kule Athene, zilikuwa zenye uwezo mkubwa kiasi kwamba zilimfanya mtume Paulo kuzishindwa na eti hiyo ndiyo sababu alipata mafanikio kidogo sana huko! Lakini sio Paulo wala maandiko ya neno la Mungu yanayohitimisha jambo hilo kuhusu aina hii ya “upungufu wa mafanikio”. Badala yake, mtume Paulo yeye anaendelea mbele na safari yake kwa mapenzi yake Mungu na mpaka anapoingia katika mji wa Korintho, hatuoni popote pale panapomuonyesha akijishughulisha na kazi ya kuzifunga roho za kimaeneo, na bado watu wengi sana walimgeukia Bwana. Maandiko hayaelezei sababu hasa inayofanya watu wengi zaidi wamgeukie Bwana katika eneo moja kuliko jingine, lakini yanatupa vidokezo na kutuelekeza kwenye kanuni fulani fulani, ambazo tutaziangalia hivi punde.

Lakini jambo moja lenye uwazi ni kwamba maandiko hawayahesabii “mafaniko” au “kupungua kwa mafanikio” kwamba imetokana na mtu mmoja ambaye ameweza kuzishinda roho za kimaeneo zinazotawala au la.

Ninadhani kuwa kama hawa walimu wa kisasa wangekuwepo kule nyakati zile za Paulo alipotembelea Athene, wangeweza kushauri kuwa Paulo aweze kuhudhuria masomo katika moja ya seminari ya Kithiolojia ili aweze kujifunza kwanza “kanuni za kukua kwa kanisa”. Pengine wangeweza kumwelezea pia kuwa mtindo wake anaoutumia katika UInjilisti bila shaka “haufanyi kazi” vizuri na hivyo anapaswa kuzisomea “mbinu mpya za mafanikio” ya uenezaji wa Injili, ambazo ndizo zimethibitishwa kuleta mafanikio! Wangeweza kumwambia kuwa yote aliyoyafanya amekosea kwa sababu tatizo halikuwa ni Wathene binafsi isipokuwa ni ile roho ya kieneo ya kuabudu sanamu ndiyo iliyokuwa inawazuia watu kule wasiweze kuiitikia Injili. Mtume Paulo angelazimika kufundishwa vita vya kiroho iwapo angependa kuona mafanikio katika kuieneza Injili! Angepaswa kujifunza kuhusu kutambua majina ya roho chafu za kimaeneo na namna ya kuzikabili katika kuzifunga kwa maombi! Asingetazamia kupata mafanikio hadi kwanza afahamu jinsi ya kuyafanya mambo haya! Lakini sasa hebu fikiria jinsi Paulo alivyoweza kuwashughulikia walimu wa uongo walionyemelea makanisa ya Galatia; sifikirii kwamba angeweza kuvutiwa kwa vyovyote vile, badala yake angeweza kuwakemea kwa nguvu kwa ajili ya kuichafua Injili ya Kristo.

Hii ndiyo sababu inayonifanya niseme kwamba, mafundisho hayo wanayotuletea ni kashfa dhidi ya mamlaka na busara za Mungu, ambaye huwaita na kuwatuma watu kwenda kuhubiri Injili kulingana na amri na mafundisho ambayo ameyaweka kwa ajili yetu. Hawa waandishi wa kisasa wanaweka busara yake Mungu na mamlaka za utawala wake katika maswali. Wangeweza kuiita huduma ya Paulo kwa ajili ya watu wa Athene ni jambo “lililoshindwa”. Wako makini kutafuta mafanikio kiasi kwamba wanadiriki kuisukumilia mbali amri ya Kristo – ya kwenda ulimwenguni kote kuihubiri Injili – sasa kinyume chake wao wanazunguka huku na huko wakianzisha amri zao wenyewe, na hivyo wanajiweka kinyume na busara za mamlaka ya Mungu na utawala wake juu ya mambo haya.

Hata kama Mungu alibariki au kama aliwaruhusu waweze kujaribiwa, hata kama kulikuwa na mwitikio mkubwa wa watu au kidogo – bado mitume wa mwanzoni kabisa, wao pamoja na kanisa waliendelea kumwangalia Mungu; wakijikabidhi kwake, wakimwamini yeye na kumtukuza yeye! Hivyo ndivyo walivyofanya! Na kama hapakuwepo na mwitikio sana, hawakumtilia shaka Mungu na kuanza kukimbia huko na kuko kujifunza na kubuni “kanuni mpya za ukuaji wa kanisa”! Wao walikuwa wakiomba na wakihubiri na walikuwa imara katika imani na upendo; kama vile tusomavyo katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini wao pia hawakujishughulisha katika aina ya maombi yanayohusika na kuzishambulia roho za kimaeneo kama ambavyo inavyohamasishwa na waandishi hawa wapya.

Ijapokuwa wanakiri juu ya ushindi wa Kristo pale Kalvari, lakini mafundisho yao hayo yanaufanya wokovu wa roho za watu uonekane kuwa unategemea matokeo ya aina fulani ya mapambano ya ana kwa ana kati ya majeshi ya kiroho ikiwepo roho chafu kwa upande mmoja, ikipambana na karama za Roho na maombezi ya Wakristo kwa upande mwingine; vita hiyo inayoelezwa humo ni ubunifu wa akili zao wenyewe tu ( ambayo wanaiazima kutoka kwenye milki za ulozi. Vitabu vya ubunifu – kama vile kitabu cha Frank Perret ) na vinajaribu kuongezea kitu kingine juu ya ushindi ambao Kristo aliupata pale Kalvari (msalabani). Katika maandishi yao, wakati mwingine inatolewa mfano wa nguvu za upinzani zilizo sawa sawa zikipigana dhidi ya roho. Wanaonyesha kuwa iwapo hutazishinda roho za kimaeneo zilizo za kienyeji na za kimaeneo zinazomiliki eneo fulani, basi kazi ya Injili na wokovu wa nafsi haiwezi kufanikiwa ipasavyo. Katika kutimiza hamu yao ya kupata “mitindo ya mafanikio”, wahubiri hawa pamoja na waandishi wao hawajikabidhi katika Neno la Mungu na maelekezo yake ambayo Yesu ameyakamilisha pale msalabani – wanafanya hayo yote kwa ajili tu ya kutafuta matokeo. Nasema tena kwamba mawazo hayo ni ya kuanzishwa toka duniani, hayamtukuzi Mungu, badala yake yanatukuza mafundisho yasiyothibitishwa ambayo husababisha machafuko na kukata tamaa, na zaidi ya yote yanamtukuza shetani.

Mafundisho yasiyothibitishwa ambayo husababisha kuchanganyikiwa na kukata tamaa.

Lakini hebu niseme hapa kuwa shauri lao halijathibitishwa! Bila shaka haionyeshi kwamba wanaweza kwa kweli kuonyesha kuwa jamii imebadilishwa kutokana na mafundisho hayo yao. Zaidi ya hayo yote, wengi wa mashabiki wa mafundisho hayo wanaishi Marekani (USA). Je huko kwao yameleta mabadiliko gani? Mchungaji mmoja wa kanisa moja kubwa kule New York aliwahi kuandika kitabu kuhusu kazi za kanisa lake na jinsi Mungu alivyopambana na mafundisho haya ya kisasa – na jinsi hata yeye alivyoumizwa katika moyo wake kuona jinsi ambavyo dhana hii isiyo ya kibiblia inavyoweza kushikilia akili za watu wa Mungu na inaendelezwa kufundishwa nchi nzima. Lakini analiweka swali lile lile na linalofanana – kuelezea ni kwa nini basi, iwapo mafundisho hayo ni ya ukweli, mbona hayabadilishi miji ya Amerika – tunaambiwa na watu wengine kuwa California ya kusini ni mji unaowakilisha kituo cha vivutio vya matamanio katika ulimwengu. Yako wapi basi mabadiliko hayo makubwa katika miji ya Marekani iwapo mafundisho hayo ni ya ukweli? Lakini mtu mwingine anaweza kuuliza hivyo hivyo kuhusu miji mingine mingi pamoja na nchi. Mafundisho hayo hayo yamekuwa yakiendeshwa Uingereza karibu miaka 15 sasa kwa kadiri ninavyofahamu, lakini sasa, yako wapi – basi mabadiliko hayo makubwa yaliyoahidiwa na mafundisho hayo? Ninafikiri kuwa watu wengi wangekubali kwamba, sio jamii tu yenye hali mbaya, isipokuwa kanisa leo limo katika hali mbaya zaidi; kwa kusema kwa ujumla, liko katika hali mbaya kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita. Tendo mojawapo lililosababisha machafuko, matengano, maumivu ya mioyo, kuchanika kwa makanisa, kadhalika na kugawanyika kwa makanisa, je huko ndiko kuzaa kwa wingi kwa imani hiyo mpya!

Mashabiki wa mafundisho hayo wametengeneza mkanda wa video, ili kuwashawishi watu waone namna ambavyo vita hivyo vya kiroho vinavyoleta mafanikio. Baadhi ya watu wengine ambao wamechunguza yale yanayodaiwa na mikanda hiyo ya video, kwa kuzuru hadi kwenye maeneo hayo waliyo chukulia mkanda huo pamoja na kupata habari sahihi za maeneo hayo, wanatuambia kuwa mambo mengi, yaliyodaiwa ndani ya mikanda hiyo yametiwa chumvi – na mara nyingi ni habari za uongo. Wale wanaoamini katika imani au mafundisho hayo, kwa uasili wa kutosha wanaamini kwamba “inafanya kazi” na wanajaribu kuonyesha watu kuwa ni kutokana na mtindo wao mpya wa kuomba dhidi ya roho za kimaeneo, ndiyo iliyoleta mafanikio makuu pale Injili ilipobanwa katika jumuiya fulani fulani. Lakini hatuoni kuungwa mkono na maandiko ya Neno la Mungu katika maeneo hayo; na wala haiwezi ikaonyeshwa kuwa hilo limekuwa ndiyo “ufunguo” au “jawabu” la ufanisi wa uInjilisti kwa namna ya kimatendo, mbali ya malalamiko ya hadithi zao.

Kwa kweli kitabu kimeandikwa ambacho nimekitaja hapo punde tu, kwa usahihi kabisa ni kwa sababu kumekuwepo na machafuko pamoja na maumivu ya moyo yaliyosababishwa na mafundisho hayo. Mwandishi wa kitabu hicho yeye mwenyewe pia anaamini katika vita vya kiroho dhidi ya roho, lakini anatueleza kuhusiana na kukata tamaa pamoja na hofu iliyowanyemelea wakristo waliokuwa na matazamio ya hali ya juu ya mafanikio kutokana na mafundisho hayo. Lakini hatimaye waligundua kuwa haikufanya kazi yoyote; ile kama walivyotarajia na hata ikawasababishia majanga! Hali hiyo imewasababishia kujisikia ni watu wawezao kunaswa na shida, hofu na machafuko! Ingawaje anajaribu kuonyesha kuwa mambo yaliwaharibikia kwa sababu ya ongezeko na ujinga wa watu wenyewe wa kutokujua kanuni za aina hii ya mapambano; mbali ya hayo yote kitabu hicho pia kinakazia ukweli kwamba, upepo huu mpya wa imani sio huo ambao mashabiki wake wamelalamikia kuwa ndio, na wala hautoi matokeo kwa namna ambayo hawa waandishi wapya wangetupelekea sisi tuamini hivyo.

Katika kitabu chake cha “Roho za Kimaeneo”, (kurasa za 17, 18), Wagner anakiri kuwa katika hali nyingi mtindo huu hautoi matokeo yanayokusudiwa. Anatoa sababu gani hapo? Haya, anatueleza kuwa shetani “anapinga mwenendo wa mambo”. Je, hii ina maana kwamba huyo shetani ana uwezo mkubwa kiasi kwamba watu hawawezi kuokolewa? Hapo haelezei kwa ufasaha. Lakini anatuelezea kuhusu uwezo, na werevu alionao na kwamba shetani anawapinga watakatifu, kupitia roho zenye kiwango cha ngazi tofauti; ili watu wasitambue mapenzi ya Mungu ipasavyo! Na kwamba kwa kadiri kiwango cha roho za kimaeneo kinavyozidi kuwa juu zaidi ndivyo nguvu zaidi zinahitajika ili kuzishinda! Hali kadhalika anatuambia kuwa Wakristo wengi hawajajiimarisha ili kukabiliana na aina hii ya roho za viwango vya juu. Kwa hivyo basi inaonyesha shetani anaweza kuzuia watu kuyatambua mapenzi ya Mungu katika mapambano haya; na hata kama watatambua aina ya roho zinazopaswa kushughulikiwa bado watu wengi hawana msimamo wa kiroho ili kuyashinda. Jambo hili humpatia mtu utukufu na humpatia pia uwezo mwingi shetani. Kwa hiyo hitimisho tunalolipata hapo ni kwamba wokovu wa roho za watu unategemea aina fulani ya watu walio jaliwa kuwa na uwezo wa kutambua mambo katika “ulimwengu wa kiroho”. Pasipo uwezo wa “kutambua” jina na tabia ya roho za kimaeneo na pasipo uwezo wa kiroho wa mtu binafsi pamoja na msimamo wa mtu binafsi kuyashinda hayo katika maombi – hakutakuwepo na ufanisi wa UInjilisti! Hakika, kama utasadiki porojo hizo zisizo na msimamo wa Kibiblia, basi wewe unaweza kuamini lolote lile! Ili kuonyesha jinsi mafundisho haya yanavyokaribia kuingia kwenye ulozi, hebu uniruhusu ninukuu yale anayoyasema mwishoni mwa ushauri wake hapo juu; anasema kuwa, “…. tunapogundua kuwa sisi ni muhimu katika kuzifunga (roho za kimaeneo) ….. tutafanya vema kutafiti uwezekano wa chanzo chake katika ulimwengu wa kiroho”. Kutafuta chanzo, na sio katika maandiko, isipokuwa katika ulimwengu wa kiroho! Je wanatutaka sisi tuwe waaguzi, wachawi au waangaliao mambo ya roho? Pasipo kuelewa, hivyo ndivyo inavyotendeka katikati yao. Wao hawaenendi kiroho, haupo utambuzi wa kiroho na kweli, hii sio maombi ya kiroho. Hivi sio vita vya kiroho – huu ni udanganyifu. Wanafanya mawasiliano ya kiuharamu na yenye hatari na ulimwengu wa maroho na hivyo hudanganyika (ninaposema ulimwengu wa kiroho ninamaanisha kuwa wanafanya mawasiliano na maroho maovu, au kujiweka katika hali inayoweza kuwashawishi na kudanganywa na maroho maovu). Tutaangalia zaidi kidogo hilo hapo baadaye kidogo. Lakini sasa hapa tunaona kwamba ili kuweza kusimulia kushindwa kwa mafundisho yao pamoja na maumivu ya moyo yaliyosababisha – wanatafuta kiurahisi tu kubuni makosa zaidi.

Niruhusu nitaje hapa yale ambayo nimewahi kuyasema mahala penginepo yaani, tunajua kwamba Bwana analijenga kanisa lake na anayaheshimu mahubiri ya neno lake na hakika hujali anapoona watu wake hujinyenyekeza wenyewe katika maombi na kuutafuta uso wake kwa mioyo yao yote. Inawezekana kuwa Mungu anafanya kazi katikati ya watu ambao baadhi yao viongozi wao huamini katika mafundisho haya na kuyashikilia, lakini kazi yake ya neema haiwezi kuhalalisha mafundisho hayo yote ambayo yameshikiliwa na watu ambao wanaweza wakawa ndio wanaoongoza kazi mahala fulani. Tunajua hivyo kutokana na historia, pia tunaweza kuziona kanuni hizo sisi wenyewe ndani ya maandiko pia. Lakini napenda niseme tena kuwa kule kuona Mungu akitembea katikati ya watu katika uweza wa kuokoa, haihalalishi kila mafundisho yaliyoshikiliwa na hao wanaokuwa katika uongozi wa sehemu fulani, na wapo mbali sana katika kuonyesha kuwa mtindo wao huo mpya kwa kweli unafanya “kazi” au kwamba mtindo huo ndio unaohusika katika kuwaleta watu wengi katika ufalme wa Mungu.

Katika mambo ya matukio ya kiroho ya nyuma na katika kujua kwa nini mambo hutokea au kutotokea, mara nyingi maandiko hayatoi jibu la maswali yetu au kufunua kila kitu. Na kutokana na hoja hiyo, Mungu anatuonya katika Kumbukumbu la Torati 29:29 kwamba “mambo ya siri ni ya Bwana Mungu wetu, lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele”. Hatutakiwi kupenyeza tu katika mambo ambayo Mungu hajatufunulia kwa neno lake. Ni busara zake Mungu, kwamba ameyaweka mambo fulani mbali na ufahamu wetu. Lakini tunatakiwa kuyazingatia kikamilifu mambo ambayo ametufunulia tayari. Hayo yatakuwa ni yenye kutuletea faida kwetu – katika kukuza ufahamu wa Mungu na kuimarisha imani yetu. Lakini katika jitihada zao za kupata matokeo wakati wote na katika sehemu zote, hawa wahubiri na walimu wa kisasa wanapenyeza kwenye mambo yasiyoonekana – ambamo wanajigamba juu ya maono yao, mafunzo yao, na uzoefu wao wa mambo ya juu – ambayo ni mazao ya akili zao za kimwili tu na wala hayailetei jamii mabadiliko katika maisha yao. Kama tunavyoambiwa katika Kolosai 2:18 na wala hawashikilii kichwa cha kanisa, Yesu Kristo. Ijapokuwa Mtume Paulo anaongelea maalum kuhusu wale wanaotafuta kuwarejesha watakatifu kwenye mila za kiyahudi, ile sura nzima Kolosai 2:6-19 inashauri sana juu yetu, kuhusiana na mambo haya ya mafundisho mapya.

Ulinganifu wa kimaandiko – kanisa katika kuomba.

Nyakati za matendo ya mitume kanisa lilijiheshimu na kuomba kwa jinsi ya tofauti kabisa ukilinganisha na hawa walimu wa kisasa wanavyoamuru. Kulipotokea mateso kule Yerusalemu, kanisa halikukabiliana na roho chafu katika maombi yao.

Kanisa halikukiri juu ya roho za kimaeneo kwamba ndizo zinazowashikilia wanaume na wanawake hata wasiupokee ufalme wa Mungu. Wao waliomba kwa Mungu na kukiri juu ya mamlaka zake na uungu wake. Kulikuwepo na upinzani mkali wakati huo ( kuliko hata ilivyo sasa naweza kusema ) juu ya kuihubiri Injili; naye ni nani anayeweza kupinga kwamba shetani anachochea ugumu wa mioyo ya hao wasiotaka kuamini ili wapinge kazi ya Mungu? Lakini sasa hebu sikiliza jinsi kanisa lilivyoomba katika Matendo 4: 24-30, kwanza walitangaza busara kuu na uweza, wa Mungu juu ya yote mengine, wakipokea maelekezo na hamasa kutoka katika maandiko ya neno la Mungu! Ndipo wakatangaza:

“. . . Basi sasa ee Bwana, yaangalie matisho yao, ukawajaalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyoosha mkono wako kuponya, ishara na maajabu zikafanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu”.

Hebu tazama hapo watumishi hao wametishwa, lakini maombi yao yameelekezwa kwa Mungu, wala hawayaelekezi dhidi ya aina yoyote ile ya roho za kimaeneo zinazotawala Yerusalemu, wanayohisia juu ya mamlaka za Mungu na za ushindi wake juu ya mambo yanayowapata, na wanaomba sio kwa ajili ya kukabililiana na roho za kimaeneo ili kwamba ziweze kufungwa, lakini wao wanaomba ili kwamba waweze kulisema neno lake kwa ujasiri na kwamba Bwana aweze kutenda kazi kwa nguvu katikati yao. Lakini hata hivyo wanakiri juu ya mamlaka za utawala wa Mungu na ushindi wake kupitia Kristo. Hayo hayawaelekezi kufuata mambo ya kuhisihisi – wao hawachukui kutoka kwa Mungu ule uweza wake mkuu na kutafuta kumtumikia kwa ajili ya kutimiza matakwa yao na mipango yao kwa ajili ya ukuaji wa kanisa. Isipokuwa wanabakia wakiwa wamejikabidhi kwa Mungu na katika busara zake wakikiri kuwa wao ni watumishi wake tu. Hilo ndilo kanisa ambalo linamwinua Yesu juu zaidi kuliko chochote kile. Na ijapokuwa wanadamu na mapepo wanaweza kupanga, wao wanaendelea kubakia wakiwa wamekaza macho yao kumwelekea Kristo- na kile alichokikamilisha kupitia kifo chake na ufufuo wake – yote mawili katika fikara zao na maombi yao. Hawatafuti kuongezea chochote kile juu ya ushindi kamili pale Kalvari, au kunyang’anya uwezo wake na maana yake kwa kuhesabia uwezo huo juu ya “roho za kimaeneo” ambao hawanao! Maombi yao yanakazia macho kwa Kristo na mamlaka zake na wanamtukuza yeye, sio shetani au roho za kimaeneo.

( Kuhusiana na maombi na kanisa, vile vile na kuhubiri Injili kama njia ya Mungu ya kuokoa hao waaminio, tafadhali soma sehemu ya pili ya makala ya kwanza ya “Kutubu kwa ajili ya Dhambi za Taifa”)

Na ni kweli tunaona kwamba wanayo sababu nzuri inayowafanya wafikiri na kuomba namna hiyo. Katika Wakolosai 2:15, tunasoma kuhusu kifo cha Kristo pale Kalvari kwamba; “… akisha kuzivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri akazishangilia katika msalaba huo”. Na kwa hiyo Mungu alikuwa na uwezo wa “kutukomboa kutokana na nguvu za giza na kutuingiza katika ufalme wa mwana wake mpendwa”.

Na katika Waebrania 2:14 tunaambiwa kuwa, “Yesu Kristo alishiriki damu na mwili vivyo hivyo;.ili kwamba kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti yaani Ibilisi”.

Na mtume Yohana anakubaliana na hilo pale anaposema katika Yoh 3:8 “… kwa kusudi hili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziharibu kazi za shetani”

Ukuu wa kimungu alilonao Kristo na mamlaka zake juu ya mambo yote umetangazwa katika Wakolosai 1:16. ” kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana, ikiwa ni vitu vya enzi au usultani au enzi au mamlaka, vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake.”

Haupo wito wowote kwa kanisa tena ili kuzidi kuharibu “mamlaka na uweza” kwa kuzifunga na kukemea roho za kimaeneo kana kwamba zenyewe zinayo haki ya kisheria juu ya nafsi. Yesu Kristo alizichukua dhambi za ulimwengu mzima na kwa hiyo yeye ni mwokozi wa wanadamu wote (1Tim 4:10) hata kama wanaamini na kupokea wakovu huo au hapana. Yeye amenunua msamaha na wokovu kwa ajili ya wanadamu kwa damu yake mwenyewe na kwa hiyo imeandikwa kwamba, “Mungu alikuwa ndani ya Kristo ……. asiwahesabie makosa yao…”. Kwa wale ambao wangeweza kuamini Injili na wakapatanishwa na Mungu, Mungu asingeweza tena kuyashikilia dhidi yao mambo yao maovu ya dhambi zilizopita (2 Kor 5:19) isipokuwa yeye huwaachia na kuwasamehe bure – pasipo malipo yoyote. Wale ambao wanaukataa na kuupinga wokovu wa bure wa Mungu na ambao wanaendelea kuzishikilia dhambi zao, watahesabiwa kuwa wanapaswa kuhukumu.

Lakini sasa haya mafundisho yao ya kisasa kwa kweli yanaifanya damu na dhabihu ya Bwana wetu Yesu Kristo pale msalabani ionekane kuwa haina maana. Mafundisho hayo yanamkataa yeye aliye wa kweli na mwenye mamlaka alizozinunua na kuzipata kama mwokozi wa wanadamu wote kupitia kumwagwa kwa damu yake. Kristo amekwishachukua msamaha wa wale wote watakaoamini. Lakini mafundisho haya ya kisasa yanatangua kazi ya msalaba kwa kuzihesabia roho za kimaeneo haki ya kisheria katika kuwaweka watu nje ya ufalme wa Mungu, kwa sababu ya kile wanachokiita wao kuwa ni “dhambi zisizoungamwa na kusamehewa za eneo la kijografia katika mkoa au jumuia.” Wao wanafundisha kuwa roho za uovu bado zina uwezo juu ya eneo lolote lile, ambalo mambo yaliyopita ya kijamii au mengineyo ya uovu uliotendeka. Imani za aina hii zinashikiliwa na kizazi kipya cha roho za wanadamu wa leo; na hapo ndipo imani ya aina hii inakotokea, kuliko kutokea katika Biblia. Wanasema kuwa maovu yaliyopita yanahitajika yapate “ondoleo” (toleo) lake, kwa wakristo kuungama na kuzitubia dhambi hizo, na kutumia damu ya Yesu, kabla roho za kimaeneo hazijaweza kufungwa! Kwa hiyo wanalundika kosa moja juu ya kosa jingine. Jambo hili limetazamwa ipasavyo ndani ya makala yangu ya kwanza.

Ikiwa tutafuata mafundisho hayo yao, tutagundua kwamba kila mtu katika ulimwengu huu sasa hawezi kusamehewa mara moja, wala kuokolewa na kukombolewa kutokana na nguvu za shetani kwa sababu ya msalaba. Hapana; ni kweli kwamba haiwi mara moja kwa haraka. Lakini Kristo akiwa amenunua wokovu huu wa bure na mkamilifu kutokana na dhambi, kuhukumiwa na uwezo wa shetani. Biblia inatangaza kwa nguvu sasa kuwa, “Injili ya Kristo ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye.” Rumi 1:16. Hivyo ndivyo maandiko yanavyofundisha; na kwa sababu ya wokovu hutujia pasipo haja ya kuzitambua na kuzifunga hizo zinazoitwa roho za kimaeneo – isipokuwa kama unataka kubatilisha matokeo ya damu ya Yesu pamoja na ushindi wake dhidi ya mamlaka na uwezo.

Hata hivyo ili kuonyesha kuwa sitii chumvi ule umaana wa jambo hili pale ninaposema kuwa mafundisho haya yanawakilisha mashambulizi juu ya Injili ya Yesu, hebu tutazame kwa makini yale ambayo kiongozi maarufu wa thiolojia hii mpya (George Ottis jr) anavyotangaza. Katika kutoa mhadhara wake kwa kusanyiko la YWAM huko Tacoma, Washingtone mnamo mwaka 1981, yeye pamoja na mambo mengine alisema kwamba:

“…Kristo hajatukomboa kwa kutupatia uzima wake kama fidia kwa ajili ya dhambi zetu, ili kwamba apate kutuachilia. Ikiwa tutazikubali asili au (chanzo) ambacho Kristo kikweli amenunua……wokovu wetu kwa damu yake …….. naye alimlipa Baba. Hivyo mtindo huu kabla ya yote unamwonyesha Mungu ambaye ni Baba kana kwamba yeye ni mwenye kulipiza mambo na ni mwenye kiu ya damu na kwa ujumla asiye patana na msamaha utolewao na Biblia.”

“Msamaha……. ni kiburudisho cha madai ya haki…….itakuwa ni vigumu kwa Mungu kuwa nayo kama mtunzi wa nyimbo anavyoiweka, “alilipa deni langu na akanisamehe dhambi zangu zote”

“Manukato ya toleo la Kristo yaliendelea katika utii wake kwa sheria za kimwili kwa niaba ya mwenye dhambi. Kristo katika maisha yake alitii sheria za mwili kwa ajili yetu na hayo ndiyo kwa uhalisi ni manukato ya toleo.”

Ijapo kuwa mwandishi huyo haelezei kwa uwazi sana kutokana na mpangilio huu, lakini bado hajayakana mawazo kama hayo, na wengine wanaamini kwamba yale aliyo yaandika tangu hapo pia yamejaa mawazo yenye kukaririwa. ( Kuyatambua mambo ya hapo juu, pamoja na taarifa nyinginezo juu ya mwandishi huyo aitwaye Ottis na mafundisho yake, hali kadhalika na mkanda wa video nilioutaja hapa kwenye makala hii angalia http://www.Bibleguide.com. Makala inayoitwa “George Ottis na mafundisho yake ya udanganyifu yaliyotayarishwa na Profesa J.S Malan – yote katika lugha ya Kiingereza.) Shirika lile ambalo linaongozwa na Ottis ndilo lililo husika na utayarishaji wa mkanda huo wa uongo wa video. Kwa sasa wameutayarisha mkanda wa pili wa video – ambao niliutaja mwanzoni – ambao unakusudia kuonyesha kwamba jumuia fulani fulani zimebadilishwa kupitia mafundisho haya ya roho za kimaeneo. Ottis pia anaheshimika kama mwanzilishi wa mawazo ya “ramani ya kiroho” ambayo nayo tutalitazama tutakapokuwa tukifikiria Ezekiel sura ya 4. Kama nilivyokwisha kusema, msingi wa kweli kuhusiana na maisha ya dhambi ya mwanadamu na hitaji lake la toba, pamoja na tabia na kusudi la kifo cha Yesu pale msalabani – inaonekana ilikuwa ni jambo lenye kutia giza (lisilo eleweka) kama si kupingwa kwa moja kwa moja na mafundisho haya ya kisasa! Ninatumaini kwamba unaweza ukajionea mwenyewe kutokana na maelezo ya hapo juu, kuwa hayawakilishi mambo mawili yote kwa pamoja, yaani ni mashambulizi juu yake na kuukana wokovu ambao Kristo amenunua kwa mapenzi ya damu yake. Ni kuyakana maisha ya dhambi ya mwanadamu ambayo ndiyo yanayomtenganisha na Mungu na pia ni kukana hitaji na tabia juu ya wokovu wetu wa ajabu kutokana na dhambi pamoja na milki yake.

Ni Injili Nyingine!

Hili sasa linatupeleka kwenye msingi wa pili wa makosa ya mafundisho haya, ambayo pengine ni ya hatari zaidi kuliko jambo lingine lolote lile kwa namna inavyodhalilisha na kushambulia moyo halisi wa Injili. Mafundisho hayo yanaonyesha kiini cha matatizo kisiwe ni dhambi, ugumu na kutokuamini kwa moyo wangu, bali uonekane kwamba ni majeshi ya uovu ya kiroho ndiyo yanayonizuia mimi kushindwa kumkubali Mungu. Wanasema kwa ujumla sio mimi mwenyewe wala sio hali ya moyo wangu ambayo ndiyo tatizo, isipokuwa ni roho chafu ndizo zinazonizuia nisimjue Mungu na kufungika katika giza. Chini ya mafundisho hayo, wenye dhambi sasa wamekuwa ni (wajinga) nao wamewekwa kuwa ni shabaha ya roho za uovu na kwamba inaelezwa kuwa, sio hali ya mioyo yao ambayo ndiyo tatizo, isipokuwa ni hizo roho za kimaeneo ambazo ndizo zinazowazuia wenye dhambi kushindwa kuitikia! Wazidi kudai kuwa kwa sasa haiwi tena ni dhambi za mtu binafsi kuwa ndiyo tatizo, isipokuwa sasa tatizo ni dhambi za jumuia, au miji, ambazo ndizo zinazohusika na roho hizi za kitaifa! Kwa sababu wao huyaamini mambo hayo, pia kuyafundisha kuwa njia kuu ya kuleta wokovu kwa watu sio kuihubiri Injili, isipokuwa ni kwanza kuzifunga roho za kimaeneo! Mahubiri ya Injili yanachukua nafasi ya pili na bado yanaweza tu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi pale tu ambapo roho za uovu zitakuwa zimefungwa kwanza! Kwa hakika mafundisho ya jinsi hii yanawakilisha Injili nyingine – ni mashambulio kwenye ile sababu ya kimsingi na halisi juu ya kwa nini Yesu alikufa msalabani! Ni kukana mafundisho ya Yesu mwenyewe kuhusiana na mtu, kuhusiana na dhambi, kuhusiana na shetani, na kuhusiana na hukumu.

Mwandishi mmoja anatuambia kuhusu kiongozi mmoja maarufu wa kanisa huko Amerika ya kusini ambaye kwa kawaida huomba yeye mwenyewe kwa muda wa wiki moja kabla hajaanza kampeni zake. Anafanya hivyo ili aweze kuzitambua na kuzifunga mamlaka ya nguvu za giza juu ya mji huo ambao amekuja kuuhudumu. Mpaka “anapojisikia” kuwa amelipata lengo lake, ndipo anapoanza kuhutubia katika mikutano ya hadhara akiwaelezea watu kuwa “sasa” wako huru kumjia Kristo! Watu hawa wanajiinua wenyewe pamoja na mafundisho yao, wanajiinua juu zaidi ya Kristo pamoja na mitume ambao hawakuwahi kufanya madai ya jinsi hiyo kwa watu waliowajia. Kristo pamoja na mitume walikuja wakihubiri habari njema na wakiwasihi waume kwa wanawake watubu! Kwa maneno mengine, watu hao wanafundisha kuwa tatizo halisi sio ugumu wa moyo wangu mwenyewe wala sio dhambi, isipokuwa ni hizi roho za kimaeneo ambazo zinatakiwa kutambuliwa na kufungwa! Sio kupinga kwa moyo wangu kuwa ndilo tatizo, isipokuwa kupinga kuwa roho za kimaeneo ndicho kinachoniweka nje ya ufalme wa Mungu. Wanataka tuelewe kuwa ni roho za kimaeneo sasa ndizo zenye kuhusika na kiburi, tamaa mbaya na ugumu wa moyo wangu – kadhalika na kutokuamini kwangu?- na sio mimi mwenyewe. Mara tu mtu akizifunga roho za kimaeneo katika jamii basi, wenye dhambi wanakuwa wamewekwa “huru” kumjua Kristo! Mwinjilisti mwingine hawezi kuhubiri katika mji mpaka pale watakapojisikia kuwa wamezishinda katika maombi hizi roho za kimaeneo ambazo zinaushikilia mji huo kwa nguvu zao, na mmoja wa viongozi maarufu wa kanisa ambaye amehamasisha makosa hayo anatangaza kuwa: “ninafahamu vizuri pasipo shaka yoyote ndani yake, kuwa mahubiri makubwa hayawezi kuzisababisha roho za watu kuokoka na kanisa kukua … Hapana, isipokuwa ni pale utakapozishusha chini ( kuziangusha ) nguvu za giza zililzokuwa zinawazuia watu kumwishia Mungu katika maisha yao; hiyo ndiyo itakayosababisha kanisa kukua“. (Makala ya Larry Lea katika kitabu cha “Roho za Kimaeneo.” – Territorial Spirits” – Kilichoandikwa na Wagner, ukurasa wa 91 kilichokubaliwa na “Karisma na Maisha ya Kikristo” ã 1989, Strang Communication Company.)

Je watu hawa hawadhihaki kwa kumpinga Kristo mwenyewe? Mwandishi wa hapo juu anasema kuwa ana uhakika mkamilifu kwamba – hata mahubiri makubwa, hayawezi kuokoa roho za watu au kulijenga kanisa! Lakini tazama mwana wa Mungu aliwaambia wanafunzi wake, “Nendeni katika ulimwenguni kote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Yeye aaminiye na kubatizwa ataokoka”. Mk 16: 15,16. Mtume Paulo naye anaurudia usemi huo huo, “siionei haya Injili ya Kristo kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye.” Rumi 1:16. Pia katika 1Kor.1:17,18,21 kwa kuwa Kristo hakunituma ili kubatiza isipokuwa kuihubiri Injili … kwa sababu neno la msalaba …. ni nguvu ya Mungu iletayo wokovu …. Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa”. Maandiko mengineyo mengi yangeweza kunukuliwa ili kuthibitisha tangazo lake Mungu litolewalo kwa ajili ya wokovu wa hao waliopotea na kulijenga kanisa lake, lakini sasa hawa waandishi wa kisasa wanapinga moja kwa moja ukweli huu kwa hiyo imani yao. Kristo hakuwaagiza wanafunzi wake, “kwenda kuzitambua na kuzifunga roho za kimaeneo ambazo zinawazuia watu washindwe kuokoka!”

Ijapokuwa waandishi hawa wanaamini kuwa kuhubiri Injili ni njia ya kuokoa roho za watu, bado wao huanza kwa kuzifunga roho za kimaeneo kana kwamba hilo ndiyo tendo la mwanzo na lenye msingi katika kanisa. Na kule kuihubiri Injili sasa hushika nafasi ya pili katika mipango yao – na bado Injili hiyo inategemea kikamilifu mtindo huo wao wa kuomba dhidi ya roho za kimaeneo. Hili ni tatizo kubwa la kasoro na ni sawa na kusema kuwa, “Sawa, ni kupitia Yesu kristo mtu anaweza kuokolewa, lakini unahitaji kutahiriwa kwanza”. Ukumbuke kuwa katika makanisa ya Galatia waliamini mambo mengi yaliyo mazuri na yenye haki kuhusu Kristo, na msamaha pamoja na wokovu ambao tunapata kwa yeye. Lakini wao waliongezea mafundisho yasiyo ya kiinjili, ambayo yalidhalilisha na kutishia uwepo wa imani yote! Mtume Paulo amesema “wamelogwa” kwa mafundisho ya aina hiyo. Na ijapokuwa wahubiri hawa wa kisasa ambao wanafundisha mapambano dhidi ya roho za kimaeneo, wanaweza pia wakaamini mambo mema na yenye haki vile vile, bila kujali kiasi gani wamejiingiza katika kujishughulisha na kazi “halisi” ya Mungu, hawajali kuwa mafundisho hayo yahusuyo roho za kimaeneo ni uchawi wenye hila ndani yake! Inayodhalilisha imani ya Injili.

Mafundisho haya hayaji kutoka kwa Yesu wala kutoka kwa mitume, au tusemeje sasa? Je Yesu alishindwa kuzitambua na kuzifunga roho zilizokuwa zinatawala Kapenaumu? Korazin na Bethsaida? Huko kulikuwa na mwitikio mdogo sana kufuatia mafundisho yake ijapokuwa amefanya kazi kwa nguvu kwao. Mat 11:20-24. Je tunaweza kulaumu upungufu wa mwitikio wa watu hawa katika miji hiyo kuwa unatokana na roho za kimaeneo, au kutokana na kushindwa kuyatambua majina ya roho hizo za kimaeneo? Au je, roho hizo za kimaeneo zilikuwa na mamlaka ya “kuzuia” huduma ya Yesu kwa sababu alikuwa bado hajafa pale msalabani (Kalvari)? Hapana! Hakuna lolote kati ya mawazo hayo ambalo lina ukweli wowote. Yesu alisema kwamba, ikiwa kazi alizozifanya katika miji hiyo zingefanyika huko Tarso na Sidon, wangekwisha kutubu siku nyingi iliyopita na hata Sodoma ingesalia hadi leo. Yesu anawakaripia watu wa miji hiyo ya Israel kwa sababu ya kukataa kwao kutubu. Anawakaripia kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kulingana na yote aliyoyasema na kuyafanya bado hawakuweza kuzioacha dhambi zao. Walikataa kumwamini na kumruhusu Yesu ayabadili maisha yao. Hiyo ilikuwa ni ugumu wa mioyo yao wenyewe na kutokuamini ndiyo iliyosababisha upungufu wa mwitikio, na ilikuwa ni kutokana na hilo ndio maana Yesu alitangaza hukumu kali juu yao. Walipaswa kujilaumu wao wenyewe na sio shetani wala sio roho za kimaeneo! Ikiwa tutafuata maelezo basi haya ndiyo mafundisho halisi ya maandiko ya neno la Mungu. Katika matendo ya mitume hatumsomi mtume Paulo akijifungia ndani mwenyewe kwa siku nyingi ili kujishughulisha na mapambano ya moja kwa moja na roho chafu, kabla hajahubiri katika mji – kana kwamba hiyo ilikuwa mbinu ya lazima! Hapana. Tunajua kuwa yeye alikuwa ni mtu wa maombi, lakini alipowasili katika miji na jiji, kwa kawaida anasema habari zake kwamba alikuwa akienda moja kwa moja kwenye masinagogi, au sehemu za masoko kumhubiri Yesu Kristo kwa watu. Na pale wayahudi walipoupinga ukweli wa Injili, Mtume Paulo analaumu juu ya mioyo yao. Mtd 13: 45,46.

Mtume Paulo alipokuwa huko Athene na alipoona mji mzima umekabidhiwa kwa masanamu kwa mara nyingine yeye hakujiingiza katika “ulimwengu wa kiroho” ili kuzifunga roho za ibada za masanamu. Hapana, bali yeye alienda katika masinagogi na sehemu za sokoni kumhubiri Kristo na ufufuo! Mtd 17:16-19. Sio wengi waliookolewa kule Athene. Na baada ya kuondoka hapo alielekea kwenye mji wa Korintho. Baadaye alipokuwa akiwaandikia Wakorintho, aliwaambia kuwa, alifika kwao baada ya kuondoka kule Athene akidhamiria asikijue kitu kingine chochote isipokuwa “Yesu Kristo aliyerubiwa”, 1Kor.2:2. Pengine kudhamiria huku kwake kuliweza kuimarishwa ndani yake alipoona uhafifu wa busara ya kibinadamu ambayo iliwashika watu wengi wa Athene, ambayo ndiyo iliyowafanya washindwe kuupokea ukweli wa Mungu. Hata kama hiyo ni kweli au hapana, Paulo mwenyewe analifafanua kwa ajili yetu, kwa nini iko hivyo kwamba watu hawapokei kweli ya injili.

“Kwa kuwa Wayahudi wanahitaji kuona ishara, Wayunani wanatafuta hekima, lakini tunamhubiri Kristo aliye sulubiwa, ambaye kwa wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuuzi.”

Anaendelea kueleza kuwa sio watu wengi wenye hekima na wenye nguvu walioitwa; 1Kor.1:22-29. Anafafanua hivyo kwa makini kuwa ni hekima za kibinadamu au tungeweza kusema ni kiburi ndicho kinachowazuia watu kuupokea ukweli wa Mungu – na sio roho za kimaeneo! Inashangaza kuona Biblia yenyewe inavyofafanua vizuri mambo yake. Wayahudi wanatafuta kuona aina fulani za ishara au miujiza na Wayunani wanatukuza hekima zao wenyewe – watu wenye vitabia vya jinsi hiyo hawako tayari kulipokea neno la Mungu kwa moyo wa unyenyekevu bali hujiinua wao wenyewe kinyume na kweli ya Mungu.

Katika mwangaza wa ukweli huu, sasa tunaweza kuona ni kwa nini watu wengi hawakuweza kuitikia kule Athene. Katika ule mstari wa 18 mtume Paulo anatangaza, “kwa kuwa mahubiri ya msalaba kwa wao waangamiao ni upumbavu bali kwetu sisi tuokolewao ni uweza wa Mungu.” Katika ile 2Kor 4:3,4 anapanua wazo hili kidogo; anasema Injili imefichwa kwao waliopotea, na anaendelea kuelezea “ambamo ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini isiwazukie nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.”

Katika sura hiyo anasimulia kwamba shetani anao uwanja wa matendo yake maovu kwa sababu ya kutokuamini au ugumu wa mioyo ya watu; ni ule ugumu wa mioyo ya watu wenyewe ambayo humpatia shetani fursa ya kuwadanganya na kuwafanya wawe mateka wa dhambi. Hapa mtume Paulo anaelezea hali ya kiroho ya hao wanaoipinga Injili; sura hii haiwakilishi mbinu kwa ajili ya “vita za kiroho”. Mtume Paulo hatuambii hapa kwamba tunapaswa kumfunga mungu wa ulimwengu huu kupitia maombi ya maombezi ili kwamba hao watu (wajinga?) waweze “kuwekwa huru” ili waweze kuamini Injili. Ijapo kuwa katika kukubaliana na hilo, maneno ya Yesu mwenyewe alipokuwa akiongelea kuhusu “saa yake” ambayo inamaanisha kifo chake pale msalabani. Katika Yoh 12:31 anasema: “Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”

Ukweli huu unarudiwa tena pale Yesu anapoongea kuhusu kuja kwa Roho Mtakatifu. Yesu anasema kwamba, Roho Mtakatifu atawahukumu wanadamu kwa hukumu kwa sababu “…yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa”, Yoh16:11. Bwana Yesu anaungana moja kwa moja na hukumu ya mfalme wa ulimwengu huu ambayo alikuwa anaenda kuitimiza pale Kalvari, pamoja na hukumu ya ulimwengu, ambayo ni hukumu ya ulimwengu huu ina maana kwamba ni ya watu waishio ndani yake. Akizichukua dhambi za ulimwengu pale msalabani Yesu angekinyang’anya kifo ule uwezo wake uliokuwa nao, (“uchungu wa mauti ni dhambi” 1Kor.15:56; Tim.1:10). Na atambatilisha yeye aliyekuwa na uwezo wa mauti, yaani huyo shetani, Heb. 2:14. Kila amwaminiye Yesu Kristo – kwake huyo mauti pamoja na shetani wamekwishapoteza haki yao na mamlaka juu yao. Kwa sababu mwanakondoo wa Mungu amezichukua dhambi zao – dhambi zao zote – na hivyo akanyang’anya toka kwa mauti na shetani ile haki yote waliyokuwa nayo juu yao. Zaidi ya hayo, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya wanadamu wote, anayo haki juu ya wote na kwa hiyo anawaagiza watu wote mahala pote kutubu (Mtd 17:30, tupo kule Athene Tena!). Tanga mwanzo mwa huduma yake na katika kuhubiri Injili, Kristo alikuwa akiwasihi watu kutubu, na mitume waliendeleza ujumbe huo huo Mk 1: 14-15; Mtd 2:38. Je, hawa waandishi wa kisasa wanasema kwamba wanaume na wanawake hawawezi kutubu mpaka kwanza roho zile za kienyeji katika taifa ziwe zimefungwa? Je hiyo ndiyo sababu iliyowafanya watu wa Kapenaum washindwe kutubu kwa sababu Kristo ameshindwa kuzifunga roho hizo juu ya Kapenaumu? Mafundisho haya hayaleti maana yoyote ile katika Agano Jipya! Yesu Kristo alizivunja mamlaka na uwezo pale msalabani kwa sababu alibakia pasipo dhambi, na bado akazibeba dhambi za ulimwengu wote na ufufuo wake ni muhuri kamili wa wokovu wetu, 1Kor.15:12–22. Akiwa amemnyang’anya shetani ule uwezo wake, Kristo sasa anaweza kupanua kwa neema ya Mungu ule uwezo wa uzima wake yeye mwenyewe akawapa hao wamwaminio. Akiwa amewasafisha kutokana na dhambi. Yesu pia anavunja ile milki ya dhambi katika maisha yetu kwa uwezo wa ufufuo wa uzima wake ndani yetu.

“Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo” kwa sababu shetani pamoja na uwezo wake wamehukumiwa na amezitangua pale msalabani. Kwa maneno mengine, huwezi kumlaumu shetani – hakuna popote inapohesabu hivyo! Sawa ni hakika kuwa shetani anawaweka watu katika giza, dhambi na vifungo – hiyo ina maana wale watu ambao hawaamini. Na yeye huja kunyang’anya, kuiba na kuharibu maisha ya watu. Lakini sasa, kwa sababu ya Kalvari huwezi tena kusema kuwa, njia ya kumwendea Yesu imefungwa kwa watu mpaka kwanza zile roho za kimaeneo zizuiazo ziwe zimefungwa! Jambo kama hili linabatilisha tu yale yote ambayo Kristo alilkuja kuyafilia. Hapana, wajibu unaangukia juu yako wewe na mimi kuiamini injili. Kama hatuamini Injili, basi kwa vyovyote vile tutakuwa tunampatia shetani pamoja na dhambi ile fursa na uwanja wa kufanya kazi ndani ya maisha yetu. Na katika hali yoyote ile bado shetani ni jeshi la uovu lenye nguvu katika ulimwengu, sawa sawa kama vile maandiko yanavyotangaza. Lakini maandiko yanatangaza kwa sauti na kwa ufasaha kwamba Yesu Kristo amezishinda dhambi, shetani pamoja na mauti, na akiwataka waume kwa wanawake watoroke wakawe huru kutokana na toleo la wokovu katika yeye ambalo linawakilishwa kupitia Injili.

Kwa sababu ya mambo haya pia, Yesu alisema kuwa na hii ndiyo kazi ya Mungu, “…. kwamba umwamini yeye aliyetumwa”, Yoh 6:29. Na kwa sababu gani roho mtakatifu atawahukumu wanadamu kwa dhambi? Yesu anasema kuwa ni kwa sababu, hawamwamini yeye. Yoh 6:9.

Na hii ndiyo dhambi ambayo wanaume na wanawake watahukumiwa kwayo. Dhambi zinginezo Yesu anaweza kutuweka huru kwa sababu kutokana na kile alicho kikamilisha pale Kalvari. Lakini njia pekee ya kuupokea wokovu huu ni kwa kumwamini yeye; na kama hatutamwamini yeye, basi tutakuwa tumepotea. Mtume Paulo anahitimisha kwa jinsi ya ajabu kwa ajili yetu pale katika Efeso 2:8. “kwa kuwa mliokolewa kwa neema katika imani na hii sio kwa uwezo wenu, bali ni kwa karama ya Mungu“. Na hawa Waefeso walikuwa ni watu wa aina gani? Haya, Mtume Paulo anatujulisha katika ule mstari wa 1-3 wa sura hii – kuwa walikuwa wafu kwa sababu ya makosa ya dhambi zao; waliishi kwa kuzifuata kawaida ya ulimwengu huu na mfalme wa uweza wa aga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi! Na wakawa kama wengine walivyo, watoto wa hasira. Kwa hiyo hapa tunawaona watu ambao wanatenda dhambi kisha wanajiridhia wenyewe, chini ya usimamizi wa shetani na vishawishi vyake kwa sababu ya kutokutii kwao; na kwa hiyo wapo chini ya hukumu ya Mungu. Na tunaambiwa wazi kwamba hiyo ndiyo hali ya wale wote ambao hawataki kuamini. Lakini mambo yalibadilikaje kwa hawa Waefeso? Haya mtu yule aitwaye Paulo, alitumiwa pia huko kwa Wamataifa ili apate “kuwafungua macho yao” na kuwarejesha kutoka katika nguvu za giza na kuwaingiza katika nuru; na kutoka katika nguvu za shetani waingie katika nguvu za Mungu, ili kwamba wapate kupokea msamaha wa dhambi, Mtd 26:18. Hii ilikuwa ni sehemu ya huduma ambayo Mungu ambaye aliyashinda mamlaka na uwezo kupitia Kristo pale Kalvari – alimpatia Paul. Mtume Paulo hakuhitaji kujitahidi au kupigana katika kupata huduma na mamlaka kwa kuzifunga roho za kimaeneo! Hapana, Paulo alikuwa kati ya Wayahudi kwa muda mrefu wa miezi mitatu kwanza kule Athene halafu akawa kwa wamataifa kwa muda wa miaka miwili, akiwa anazungumza, anajadiliana, akichunguza na kuhubiri – na watu wengi walimgeukia Bwana! Na hawa waefeso walipataje kuokolewa? Haya mtume Paulo anatuelezea katika ile sura ya kwanza mstari wa 13. Walimtegemea Kristo baada ya kusikia lile neno la kweli, injili ya wokovu wao! Ilikuwa ni kupitia Mtume Paulo aliyeihubiri Injili ya Kristo kwao na wao wakaiamini Injili, hilo ndilo lilliowasababishia kumgeukia Mungu wakiondokana na nguvu za shetani! Mungu asifiwe!

Kristo alipoenda kwenye nchi yake mwenyewe, Mk 6:1-6, hakuweza kufanya kazi zenye nguvu kwenye eneo hilo mbali ya uponyaji alioufanya kwa watu wachache. Je hii ni kwa sababu roho ya kieneo hiyo ilikuwa ni nguvu sana? Hapana! Biblia inatupatia sababu – inasema Yesu alishangazwa na kutokuamini kwao. Hakushangazwa na nguvu za baadhi ya roho za kimaeneo, isipokuwa yeye alishangazwa na ugumu wa mioyo yao na kutokuamini kwa watu hapo. Mty 13:58 anatuambia kwamba, ” … wala hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao“. Ni ile imani katika Kristo ndiyo iletayo wokovu na sio kule kuzifunga roho ya kitaifa; na imani inakuja kwa kusikia neno la Mungu – Rumi 10:17! Hivyo Yesu Kristo anatueleza katika Yohana 3:18,19:

“Amwaminiye yeye hahukumiwi, bali yeye asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Bwana pekee ya Mungu. Na hii ndiyo hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni na watu wakapenda giza kuliko nuru, kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.”

Sawasawa na mafundisho ya Yesu, watu wale ambao wanakataa wasimjie na kumwamini, wanafanya hivyo si kwa sababu wanazuiwa na roho za kimaeneo, bali kwa sababu walipenda matendo maovu yao. Mafundisho haya ya kisasa kwa ujumla yanasababisha kuchanganyikiwa na inaleta dhihaka kwa mafundisho ya biblia. Yanafanya maroho ya kimaeneo yaonekana ndiyo yanayohusika na uovu wa watu pamoja na kutokuamini. Wanataka tuelewe kuwa, iwapo tutafanikiwa kuzifunga hizi roho za kimaeneo ndipo watu watakuwa huru kuitikia Injili. Na hivyo makanisa yetu yataongezeka kwa kiwango kikubwa ambacho hujawahi kukiona kabla. Hii kimsingi inachafua mafundisho ya Kristo na ya Mitume. Hawa walimu wa kisasa wanasema kuwa ikiwa mji umeshikiliwa na matabia ya uchoyo, kiburi, ulevi na au tamaa mbaya basi hiyo ni roho ya kieneo ya uchoyo, kiburi, ulevi au tamaa mbaya ambayo inatawala juu ya mji huo na hiyo inahitajika kufungwa katika maombezi ya maombi. Hakuna lolote kama hilo ndani ya biblia. Eti nini? Kukemea roho za kimaeneo au tamaa mbaya na kisha watu wa mji huo wataachiliwa huru kutokana na dhambi hizo? Eti nini? Kwamba tatizo halisi sio mioyo ya watu bali ni uwezo wa roho za kimaeneo? Haya si mafundisho ya kibiblia. Biblia inatambua tatizo halisi kuwa ni moyo wa mwanadamu mwenyewe – au ndani ya moyo wa mwanadamu mwenyewe ndiko liliko tatizo. Tatizo sio kuwa tunatawaliwa na roho za kimaeneo za nje yetu – hapana – bali tatizo halisi ni dhambi iliyomo ndani ya moyo wangu mwenyewe na kule kujipenda. Tatizo halisi ni ugumu wa moyo wangu mimi mwenyewe. Hawa walimu wa kisasa wanafikiri kuwa iwapo utafunga “roho ya ulevi” katika eneo au jumuia ndipo nguvu ya kupendelea ulevi itavunjwa katika jumuia na kuwawezesha watu wote kuwa huru kutokana na ulevi. Huwezi kuifukuzilia mbali roho ya “ulevi” kutoka kwenye eneo kana kwamba hiyo ndiyo inayowashikilia watu katika dhambi hiyo! Watu hawa wanafikiri nini? Wanajaribu kulihamisha lengo la Injili lisieleweke kwa jamii; na lengo la Mungu kwa ulimwengu mzima pale wanapopotosha ukweli wa Injili. Wanajaribu kung’oa mwelekeo wa Mungu kwa wanadamu, kwa kuichepusha ile kweli. Lakini sasa unaweza ukaihubiri Injili kwa watu wote na ikiwa kwa neema ya Mungu watu binafsi wataitikia na kuokoka. Ndipo bila shaka utaweza kuona kupungua kukubwa kama sio kutoweka kabisa kwa ubaya wa aina fulani kama matokeo ya watu wakigeuka kutoka katika dhambi wakimgeukia Mungu! Mtd 19:19, 23-27. Huko Efeso watu wengi walichoma moto vitabu vyao vya uchawi na kuabudu sanamu ya Diana yalitoweka kimchezo tu – lakini hiyo ilitokea kama matokeo ya watu wengi kugeuka kutoka katika dhambi zao kupitia mahubiri ya mtume Paulo (mstari wa 26)! Katika Biblia nzima neno la Mungu huja moja kwa moja kwenye mioyo ya watu wa kuliona tatizo halisi pamoja na kupinga limelala hapo, yaani ndani ya mioyo ya watu. Tunaweza kutaja Yeremia 4:1-4 na Lk.13:34,35, pamoja ni mifano miwili kati ya mingi iliyomo katika Biblia.

Ijapokukwa watu wa Mungu walipaswa kumuombea, lakini hakuna chochote kile cha kuzifunga roho za kijiografia kana kwamba hizo zinawakilisha jeshi linalowaweka watu katika vifungo na kuwakataza wasimpokee Mungu.

Hii tena ni msingi mwingine wa kasoro za mafundisho haya ya kisasa – ni hatari izidiyo. Tatizo la wema na ubaya linaonekana kama ni jitihada kati ya mambo mawili ya ulimwengu mzima au nguvu za roho zinazopingana; na hazionekani kama zinahusika na chaguo ambalo mtu anaweza kulifanya kama yale yaliyoumbwa kwa mfano wa Mungu! Inaonekana kana kwamba wenye dhambi wenyewe sio tatizo halisi na hawafikiriwi kuwa wao wanabeba sehemu muhimu katika kuokoka kwao. Hapo inaonesha kwamba mapambano hayamo ndani yao au kwa ajili ya mioyo yao, bali ni sehemu fulani huko “angani”. Haionyeshi pia kuwa ni dhambi zangu binafsi na kule kutokuamini kwangu, hilo ndilo tatizo, bali inaonekana kama ninashikwa juu kwenye mashindano ya majeshi ya kiroho. Na mimi nipo pale katikati, karibu sawa na mlengwa mjinga. Ninahitaji tu nguvu za roho zilizo kubwa zaidi ili kuzidisha nguvu za roho ndogo ndogo kunifanya niwe huru! Ni huzuni ya jinsi gani hiyo; kuchanganya mafundisho kwa udanganyifu kwa jinsi gani huko? Injili ya Kristo ni uweza wa Mungu kwa kila aaminiye. Wokovu wa roho za watu hautegemei kule kuzishinda roho za kimaeneo! Lakini hawa walimu wa kisasa, sasa wamebuni Injili mpya ya ukombozi kupitia vita vya kiroho!

Kama nilivyokwisha kusema katika zile makala zangu mbili, na bado nazidi kukazia tena kuwa mafundisho hayo ni ya kimwili yanakazania kwenye mambo ya nje na siyo mambo ya kweli ya ndani. Wanamfananisha shetani kama anayetaka kuichukua nchi anayofikiri kuwa kama yake. Na wao wamesema kuwa hiyo ndiyo nchi ya kijiografia! Shetani ni mungu wa dunia hii maadam hii ndiyo mazingira ya kazi yake. Lakini kwa vyovyote vile viwavyo, iwe ni roho za kimalaika, mamlaka za uweza uwao wowote, bado maandiko yanaiweka wazi kwamba uwanja ambao ibilisi anapenda kuumiliki ni mioyo yetu, akili na nafsi zetu! Mapepo hawahamii kwenye “vumbi” kavu, bali wao wanapenda kupata makazi ndani ya binadamu Mty 12:43-45. Hawapati pumziko kwenye maeneo makavu, isipokuwa wanapenda kuishi ndani ya watu. Na hii ndiyo “nchi” ambayo Yesu aliifilia na akamwaga damu yake ili kutafuta nafasi ya kukaa yeye pamoja na Baba! Yoh 14:18-23. Tunatakiwa tuwe makazi ya Mungu kwa Roho, Efe 2: 22. Kwa kupitia kuiamini Injili ya Kristo sisi tumesamehewa na tumeingizwa ndani ya Ufalme wa Mungu kwa uzao mpya! Bali Shetani anataka kutufanya sisi tuwe ni makazi ya roho zake, sio kupitia nguvu za ziada za roho ya kitaifa, isipokuwa kwa kututaka sisi tuamini uongo wake ambao anaupendekeza kwetu kwa kutujaribu ili tusimwamini Mungu na kisha tujipendeze wenyewe. Huo ndio uwanja wa mapambano. Na katika huo uwanja wa mapambano mioyo yetu pamoja na dhamira zetu, Mungu alionyesha pendo lake mwenyewe kwetu sisi kwa kumtuma mwanae pekee afe kwa ajili yetu na kututaka tugeuke mbali na matendo maovu na tuupokee wokovu wake wa bure. Hiki ni kipawa cha Mungu!

Lakini madanganyo ya mafundisho hayo yanazidi kutumbukia ndani zaidi. Baada ya kuwa wameamini kuwa wamekwisha kuzifunga roho za kimaeneo zitawalazo juu ya mji, wengine wao wanawachagua “walinzi wa milangoni.” Eti hao ni watu ambao wanapaswa kuomba ili kuzuia roho za uovu zisiweze kuingia katika miji – hatimaye, watu hao watasimama pia kwa mbinu fulani ndani na karibu na mji – kwenye barabara kuu ndani na nje ya mji na kuendelea! Kwa kufanya hivyo, wanazihesabia roho za mikoa yaani wanazipatia uwezo wa kutawala jumuia yote kana kwamba watu hawana chaguo lao katika mambo – na kwa kiasi kwamba Injili ya Kristo haiwezi kuwafikia kwa ufasaha na kuwaokoa! Hivyo siyo Injili ya Kristo – wanacheza michezo ya ulozi pasipo kutambua! Kwa hivyo, wao kwa vyovyote wanaamini kwamba ikiwa utaweza kuzifunga roho hizo, basi roho ya Mungu itatawala juu ya mkoa, basi hapo sasa watu wapo huru kuitikia Injili na kisha Wakristo wanaweza kuanzisha utawala wa Mungu katika taratibu za jamii ya kienyeji – kwenye mifumo mbali mbali ya serikali na jamii katika mji! Hii inaonekana kama uanzishaji wa ufalme wa Mungu hapa dunianli na “kurejesha” nchi kutoka katika mikono ya shetani. Hawa waombezi wapya wanachokifanya hapo wanapigana ili kupata ardhi, vumbi na dunia ambayo ndiyo wanayoisemea kuwa inapaswa kurejeshwa kutoka katika mikono ya shetani. Baadhi ya hao waandishi wanayo mafundisho mengine yanaweka kwa urahisi yanaeleza kwamba, kwa sababu ya dhambi zake katika bustani ya Adeni – Adamu alipoteza milki ya mipaka ya nchi kwa shetani kwa kufanya hivyo, wanazipatia haki roho za mikoa yaani wanazipatia uwezo kutawala sio tu nchi bali pamoja na watu wanaoishi katika nchi hiyo. Wanasema kuwa Yesu alikufa pale msalabani ili kurejesha milki juu ya vumbi hili na dunia – pamoja na mipaka ya kijiografia. Lakini tunaelezwa zaidi na hawa waandishi wa kisasa kwamba, pale msalabani hapakuharibu mamlaka zote pamoja na uweza wake. Hapana, tunatakiwa kutumia uwezo ambao Bwana ametupatia sasa, ili kuzifunga roho hizi chafu zitawalazo juu ya mkoa na kisha watu wa mkoa ule watakuwa huru kuupokea utawala wa Mungu! Hiyo ni injili yao ya kimwili. Kulingana na mafundisho hayo, pambano la msingi sio kwa ajili ya nafsi za watu (wauume kwa wake) isipokuwa ni mavumbi – yaani, sehemu ya kiografia! Na mara tu tunapokuwa tumezifunga roho hizo zinazotawala juu ya kipande hicho cha vumbi na ardhi, kwa watu wanaotembea au kuishi juu ya kipande hicho cha vumbi au ardhi, watakuwa huru kuipokea Injili na kuingia katika ufalme wa Mungu. Mafundisho haya ya kimwili yote yanawafunika macho watu wasiijue kweli ya maandiko, ihusuyo asili ya dhambi, wokovu na ufalme wa Mungu.

Hebu niseme hapa, kwamba, ninafikiri sote tunajua kwamba eneo fulani fulani au jumuia inaweza ikaingiwa na tabia fulani ya dhambi maalumu inayoonekana kumiliki eneo hilo. Na kwa vyovyote vile, mtu yeyote anayezaliwa katika mazingira ya aina hii, anaweza akashawishika. Na desturi hii ya dhambi katika jumuia, na desturi hii ya dhambi bila mashaka yoyote yale, inakuzwa na Ibilisi na anaweza kuwatumia kuchanganya upinzani wa Injili ndani ya wale wasioamini, Mtd.19:23-28. Lakini hali hii ndivyo haswa iliovyokuwa katika jumuia nyingi na miji ambayo mtume Paulo alitembmelea. Kulikuwepo na zinaa inayoendelea katika miji mingi. Dini za Ulozi na Uchawi zilishikilia jumuia fulani fulani. Kulikuwepo na uchoyo, kiburi, na uchafu. Koritho ilikuwa ni sehemu iliyozoelea mambo ya aina hiyo. Lakini sasa kupambana na roho za kimaeneo ili kuwaweka huru watu kutokana na tabia zao za uzinzi, mambo ya kimwili au uchawi, jambo hili hamna msingi wowote ule wa Kibiblia.

Kwa hakika, mtume Paulo anachagua maneno kwa makini pale anapoyaulizia makanisa ya kule Galatia – “Ni nani aliyewaloga? Mafundisho hayo yanafanana kama ulozi na kadiri mtu anavyoendelea kujifunza mafundisho haya ya kisasa ndivyo mtu anavyoona kwa urahisi kuwa yanafanana na kile ambacho mtu anaweza akafikiria kuwa ni mafundisho na mtindo wa ulozi au wa Uaguzi. Kadiri mafundisho haya yanavyozidi kuenea ulimwenguni kote, bila shaka yanaweza kutengeneza vijitabia vyake kutoka nchi fulani hadi nyingine kadiri watu walivyo na shauku ya mambo mapya; na katika njia tofauti. Kwa mfano; yapo magazeti ambayo yanawahamasisha na kuwasihi wakristo wote kuomba dhidi ya roho za kimaeneo juu ya baadhi ya miji na jiji fulani; magazeti hayo yanajishughulisha sana katika kutafutia aina fulani ya dhambi nyingi hasa Uchawi, ambao umefanywa katika nchi. Na kisha huyatangaza matokeo waliyoyapata ili kwamba wakristo waweze kuomba maalumu dhidi ya roho hizi za kimaeneo, ambazo zinafikiriwa kuhusika na matatizo ya dhambi hizi zote. Hata pia wanawasihi wakristo watembelee maeneo fulani fulani ya kijiografia katika jiji huku wakikemea roho chafu. Lakini vitabu vinavyoongoza ambavyo vimeandikwa kuhusu somo hili kwa ujumla haviwahamasishi wakristo kuingia katika “vita vya kiroho” dhidi ya roho za kimaeneo. Kinyume chake, wanaonya juu ya hayo na watuambia kuwa ni wakristo wale waliokomaa, “na wenye karama rasmi” na wale walioitwa ndio wanaopaswa kuingia katika mapambano hayo. Ijapokuwa bado wanasema kwamba vita hivyo ni vya lazima kwa ajili ya kuleta mafanikio ya uenezaji wa Injili. Zaidi ya hayo bado wanakubali kuwa jambo hili ni kujitumbukiza katika matatizo ya bure na yenye kuogofya na ni mapambano ya hatari yenye kuwapatia wengi misiba. Hayo yote ni sawa na kubatizwa katika mambo ya ushirikina na udanganyifu.

Vita vya Kiroho – ni Matendo yenye Hatari?

Lakini sasa kwa nini “vita hivyo” viwe ni mambo “yenye hatari”, kuogofya na kukuletea matatizo? Haya, wanasema kwamba wakristo “wa kawaida” huwa hawana mamlaka na nguvu zilizo katika kiwango cha “madaraka ya juu” ya roho za kimaeneo. Na wanazidi kutuambia kuwa kumewahi kutokea na itaendelea kuleta msiba katika “vita” hivyo! Waandishi hawa wanatuambia juu ya wachungaji ambao wameanguka katika dhambi “kwa sababu” ya kujiingiza kaika “mbinu ya kiwango cha mapambano ya kiroho” (strategic – level spiritual walfare)! Waandishi hawa wanatuelezea kuhusiana na kuvunjika kwa ndoa, magonjwa, mambo ya kimwili, watu wanajifanyia uvunjifu juu ya Imani zao na hata juu ya kifo – kwa sababu ya kujihusisha kwao katika aina hii ya vita! (Ikiwa ni kweli kuwa matatizo hayo yamewazukia kwa sababu ya watu wenyewe kujihusisha katika aina hii ya mapambano, basi litakuwa ni swali lingine lenye kuhojiana). Kumekuwepo na michanganyiko mingi pamoja na maumivu ya moyo kutokana na mafundisho haya kiasi kwamba kiongozi wa aina fulani ya huduma huko Amerika ameandika kitabu kuhusiana na jambo hili kiitwacho (Needless Casualties of War”; “Misiba isiyo ya Lazima katika Vita”, kilichoandikwa na John Paulo Jackson, Kingsway Publications. Copyright John Paul Jackson 1999). Yeye pia anapendelea mapambano dhidi ya maroho, lakini katika kitabu chake anaeleza jambo fulani zuri na anaonya kuhusu kutokuwa na kiasi, ambako analaumu kuwa ndiko kunako husika na majanga ya kutisha katika maisha ya wakristo. Lakini sasa kule kuamini kwao juu ya imani ya kufunga roho za kimaeneo, kinawafanya waandishi hawa wote wawe vipofu juu ya ukweli uliofunuliwa katika maandiko, nao huuacha ukweli huo kirahisi tu na hawaonyeshi kuhusika kihalisi kwa yale yanayofundishwa na Biblia ili wahalalishe makosa yao. Wanaeneza mafundisho yenye kasoro, na watu wengi wanayafuata mafundisho hayo na mara zote hutumbukia katika matatizo ya kutisha. Kwa hiyo waandishi hawa wanabuni kasoro ili waweze kuzielezea ni kwa nini misiba hiyo! Kwa hiyo, hata mwandishi niliyemtaja hapo juu, anaelezea kwamba “kwa kawaida” wakristo huwa ndani ya Kristo Yesu, Kolosai 3: 3, lakini kama tutajihusisha katika aina yoyote ile ya mapambano ya kiroho, basi hapo tutakuwa tumejiweka wazi kama shabaha kwa nguvu za mapepo na tunaweza kudhuriwa na kuharibiwa na mapepo yale!

Anasema kwamba hata kule kuomba tu kwa Mungu kuhusiana na nguvu za mapepo ni mtindo wa mapambano ya kiroho! Inafanana kama mbwa mwitu kuweka kichwa chake nje ya tundu lake la usalama, hiyo inamfanya aonekane ni chambo cha mnyang’anyi anayezurura! Hii ni aina fulani ya udanganyifu ambao unaenezwa na hawa waandishi. Hayo ni mashambulizi juu ya mafunuo ya mandiko kuhusiana usalama wetu na wokovu katika Kristo! Eti mimi? “Kwa kawaida” tupo ndani ya Kristo, isipokuwa tunapojishughulisha na mapambano ya kiroho “hatuwi tena ndani ya Kristo” au “hatuwi kabisa ndani ya Kristo”, isipokuwa tunakuwa tu “sehemu ndani yake?” Eti mimi? Na kwamba eti tunaweza tukawa ni “shabaha” ya roho chafu anayeweza kusababisha uvunjifu wa ndoa, maradhi na kifo ikiwa tutakuwa si waangalifu?! Hii si kitu kingine isipokuwa ni ubatizo katika mambo ya ushirikina na mafundisho ya ulozi. Agano jipya linafundisha kinyume cha hayo yote; yaani inafundisha kuwa ni kwa njia ya kuenenda katika silaha zote za Mungu tu na kupigana vita vizuri vya imani, hapo tunakaa kwa Usalama kutokana na michezo yenye maumivu ya shetani – hivi ni vita vya kweli vya kiroho na vinapaswa kuhusika na mwenendo wetu kiroho – na wala sio katika kupambana dhidi ya roho za uovu katika maombi kama tutakavyoona baadaye katika Efs.6:10 –18.

Maandiko hayafundishi wala kuhamasisha udanganyifu huu; wala hawawezi kuingiza aina hii ya woga ndani ya moyo yetu. Tunaambiwa kuwa “yeye aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye aliye ulimwenguni” na kwamba “hakuna kitu kinachoweza kututenga na upendo wa Mungu uliomo katika Kristo Yesu.” Na hii Inajumlisha mamlaka zote na uwezo! Tumeketi pamoja katika Kristo Yesu mbinguni na Uhai wetu umefichwa katika Kristo ndani yake Mungu” – mambo mengi ni yenye kutia moyo na ahadi zake Mungu akituthibitishia Usalama na baraka zaidi ya kingine chochote kile pale tunapotunza neno lake na kumwamini yeye. Hatusomi chochote kihusucho kushambuliwa na maroho machafu au maisha yetu kuharibiwa kwa sababu tu, tunaomba kama maandiko yanavyo tushauri kuomba. Biblia haikiri aina yoyote ile ya misiba kati ya wale wanaoomba. Au je! Unaweza kupata mausia yoyote ya maombi katika Biblia yanatuonya juu ya uwezekano wowote ule wa misiba. Au Biblia inaelezaea kukumbukia wapi ili kuonyesha kikundi maalum na teule cha Kikristo, ambacho wao pekee waliitwa kwenye vita maalum kwa sababu tu kwamba mapambano hayo ni yenye hatari sana kwa wakristo wa kawaida kuyashiriki?! Hivyo ndivyo wao wanavyofundisha, lakini hii pasipo ugumu wowote ni kuwatumbukiza watu ndani ya nyumba ya matope ya ushirikina na makosa.

Mausia yote ya kuomba katika Agano jipya, ni kwa waamini wote na hakuna hata mausia yanayohusu maonyo kwamba inawezekana ikawa ni “hatari” kuomba, na kwamba aina fulani ya maombi inapaswa kushirikisha aina fulani tu ya waamini wenye wito maalum!

Lakini hii karama maalum ni kitu gani ambacho hawa waombezi wanamaanisha kuwa nazo kulingana na mafundisho hayo? Tunaelezwa kuwa wanapaswa kuwa ni wakristo walio komaa na haswa wawe na karama ya kutambua majina na tabia ya roho za kimaeneo na uwezo wa kusikia toka kwa Mungu, ambaye huwasiliana nao ili kujua ni aina gani ya roho inaweza na inahitajika kufungwa. Karama hizi zinafikiriwa kuwa ni za lazima katika vita vya kiroho. Kwa hiyo waombezi hao wanaweza kutumia masiku na mawiki katika maombi wakiwa na shabaha ya kutambua jina au aina ya roho za kimaeneo zinazotawala juu ya jiji na wanasubiri toka kwa Mungu ili kuwaonyesha ni aina gani ya roho inayostahili kukabiliwa katika maombi yao. Wengine wao wanashuhudia kuwa wanajisikia kuwa wanaingia katika milki nyingine ambako wanakabiliana na roho chafu. Wakati mwingine eti wanaweza kuziona hizi roho chafu labda kama katika maono, au dhahiri. Yanaweza kujitokeza kama kiumbe cha kutisha, nasi tunaambiwa kuwa “mivutano” inaweza wakati mwingine ikawa kwa nguvu. Mchungaji mmoja alivutana ili kutia changamoto roho ya kieneo kuhusu mitaa mingapi katika mji inapaswa kuachiliwa. (Inaonekana kuwa mitaa hiyo ambayo huyo roho mchafu aliiachilia kwa washujaa wa maombi, basi watu katika eneo hilo wangeweza kuitikia Injili, lakini kwa bahati mbaya mitaa ambayo roho mchafu hakuiachilia kwa washujaa wa maombi, watu waliopo pale hawakuweza kuokoka! Au tufikirije?!). Baada ya kufungwa kwa roho za kimaeneo (kama wanavyofikiri), mhubiri huyo anaita mikutano ya Injili akiwaambia watu, eti sasa wamewekwa huru waitikie Injili!

 

Hatari za Mafundisho ya Kisasa – mafundisho yenye makosa, yanayowaongoza watu katika uzoefu udanganyao.

Wanasema kuwa aina hii ya “mapambano ya kiroho” ni muhimu kwa ajili ya mafanikio ya Injili. Pasipo shaka yoyote huo ni udanganyifu. Lakini tena wanatuambia kuwa kutakuwa na “majeruhi” miongoni mwa Wakristo, kwa sababu Wakristo wengi “hawana silaha zifaazo” kwa ajili ya aina hii ya mapambano au hawajafahamu “jinsi ya kupigana” aina hii ya vita! Lakini wazo la kuwa mtu anajishughulisha na vita vya kweli vya kiroho inaweza kumletea matokeo ya roho chafu kukushambulia na kuharibu maisha ya familia yake ni mafundisho yasiyo na maana na yasiyo ya Kibiblia. Hii ni zaidi ya aina fulani ya mafundisho ya ulozi ambayo yanaweza tu kuwaletea watu hofu katika mioyo yao. Hata kama chanzo cha majanga ambayo tunaelewa yanawaangukia wakristo, yanaweza kuwa ni kutokana na kujihusisha kwao na aina hii ya vita vya kiroho ambavyo sio vya Kibiblia, hii ni hoja ya kuijadili kama nilivyokwisha sema. Na sasa ningependa kufanya mambo mawili ya muhimu.

Kwanza, kwa vyovyote vile aina zote za matatizo hutokea katika maisha yetu ikiwa tutakuwa hatuishi kulingana na neno la Mungu. Katika Efeso 4:11-14, Mtume Paulo anaongea kuhusu huduma zitolewazo na Mungu kwa kanisa ili kwamba wote tupate kupokea kukua katika Kristo. Tunapaswa kukua na kuwa wenye nguvu katika ufahamu wa Kristo na tusibaki kama watoto wadogo au kama watu wa mwilini ambao huchukuliwa na kila aina ya upepo wa imani wakitazamia “jambo jipya” linalofuata – ili kutushitusha sisi na hivyo kutufanya shabaha ya hila na udanganyifu wa wanadamu.

Kumewahi kutokea uzao mwingi wenye hatari ya “upepo wa imani” au makosa yenye hatari kwa kadiri ya miaka mingi sasa. Makosa haya yawezekana yanaanzia au yanapata msaada wenye nguvu kutoka kwa waamini wa Amerika. Mafundisho hayo hayana msingi wowote wa neno la Mungu isipokuwa ni matokeo ya kufikiri kwa watu wenyewe na mafunuo ya pekee. Hali kadhalika na uzoefu wao binafsi ambao hauna ulinganifu wa kweli wa kimaandiko. Imani hizo zinahamasishwa na baadhi ya majina yanayo julikana vema, wengi wao ni viongozi wa mashirika yenye nafasi nzuri ya fedha nyingi ambazo ndizo zinazo wasaidia sana kusambaza ujumbe wao. Mengine hupeperushwa na upepo huu wa imani, pasipo hata kufikiria yale ambayo Biblia inasema au kufundisha. Na mradi wanakataa kuongozwa na neno la Mungu, haishangazi kwa hiyo kuona kwamba matendo yao pia huwa ni ya kimwili, Rumi 1:21-24. Ikiwa tutajiondoa kutoka kwenye neno la Mungu ndipo tutakuwa tunajiondoa pia kutoka katika maisha matakatifu yaliyo takasika. Yesu alisema, “watakase kwa kweli.” Yoh 17:17. Maisha ya watu hayajajengwa juu ya mwamba wa Yesu Kristo; juu ya mwamba wa kulitii neno la Mungu. Kwa hiyo si jambo kubwa la kushangaza kuona watu wengi wakipitia katika maisha ya taabu – katika nyakati hizi kunaonekana kuenea kwingi kwa watu kuondoka kutoka katika neno la Mungu ambavyo inaleta matokeo katika hali ya maisha kuwa ni ya kimwili na yasiyo imara kwa wakristo, ikiwafanya watu kuanguka katika aina fulani ya dhambi na shida na kuchomana wao kwa wao na kupitia kwenye huzuni nyingi. Katika mtiririko wa habari hii ni rahisi kwa waandishi hawa kusema kuwa watu wanapambana na matatizo katika maisha yao “kwa sababu” ya kujihusisha kwao katika aina hii ya vita vya kiroho, kwa sababu wapo wengi wenye matatizo tayari, lakini chanzo halisi cha matatizo yao kwa hakika yaweza ikawa ipo sehemu fulani.

Watu hawa hawaingii katika mapambano ya kiroho kabisa, bali wanaingia kwenye ulimwengu wa maroho unaotofautiana kabisa – pale wanapokuwa katika kudanganywa na kutokana na hilo huwajia “Injili nyingine”, “Yesu mwingine” na “roho mwingine”. Wanazitengeneza nguvu za “maroho ya kibinadamu” na kufanyika kuwa ni shabaha ya maroho yadanganyayo, ambayo ndiyo yanayowashawishi kuona kuwa wanajishughulisha na vita vya kiroho na kwamba watu wengi wanaendelea kudanganywa kunyang’anywa ufahamu wa kweli wa Mungu ambao umo ndani ya Kristo. Ndiyo naweza kuhisia kwamba mtu yeyote anayeifuata elimu ya mtindo huu na kuamini huku katika uzoefu unaofanana, lazima watajitumbukiza katika matatizo makubwa. Wanalivunja neno la Mungu, na wanalivunja ndani ya milki isiyo halali.

Inaweza ikatusaidia tukitazama katika 2Kor.11:1-15 ili kutusaidia kuelewa jinsi gani mambo haya yanavyoweza kuwa. (Tafadhali angalia katika makala ya kwanza ambamo hali ya kanisa la wakorintho pamoja na misingi ya udanganyifu wao ilivyoangaliwa). Katika kanisa la Korintho wengi wa watu wa Mungu huko walikuwa wanaenenda kimwili. Walipenda kupata “uwezo na utukufu”. Na hiyo hali ya kimwili pamoja na hayo matamanio ya kimwili ya kupata uwezo na vyeo ili wasababishia kupotelea mbali na mafundisho ya Kristo. Kung’ang’ania  kudumu katika mwenendo na tabia hizo kuliwaletea kuonekana wazi na kuwafanya wawe ni kafara ya udanganyifu wa shetani – ni udanganyifu wa kutisha! Tunaambiwa kuwa shetani mwenyewe hujigeuza katika sura ya “malaika wa nuru”, ule mstari wa 14. Ninaamini kwamba baadhi ya uzoefu wa watu hawa unapaswa ueleweke katika habari hii. Katika mstari wa 13 anaongea kuhusu “mitume wa uongo, wafanyakazi wenye hila, wakijibadilisha wenyewe kuwa mitume wa Kristo”. Katika mstari ule wa 4 anatueleza kwamba hata watu wa Mungu wanaweza kuongozwa na udanganyifu huu katika kumpokea Kristo “mwingine”, roho “mwingine” na Injili “nyingine”. Hatujaelezwa, kuwa mambo yanaweza kuwaje, lakini yanaweza kutokea iwapo mtu analiacha neno la Mungu, hilo limewekwa wazi sana kwetu. Na iwapo hilo liliweza kuwatokea wale ambao mtume Paulo mwenyewe aliwashuhudia na kuokoka ambao pia walikuwa katika hesabu ya kuongozwa na kuangaliwa kwa karibu na mafundisho yake; hivyo tusifikiri kuwa mambo haya basi hayawezekaniki nyakati za leo! Na hiyo ndiyo sababu inayoelekea kuandikwa kwa makala hii, kwa sababu mafundisho hata ya kisasa yanatuletea hila za shetani ili kuzichafua fikira za watakatifu kutokana na unyofu uliomo katika kristo – msitari wa 3. Katika Yeremia 5:30,31, tunakuta kufanana kunako shangaza juu ya yale anayoyasema mtume Paulo kwenye 2 Kor.11:13-20. Manabii wa uongo wakiwadanganya watu wa Mungu, viongozi wao wakiwatawala kwa nguvu, na bado watu wa Mungu wakiyapenda hayo yote! Mungu anaisema juu manabii kwenye Yeremia 14:14, “ndipo Bwana akaniambia, hao manabii wanatabiri uongo kwa jina langu mimi, mimi sikuwatuma, wala sikuwaamuru , wala sikusema nao; wanawapeni unabii wa maono ya uongo na uaguzi na neno la ubatili na hadaa ya mioyo yao“. Mambo kama haya yamewai kutokea na hata leo yanatokea pia.

Ijapokuwa yanawezekana kuwa mambo katika habari hii ambayo si rahisi kueleweka, inaonyesha wazi kuwa mtu yeyote asiye na haki anaweza akawasiliana na ulimwengu wa maroho, lakini umaarufu wake kwa watu wa Mungu ni kuwachafua iwapo angepata nafasi ya kufanya hivyo. Nimenukuu habari hapo juu ili kuonyesha kuwa watu wanaweza kuwasililana kimakosa na maroho, hata wakristo wanaweza kufanya hivyo. Ijapokuwa bila shaka sio habari yote hiyo ambayo inaweza kuwahusu waandishi hawa wa kisasa, bado kwa namna fulani, ninafikiri wameiharifu mipaka halali kama ilivyoonyeshwa katika 2 Kor.11:1-15.

Nilikuwa nasoma kitabu kimoja ambacho kimezungukia kasoro zote nilizo zitazama katika makala hizi tatu. Nilipokuwa nikisoma, niliamini kuwa mwandishi huyo amehalifu na ametumbukia katika udanganyifu. Kisha nikasoma kuwa mwandishi wa kitabu hicho yeye mwenyewe alikuwa analifahamu hilo. Yeye ni mwenye historia ya nyuma ya Kimarekani ya asili, naye anashuhudia kuwa, akiwa kama mkristo, bado mambo ya siri zake za hapo kale (au pengine tungeweza kusema kwamba unajimu au uchawi) ule uwezo wake wa kinajimu alioupata kutokana na desturi au mila za kihindi, ungeweza kujitokeza tena ndani yake na angeweza kufanya mambo yenye fumbo za kiunajimu (akiendesha ndani ya ulimwengu wa roho) ambao kwa uaminifu kabisa anakiri wazi kuwa hiyo haikuwa karama ya Roho Mtakatifu. (Ninaamini kuwa mambo kama hayo yanaweza kutokea na yanatokea siku za leo). Lakini ndipo anaendelea kusema kuwa alimwomba Bwana ili aondoshe na kuangamiza kabisa uwezo huo aliokuwa nao hapo kale. Hilo ni jambo jema. Lakini tena anaendelea kusema kwamba Roho Mtakatifu alishuka chini na kufikia kwenye ujuzi huo wa zamani na akawasafisha ili kuwatumia kwa ukamilifu zaidi! Hilo sio jambo jema! Na kadiri mtu anavyosoma kitabu, mtu huyo anaona kuwa huo ni ushuhuda wa uwezo wake wa mambo yake ya “kiunajimu” ya hapo kale yakimpeleka kwenye udanganyifu wa mambo ya uzoefu wa maroho ya kigeni ambayo hayatokani na Mungu. Wamebuni mafundisho mapya na uzoefu ambao wao wanauita “Baraza la Bwana” ambapo unaitwa mbele ya uwepo wa Bwana kwa ajili ya aina fulani ya mazungumzo. Sio uchaguzi wako. Mwandishi wa kitabu hicho wakati fualni alijisikia “ameitwa” kwenye uwepo wa Mungu pamoja na mtu mwingine, ambako Bwana aliwauliza iwapo Mungu sasa anaweza kuihukumu dunia hii. Na eti kwa sababu ya maombezi yao, ulimwengu uliachiliwa kutokana na hukumu ya dunia nzima kwa wakati ule, hii ni kulingana na watu hawa wawili wote kwa pamoja walivyoona na kuskia katika maono yao! Katika aliamini kuwa yeye mmoja na rafiki zake wanane walikuwa wakiitwa kwenye baraza la Bwana, lakini sasa yeye alishangaa kuona kuwa imekuwaje watu wote tisa waweze kusikia kitu kile kile na kuyaona maono yale yale (yanayofanana) kwa wakati mmoja. Hata hivyo alijisikia kuwa anapaswa “kutii na” wakaondoka pamoja, naye anasimulia jinsi ambavyo wote walivyoona kitu kile kile “katika roho” na kusikia kitu kile kile – sauti na maono ambayo wote kwa pamoja walipata kuyajua! Huo ndio upuuzi wa makutaniko ya mizimu, unajimu na ulozi! Hakuna hata moja kati ya hayo inayotokana na Mungu. Halifanani na chochote katika maandiko ya neno la Mungu. Wamefanya makosa ya nje hatari sana na wamedanganywa vibaya na hali hiyo italeta madhara mabaya. Kwa hakika huu ni “moto wa kigeni”! Yeye anasimulia maono hayo kwa kirefu katika kitabu chake lakini bado ni ya tabia ya kigeni na wala hayaleti sura yoyote ile ya kibiblia au hayana misingi yoyote ile ya Kimungu ndani yake. Ni kutokana na wanaume na wanawake wa jinsi hii ndio wanao leta mafundisho ya aina hii. Kama ilivyo kuwa kule Korintho nyakati za Mtume Paulo, ndivyo inavyotokea nyakati za leo pia. Watu wamejazwa maono yao wenyewe, wakimleta roho mwingine, Yesu mwingine, Injili nyingine. Wao wanaamini, kwa kadiri mnavyojua kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa wakimtumikia Mungu, lakini kwa ujumla kwa huzuni kubwa wamekosea.

Mambo haya yote huwaletea huzuni watu wengi wa leo kadiri wanavyo ona udanganyifu wa aina hii na kuchanganyikiwa kunako sababisha maumivu ya moyo, pamoja na matengano ikiwasababisha watu wa Mungu kukosea na kuwaondoa kutoka katika kweli na kuwaingiza kwenye vifungo Inaonyesha kuwa nyakati hizi shetani anajitahidi kufanya kila awezalo kudanganya ikibidi hata wateule. Je, anatumia njia gani kujaribu kufanikisha jambo hili? Kwa mujibu wa Yesu Kristo. Wakristo wa uongo (hii inamaana kuwa, ni wale wenye upako wa uongo) na watatokea manabii wa uongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu. Ishara, maajabu manabii wa uongo na upako wa uongo ni vitu ambavyo shetani atatafuta kudanganya ikiwezekana hata wateule Mt. 24:24. Ikiwa mtu yeyote anaweza kutoa aina yoyote ya ishara na maajabu, au wanajifanya wenyewe kuwa ni mitume wenye nguvu au manabii, hapo ndipo wengi wa watu wa Mungu huonekana kuwa tayari kupokea mafundisho yoyote yale yanayoambatana nao! Hizo ndizo nyakati tunazoishi.

Kwa hiyo, ikiwa watu wanapata matatizo katika maisha yao, sababu kuu ni kwamba wamechagua kuishi pasipo imani na kutokuwa na utii wa neno la Mungu. Na nyakati za leo ni yote mawili hufanyika; yaani mafundisho ya uongo na uzoefu wa uongo ndiyo yanayowapeleka watu wa Mungu kuwa mbali na kweli na kuishi kwa ile kweli; sio kule kujiingiza katika mapambano ya maandiko kiroho ambako ndiko kunako sababisha matatizo, isipokuwa ni mafundisho yaliyokosewa ya aina hii ya vita vya kiroho, hiyo ndiyo chanzo cha mchanganyiko mkubwa, udanganyifu pamoja na matatizo.

Fungu la Maandiko Wanayoyatumia

Sasa tutaangalia aina ya aya ambazo waandishi hawa hupenda kuzilinganisha ili wapate kuyahalalisha makosa yao. Moja kati ya zile kuu inapatikana katika Efeso 6 na tutaanza kwanza kuitazama sura hii, pamoja na kufikiria kwa kifupi juu ya vita vya kiroho ni nini hasa, kabla hatujaendelea kuangalia katika sura nyinginezo.

 

EFESO 6:10-20

Hii penginepo ni sura ya msingi mkuu na ambayo mara nyingi hunukuriwa vibaya, ambayo hutumiwa kuunga mkono mafundisho yao kuhusu roho zitawalazo katika nchi. Mara nyingi hutumiwa na hawa waandishi wa kisasa ili kuainisha mapambano ya kiroho kuwa yanahusika na kuomba dhidi ya, na kuzifunga mamlaka na uweza ambayo inahusisha na roho zile za kiinchi, hii ni kulingana na tafsiri yao. Kama tunavyoangalia katika sura hiyo tuliyoitaja hapa, tunaona kuwa sura nzima haihusiki na chochote juu ya mambo kama hayo (niliishughulikia kwa makini sura hii pia pale nilipokuwa nafikiria ju ya maombi katika Agano Jipya kwenye makala yangu ya kwanza). Katika mstari wa 10 na wa 11, mtume Paulo anatusihi tuwe hodari katika Bwana tukizivaa silaha zote za Mungu ili tupate kuzipinga hila za shetani. Kwa nini tunahitaji silaha za Mungu? Ni kwa sababu adui yetu ni wa kiroho na kushindana kwetu ni kwa kiroho. Ule mstari wa 12 unatuambia kwamba kushindana kwetu, au vita vyetu sisi, sio juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”, (katika hali hiyo hatuhitaji kufafanua majeshi hayo yote ya kiroho, isipokuwa ni bora kuendelea kufuata hoja za mtume Paulo hapa). Kwa sababu ya hilo, tunahitajika kukamilika kiroho. Peke yetu wenyewe tu, hatuwezi kuushinda upinzani huu wa kiroho na hila! Sasa, baada ya kuliweka hili wazi katika ule mstari wa 12 mtume Paulo anatusihi kufanya nini hapo? Je, yeye anasema kwamba, “kwa kuwa upinzani wetu ni wa kiroho, jichukulieni wenyewe silaha za Mungu ili kwamba unaweza kuomba dhidi ya mamlaka hizi na uweza na kuzifunga kwa jina la Bwana”? Je, hivyo ndivyo mtume Paulo anavyozielewa vita vya kiroho? Je, hii ndiyo njia ya kupata ushindi? Hapana! Hivyo siyo hoja yake kabisa!

Anatuambia katika ule mstari wa 13 kwamba tutwae silaha zote za Mungu, ili tupate kuweza kushindana siku ya uovu na tukisha yatimiza yote kusimama! Mtume Paulo anazungumza kuhusu silaha ambazo zitatuwezesha kuyashinda majaribu na vishawishi mbali mbali ambavyo majeshi ya kiroho ya uovu yanaweza kutuingizia, na hatimaye tuweze kushinda. Anazungumza kuhusu mwenendo wetu kiroho katika Bwana. Hivyo mtume Paulo anatutia moyo kwamba “tupate kusimama”, hiyo ina maana kumpinga shetani na kuyashinda vishawishi vyake katika maisha yetu ya kila siku. Ili kuyafanya hayo tunapaswa kuipata kweli ya Mungu, na kuvaa dirii ya haki (mstari wa 14). Kweli ya Mungu itashughulikia uongo wa shetani na pia itatuadilisha na kututia moyo. Kusimama katika haki tuipatayo katika Kristo kutaitunza mioyo yetu ikiwa imesafishwa na kulindwa. Ushuhuda wa Kristo unapaswa mara zote uwe hai ndani yetu ili kwamba tuwe tumejiandaa kuwashirikisha watu wengine Injili hii (mstari wa 15). Kisha katika ule mstari wa 16 mtume Paulo anatusihi, “zaidi ya yote, tuitwae ngao ya imani ambayo kwa hiyo itatuwezesha kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu”. Anachokiongelea hapa ni kujishughulisha na kukataa malaumu yote, uongo na mashauri ya shetani ambao anatutupia ili kutufanya tumtilie mashaka Mungu pamoja na upendo wake kwetu, ili kutufanya tujisikie wenye kuhukumiwa, tusio na maana; na pweke ili kutufanya tujisikie wasikitivu au tunao jihurumia. Tunapaswa kuyashughulikia hayo yote kwa kuiweka imani yetu na matumaini yetu kwa Mungu na katika yale aliyokwisha yasema. Wote huwa tunashawishiwa na kujaribiwa kama ilivyo katika mstari huu; sote tunajua yanafananaje mambo hayo. Lakini sasa hayo ndiyo mapambano yetu kiroho na tunapaswa kuchukua ngao ya imani na wala tusijiachie wenyewe kudhurika kwa uongo wa shetani na mashauri yake. Ni kweli kuwa katika hali hii wengi wetu huanguka. Hatusimami kama mtume Paulo anavyo tusihi, na hivo tunaupoteza ujasiri wetu, furaha na amani yetu katika Bwana. Tunaishia katika kujisikia kuhukumiwa na tusio na maana, tukishangaa iwapo ni kweli Mungu anatupenda na kutujali. Katika hali ya jinsi hii, kwa kweli hatuwezi kukua katika Bwana na bado kuna upungufu wa matunda juu ya Mungu. Sura hii inapiga moja kwa moja nyumbani katikati ya mwenendo wetu na vita vyetu kiroho.

Ukweli ambao mtume Paulo anauelezea hapa ni wa lazima kwa ajili ya mwenendo wetu kiroho na kimapambano. Ni wa maana na ni dhahiri. Wanakaa katika moyo wa maisha ya kiroho na ya ushindi. Hivyo ndivyo inavyohusika na vita vya kiroho. Sio kuanza kuikunja “mikono ya kiroho” na kupiga kelele na kumkemea shetani na maroho ya nchi. Pasipo maswali yoyote, ni vyepesi zaidi na inaashiria kimwili zaidi mtu kuomba dhidi ya roho mbaya katika maombi ya mikutano, kuliko ilivyo katika maisha ya kila siku katika imani, upendo na utii kwa Mungu kusimama katika silaha za Mungu; hi ya mwishoni inawakilisha vita vya kiroho kulingana na maandiko, lile la kwanza halina lolote!

Mtume Paulo anaendelea katika kutusihi tuchukue chepeo ya wokovu – ambayo itatunza na kulinda akili zetu katika kristo – na upanga wa roho, ambao ni neno la Mungu. Tukiwa tumevaa silaha zote za Mungu, Paulo anatusihi sasa kuomba (mstari wa 18). Haya, je sasa tunatakiwa kuomba dhidi ya mamlaka na uweza na kuzifunga? Sasa, kwa kuwa tumepata silaha za Mungu, tunapaswa kusimama dhidi ya roho zitawalazo maeneo na kufunga uweza wake? Hapana. Sio hivyo, kulingana na mtume Paulo. Lakini Je, hivyo si ndivyo silaha inavyotakiwa kuwa? Kutujaza nguvu katika maombi kuzifunga roho mbaya? Hapana; sio hivyo, kulingana na mtume Paulo. Mtume Paulo hataji kuomba dhidi ya maroho na kuzifunga. Anazungumza kuhusu “kuomba kwa sala zote, na maombi kila wakati katika roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote na kwa ajili yangu mimi…..”

Kwa hiyo kuenenda kiroho, na kuzishinda kwa mafanikio hila za shetani katika vita hivi vya kiroho katika maisha yetu ya kila siku, kunatuwezesha kuomba kwa ufasaha kwa ajili ya watakatifu. Kwa uwazi kabisa maombi ni sehemu muhimu ya mwenendo wetu kiroho mbele za Mungu, lakini tunawezaje kuomba kwa ufasaha pale tunapolitilia shaka pendo la Mungu na matunzo yake kwa ajili yetu, pale tunapojisikia kuhukumiwa watu tusio na maana, au tusiopendwa, pale tunapokuwa na uchungu, kutokusamehe na ugumu mioyoni mwetu; pale tunapokuwa katika kutokuamini! Kwa hiyo tunaweza kuona kuwa, mtume Paulo anatupatia amri sahihi katika sura hii – uhusiano wetu na Mungu, pamoja na mwenendo wetu mbele zake lazima uwe safi kabla hatujaweza kuwa wenye mafanikio kiroho katika maeneo mengine. Kwa hiyo vita vya kiroho vinahusika na kupinga vishawishi vya shetani na uongo wake katika mwenendo wetu wa siku kwa siku na Bwana – tukivaa silaha zote za Mungu. Hilo ndilo linatuwezesha kuomba kama itupasavyo kwa ajili ya watakatifu.

Sura hii yote ya mtume Paulo haiwakilishi mbinu fulani fulani au maagizo ya kuyashambulia na kufunga maroho mabaya kupitia maombi! Kwa urahisi tu anasema kwamba, kwa sababu adui yetu ni wa kiroho, kwa hiyo silaha zetu zinapaswa kuwa za kiroho, katika mapigano yanayotuhusu ili kupinga vishawishi, uongo na mashauri ya kutokuamini ambayo shetani atayapanda ndani ya mioyo yetu na maisha yetu. Kwa kweli, mbali ya mapepo kufukuzwa nje ya mtu mmoja mmoja, haupo mfano hata mmoja katika maandiko unao mwonyesha mtakatifu yeyote moja kwa moja akishambuliana na kuzifunga mamlaka zozote zile, uweza au roho zitawalazo maeneo, katika maombi. Maombi yote katika Biblia yanaelekezwa kwa Mungu.

Katika maombi watu wa Mungu wanakiri na kutukuza Uungu wa matoleo yake na wanatoa haja zao kulingana na mafunuo ya neema ya tabia ya uungu wake. Na maombi yao mengi ni kwa ajili ya watu wa Mungu. Kama inavyoonyeshwa na mtume Paulo katika sura hii.

 

Vita vya Kiroho Kulingana na Maandiko – kwa kifupi.

Hatutakwenda kuangalia kwa undani juu ya somo hili katika makala hii, lakini ningependa kutoa muhtasari wa ukweli huu wa lazima; huku tukifikiria juu ya Efeso sura ya 6.

Hebu tuanze mwanzoni kabisa; katika bustani ya Adeni mambo yote yalikuwa mema, lakini baadaye nyoka alikuja katika bustani. Je, hiyo ilikuwa ni kuvamiwa kwa nchi ya Mungu na mapepo? Je, haya yalikuwa ni mashambulizi ya ghafla na upenyezaji usiotakiwa ili kuharibu kusudi la Mungu? Kibinadamu, tunaweza kufikiri, kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuona shetani kupewa nafasi katika bustani, wakati kila kitu kilikuwa salama na pengine tunashawishiwa kufikiri kuwa Adamu na Hawa wangeweza kufanya maendeleo iwapo kama isingekuwa huo upenyezaji wa shetani. Tunaweza kufikiri ingeweza kuwa ni vema kuitisha mkutano wa maombi na kuanza kumfunga na kumkemea shetani au kumtaka Mungu atumie uwezo wake kumfukuza shetani. Lakini pengine tunaweza kupata ufahamu mzuri zaidi na undani wake juu ya tukio hilo kwa kuyatazama maandiko mengine.

Kama tutaangalia katika kitabu cha kumbukumbu ya torati sura 8:2,3, Ayubu 1:6-12 na Mathayo 4:1, kwa uangalifu na moja baada ya nyingine, tunaona kuwa Mungu aliruhusu watu wake pamoja na mwanae pekee ili aweze kujaribiwa na kushawishiwa kwa kupitia mazingira na kwa mashauri ya shetani. Kusudi la Mungu ni kuona kuwa hakuna mtu hata mmoja awezaye kuumizwa, kuharibiwa au kuanguka katika dhambi bali waweze kupitia katika mazingira hayo yanayowajaribu na kuwapima. Na ilikuwa ni mazingira hayo ambayo ndiyo yangewataka kufanya uchaguzi! Kupitia mambo yote mawili lile linalohusu namna walivyofikiri na lile lihusulo jinsi walivyoweza kufanya. Na ilikuwa ni kupitia uchaguzi huu sahihi, kwa kuchagua kumwamini na kumtii Mungu ndiko kutakako wafanya wakue kiroho katika maumbile na katika kumfahamu Mungu. Majaribu na shida za jinsi hiyo kwa kweli ndizo zilizokuwa ni njia yao ya kukua katika neema na kumfahamu Mungu. Mungu hakuhitaji watu wake waanguke au watende dhambi. Hiyo ni kinyume cha tabia yake! Yeye alipenda kuwaleta katika ufahamu na sura yake yeye mwenyewe, kwa wao kuukataa uovu na kuchagua mema. Mistari inayofuatia inabeba ukweli huu tunao uangalia hapa Rumi 5:3-5; Heb.5:8,9,13,14; Yak.1:2-4; 1Pet.1:6-8.

Kusudi la Mungu la kumturuhusu shetani amjaribu Adamu na Hawa ilikuwa ni kuwawezesha kukua katika neema na haki ya Mungu wao, na katika upendo wao kwa yeye. Na walipokabiliana na mashauri ya shetani jibu la Adamu na Hawa halikuwa ni kuitisha mkutano wa maombi ili kumfukuza shetani nje ya Adeni; isipokuwa ni kuvaa silaha zote za Mungu na kuupinga uongo wa shetani na sio kuyaruhusu mashauri ya shetani yapate sehemu katika mioyo na akili zao! Hili la mwishoni linawakilisha vita vya kiroho; lakini lile lililo tangulia halihusiki na lolote. Kama wangaliweza kulifanya hilo la mwishoni, ndipo shetani  angewaachia Yakobo 4:7. Shetani alipomjia Hawa angepaswa kutumia upanga wa roho dhidi yake shetani kwa sababu alilijua neno la Mungu kwamba watakufa iwapo watakula mti wa ufahamu wa mema na mabaya. Lakini yeye hakuuchukua upanga wa kiroho dhidi ya uwongo wa shetani; hakuchukua ngao ya imani dhidi ya mashauri yake yanayoendelea. Mungu alikuwa ni mwema sana kwa Adamu na Hawa kwa kuwaumbia kila kitu kwa ajili yao naye kuwaumbia kwa mfano wake mwenyewe ili kwamba waweze kuwa na ushirika pamoja naye.

Yule nyoka alipomjia, Hawa angeweza kutumia upanga wa kiroho dhidi yake, kwa vile alilijua neno la Mungu kwamba wangekufa iwapo wangekula tunda lile. Lakini Hawa hakuushika upanga wa Roho wala ngao ya imani juu ya maongo ya Shetani. Alisahau ule wema wa Mungu kwao akiona tunda lile alilolitaka ili kujipendeza. Hivyo shetani anawadanganya na kuwaongoza kuelekea kwenye kiburi. Na hasipo dirii ya haki na chepeo ya wokovu kwa kule kumruhusu mawazo mabaya kuhusu Mungu yaweze kupandwa ndani ya moyo wake na akili zake. Mawazo mabaya ya kutokuamini ambayo shetani aliyapanda ndani ya moyo wake, ilimfanya Mungu aonekane kama ni mtu asiyetujali na kutupenda, kana kwamba anayekataza mambo mazuri yasitupate, kwamba aonekane ni mtu asiyetutakia mema ila mabaya. Mungu alikwisha waambia wasile mti ule kwa ajili ya manufaa yao wao wenyewe na wokovu wao. Yeye alipenda wawe kama yeye alivyo, lakini shetani aliwashauri kuwa Mungu alikuwa anawazuia kula tunda la mti ule, kwa sababu hakupenda mambo mema yawajie. Hakupenda wao wawe kama yeye alivyo! Ni kweli shetani ni baba wa uongo! Anaweza tu kuzungumza uongo, na kusudi lake ni kutokumheshimu Mungu na tabia yake ndani ya mioyo na akili za watu, ili kwamba watu hao wasiweze kuweka imani zao na matumaini yao kwa Mungu. Kwa hakika pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, naye asiyeamini amemfanya Mungu kuwa ni muongo, 1Yoh.5:10. Pasipo imani hatuwezi kuufaidi wokovu wa Mungu pamoja na neema yake ambao tumepewa kupitia Kristo. Jambo hili kwa hakika shetani analijua na hapo ndipo anapopazingatia na kuelekeza shughuli zake, ambayo ni kutufanya sisi tumtilie shaka Mungu!

Shetani huja kupanda hoja na mawazo yasiyo na faida ndani ya mioyo ya watu, ikiwa pamoja na watu wa Mungu. Kwa kutumia mashaauri yake yanayoendelea, yeye hutafuta kuziinua hoja zake hizo kinyume na ufahamu wa Mungu; na kuangamiza ile sura na ufahamu wa Mungu. Mashauri yake hayo yakudanganya yanaendelea kushikilia akili za watu wale wanaoyakubali. Ni “mambo ya juu” yanayopinga maarifa na utukufu wa Mungu, 2 Kor.4:4-5. Katika sura hii, ndani ya waraka wa Wakorinto wa pili, Mtume Paulo anaelezea ukweli unaofanana na ule ulioko katika Efeso 6, yaani, vita vyetu sio vya kimwili, lakini silaha zetu zina nguvu kupitia Mungu, na kuziangusha “kila ngome” za aina hii, hoja za udanganyifu ndani ya akili za watu, ambazo zinapinga ukweli na ufahamu wa Mungu. Sura hii haiwakilishi mbinu ya kuzifunga roho zitawalazo katika maeneo ambazo ziko mahala fulani huko angani, bali inakusudia kuonyesha silaha za ki-Mungu ambazo tunazo pale tunaposhughulika na hoja za udanganyifu za shetani! Ufumbuzi kwa Hawa, haikuwa ni kujaribu kumfunga shetani, isipokuwa ni kupinga na kukataa uwongo wake na ndipo angeweza kumkimbia, Yak. 4:7.

Majaribu ya jinsi hii yanaruhusiwa na Mungu. Kristo alipokuwa anabatizwa, mara moja akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenda nyikani kujaribiwa na shetani, Mt. 4:1. Hayo yalikuwa ni maongozi ya ki-Mungu. Wala haikuwa ni kujipenyeza kwa mapepo! Hiyo ilikuwa ni msingi wa makusudi alioudhamiria Mungu; haikuwa ni ajali ya bahati mbaya ili kuiharibu kazi ya Mungu. Ilikuwa ni kupitia majaribu haya halisi, ndiyo yanayotufanya tuwe imara katika Mungu na kukua kiroho. Tunasoma katika Injili ya Luka kuwa Yesu alienda nyikani akiwa amejaa Roho. Na baadaye alirudi akiwa na nguvu za Roho (Luka 4:1-14), na hilo ndilo kusudi la Mungu kwetu. Lakini sasa Mungu anatutazamia tumchague, kumpenda na kumwamini yeye!  Ikiwa hatuwezi, ndipo majaribu yanafunua udhaifu, kujipendeza kwetu au matendo maovu katika mioyo yetu, Kumb.8:2,3. Sura hii yenye msingi katika kumbukumbu ya Torati inatuonyesha kwamba Mungu anayaruhusu majaribu ili kutufanya tuweze kujifunza kumtumaini yeye kuliko kitu kingine chochote kile. Hata mbele ya mahitaji mengi na masumbufu; neno lake ndilo lipaswalo kuwa la maana zaidi kwetu kuliko baraka zozote za muda zilizo nje. Upendo wetu na imani unapaswa uendelezwe na kutumbukia ndani zaidi nyakati kama hizo – na hivyo haitatusababishia sisi kukua katika maumbile kiroho tu – bali pia itamtukuza Mungu!

Hebu angalia jinsi Yesu anavyomshughulikia shetani pale nyikani. Yesu hakumpigia makelele shetani na kumfunga kwa kujaribu kumfuata yeye! Kwa hakika, yeye ameongozwa katika nyika ili aweze kujaribiwa na shetani. Na shetani mara zote huja na aina hiyo hiyo ya mashauri: “Mungu wako yuko wapi? Je, wewe ni mwana wake hasa? Una njaa na ni muhitaji. Je ni kweli anakujali wewe? Kwa nini hufanyi kitu kingine chochote kile sasa ili kutimiza hitaji lako? Fanya ili kujisaidia wewe mwenyewe! Fanya ili kujipanga mwenyewe. Ikiwa utajifurahisha mwenyewe, tazama utanufaikaje na jinsi gani ambavyo mambo yako yatakuwia rahisi!” Mambo kama hayo ndiyo tabia ya mashauri yake. Lakini Yesu alijibuje? Alijibu kwa upanga wa roho – kwa neno la Mungu. Naye ananukuru katika kumbukumbu la Torati 8:31 Israel wamekuwa wakitembea jangwani kwa miaka 40; na Yesu aliitumia siku moja nyikani kwa ajili ya kila mwaka wa miaka hiyo, akiwa anajaribiwa, kama vile na wao walivyojaribiwa. Lakini Yesu hakuhusika na “mahitaji” yake mwenyewe, wala hakuweza kumpatia muda wowote ule shetani kwa kuyasikiliza mashauri yake – Yesu yeye aliishi kwa neno la Mungu, akimheshimu na kumwabudu Mungu zaidi kuliko lolote lile lingine! Yesu alimpinga shetani na shetani akamwachia kwa muda.

Lakini Israel alishindwa kule jangwani. Wao hawakuishi kulingana na neno la Mungu pale walipokabiliana na shida na mahitaji. Hawakuchukua upanga wa imani bali waliruhusu shetani ajaze mioyo yao na akili zao kwa mashauri ya uongo kumhusu Mungu. Na hivyo mashauri hayo yakajenga ngome katika fikara zao nao wakampinga Mungu na kukufuru tabia yake. Asili ya vita vya kiroho vya shetani ni kuwaelekeza watu waingie katika hali ya akili na moyo ambapo watakuwa wakifikiri kama Israel walivyofikiri. Katika Kumb. 1:27, tunaambiwa kuwa kwa kweli Israel waliamini kuwa Mungu alikuwa amewachukia na kwamba amewaleta jangwani ili kuwaangamiza! Na hivyo ndivyo walivyoweza kufikiri hata baada ya kuona yale maajabu ya Mungu aliyowafanyia huko Misri na katika jangwa! Huo ndio udanganyifu wa dhambi na kutokuamini! Na hizo ndizo mbinu za shetani kutufunga sisi tufikirie mambo mabaya kuhusu Mungu na kuutilia shaka wema wake juu yetu. Ni kwa njia hiyo ndivyo shetani anavyo tafuta kutuleta au kutuweka nje ya neema ya Mungu, wokovu na urithi ambao ametuwekea. Tunaweza kutenda dhambi, lakini ikiwa tutajinyenyekeza wenyewe na kumtumainia Mungu kuutafuta msamaha wake, ndipo atatusamehe kulingana na neno lake. Lakini ikiwa mtu atautilia shaka wema wake na asili yake Mungu, mtu huzo atawezaje kupokea chochote toka kwa Mungu? Tunaelewa kuwa Israel alipoteza kutokana na kutokuamini. Lakini hawakuweza kumlaumu shetani kwa ajili ya hali ya mioyo yao. Mungu alikuwa anawategemea wamwamini na kumtii yeye. Majaribu hayo yaliweza tu kufunua hali ya mioyo yao.

Ni kazi ya shetani kuwapata watu ili waweze kuamini mambo haya, lakini sisi tunahusika kama wana wa Mungu, ikiwa tutajiruhusu kushawishika katika kuamini mambo hayo! Hivyo ndivyo moja ya sababu kuu za kwa nini Paulo anaandika yale anayofanya katika Efeso 6.

Kama ilivyokuwa kwa Hawa katika bustani, na ilivyo kwa Israeli kule jangwani, na ilivyo kuwa kwa Yesu kule nyikani, ndivyo itakavyokuwa kwako wewe na mimi. Shetani hutujia ili kupanda mashaka ndani ya mioyo yetu dhidi ya Mungu. Dhambi hii ya kutoamini inavunja ushirika wetu na Mungu na inatuzuia kupokea mambo mema aliyo tuwekea Mungu, inapofusha mioyo yetu isione kweli na inampa nafasi shetani kutufanya mateka kwa aina zote au mwenendo mbaya. Hivyo tunapaswa kumpinga na kupigana vita vizuri vya imani, ambavyo kwa hiyo tumetunzwa salama na kukua na ambavyo kwa hiyo Mungu anaheshimika!

Mmoja wa wahamasishaji wakuu wa mafundisho hayo ya kisasa anashauri kuwa Yesu alishiriki katika “vita vya kiroho vya kiwango cha mbinu” (strategic – level spiritual warfare) ambapo alijaribiwa nyikani. Anasema kuwa, eti hayo majaribu aliyoyapata Yesu kule nyikani yanawakilisha kiwango cha juu cha mapambano ya kiroho na shetani, ambayo wachache wetu tu au hakuna hata mmoja awezaye kuyapata. Kwa vyovyote vile jambo kama hilo ni uwongo mtupu! Sote huwa tunapitia katika majaribu yanayofanana vile vile kama hayo, ndani ya maisha yetu! Shetani hatokezi kwetu kama aina fulani ya dudu baya lenye mapembe kutushurutisha kufanya makosa. Ingekuwa ni wazi! Tungeweza kuona kupitia mbinu hizo na kushituka! Shetani yeye hutumia hila. Huja katikati ya majaribu na shida; na kujaribu kupanda lile linaloonekana kama la “maana” au “mashauri yenye kusihi” na mawazo katika “akili” zetu. Lakini mashauri yote hayo yanalo lengo moja tu na yanatuongoza kuelekea katika aina moja ya hali ya akili – kutufanya tumtilie mashaka Mungu na tutende kwa kujitegemea! “Yuko wapi sasa Mungu wako? Je, ni kweli anakujali? Kwa nini basi huchagui njia nyepesi?” Haya ndiyo aina ya mawazo ambayo shetani anaweza kuyapandikiza ndani ya akili zetu. Nasi tunaweza kuona kutokana na mistari iliyotajwa hapo juu, kwamba iwapo tutakuwa tunaonyesha haja ya kutaka kutosheleza miili yetu au sisi wenyewe, kuliko kumpenda na kumtii Mungu, ndipo majaribu ya shetani yatatujia. Kwa vyovyote vile shetani hawezi kutujia na kutusimamisha juu ya jengo, wala hataweza kuja na “kutupatia” ulimwengu iwapo tutamwabudu yeye. Mazingira haya maalum kwa hakika ni ya kipekee kabisa kulinganisha na majaribu ya Yesu. Lakini lile ambalo sio la kipekee ni kwamba shetani anatujia na aina ile ile ya majaribu kwetu kila mmoja. Ikiwa shetani hatafanikwa kutupata tumtilie mashaka Mungu, ndipo anajaribu kutupata tutumbukie mbali zaidi katika yale tunayoyaamini ili kwamba tuweze kuwa na kiburi na tuishie katika kumjaribu Mungu – ambayo ndiyo yale ambayo shetani anajaribu kuyafanya kwa vyovyote vile, ili kumtia moyo Yesu aweze kurukia juu ya hekalu, au shetani atajaribu kutia moyo au kuweka katika akili zetu chanzo cha tendo fulani ambalo litatufurahisha, kufanya mambo yawe rahisi kwa ajili yetu, kutupatia faida au litutukuze sisi. Hii ndiyo ilikuwa tabia ya jaribu la mwisho la Yesu. Lakini maandiko yote yanatusihi kujikana wenyewe, kumpinga shetani na tujikabidhi wenyewe kwa Mungu na kuyaweka matumaini yetu kwake. Hivyo ndivyo alivyofanya Yesu, ambaye katika maeneo yote alijaribiwa kama tunavyojaribiwa sisi, (Heb. 4:15), na hivyo ndivyo itupasavyo na sisi kufanya. Hivyo ndivyo tunabyokua kiroho kiroho, na hivyo ndivyo tunavyoweza kuingia katika urithi ambao Mungu ameutayarisha kwa ajili yetu katika Kristo.

Tabia halisi ya vita vya kiroho kama ilivyo kuwa kwa Adamu na Hawa, kama ilivyo kuwa kwa Israel kule jangwani, kama ilivyo kuwa kwa Yesu kule nyikani na kama ilivyo kwako wewe na mimi, inatupasa kupinga na kukataa mashauri yote ya aina hii ili kusudi yasipate nafasi katika mioyo yetu. Na tunapaswa kufanya hivyo hasa tuwapo katikati ya majaribu, wakati wa shida na maumivu, tukiwa na juhudi katika imani ya Mungu pamoja na wema wake ambayo inalikumbatia neno lake. Na katika hili agano jipya sasa tumepewa nguvu ya kumpinga na kumshinda yule adui kwa roho na ule uzima wa Kristo uliomo ndani yetu.

Nimewahi kuhudhuria katika makanisa ambayo tumeweza kuomba dhidi ya shetani na kuzifunga roho chafu. Wakati fulani mtu mwingine angeweza kuomba, angeweza kumfunga shetani na kumtupa katika bahari au shimoni! Ninakiri ya kuwa niliweza kushangaa niliona ni jinsi gani shetani alivyoweza kutoka huko alikotupiwa baada ya kuwa tulikwisha “mfunga” katika mikutano ya maombi yetu! Nilijiuliza iwapo yale tuliyokuwa tukiyafanya yalikuwa ni mambo ya kiroho au la, na iwapo ilikuwa na ufanisi wa kweli mbali ya kutufanya sisi “tujisikie vizuri”. Na ilitufanya sisi tujisikie vizuri na “wenye ushindi” kule kupandisha sauti zetu na kupiga kelele na kuzifunga roho chafu – kwa vyovyote vile kulikuwa upande wa washindi! Ninaamini kuwa shetani na roho chafu na kwamba wapo kazini kupinga kazi ya Mungu ndani na kati ya watu, lakini kwa uaminifu kabisa siwezi kusema kuwa kwa kelele katika mikutano ya maombi yetu ambayo inakazia juu ya shetani na kuomba moja kwa moja dhidi yake, kuwa inaweza kuwa na ufanisi wowote ule wa kweli. Hapa sisemi kuwa haitupasi kuomba juu ya mazingira ambayo yanaonyesha kuwa shetani anaingilia, au haitupasi kupiga kelele katika maombi. Sisemi hivyo. Napenda tu kuwatia moiyo watu wa Bwana katika maombi, lakini iwapo tutaangalia katika maandiko kwa uaminifu, hatuwezi kupata kuiona aina hii ya uombaji kuwa ndio njia ya kumshinda adui.

Niliwahi kujihusisha na aina hii ya maombi hapo zamani, na bado sijabadili kuamini kwangu juu ya Mungu au shetani, lakini ninatakiwa kukabiliana na yale ambayo kwa kweli maandiko yanaonyesha na kufundisha, kuhusiana na kuomba pamoja na vita vya kiroho. Vile vile nilipaswa kukabiliana na ukweli kwamba, mbali ya kutufanya tujisikie wazuri, hatukuweza kwa hakika kuelewa au kusikia ushahidi wowote kwamba kumfunga shetani kwetu au roho chafu kuliweza kuleta ufanisi wowote ule. Katika hayo yote kuhusika kwangu ni kwamba tunajaribiwa na Ibilisi mwenyewe kutuingiza katika kiburi. Mbinu moja wapo ya shetani, pale aliposhindwa kumpata Yesu ili ajifurahishe mwenyewe na kuyabadili mawe yawe mkate, ilikuwa ni kumshawishi Yesu zaidi ya njia nyingine. Kwa kuwa Yesu alikuwa akiishi kwa neno la Mungu, shetani angejaribu kutumia hilo ili kumpeleka Yesu katika kiburi. Shetani alimpandisha Yesu juu ya hekalu, akanukuu maandiko kutoka katika kitabu cha Zaburi kuhusu malaika wakimwangalia Yesu ili kwamba asiweze kudhurika. Na tena akasema ikiwa yeye ni mwana wa Mungu basi ajidhihirishe kwa kuruka kutoka juu ya hekalu! Yesu hakufanya hivyo, akanukuu maandiko “usimjaribu bwana Mungu wako”, Kumb. 6:16. Katika majaribu hayo tunaona kwamba shetani ananukuu maandiko lakini anafanya hivyo ili tu aweze kumpata Yesu ili afanyemambo kipekee pasipo Mungu. Yesu hakuhitaji kufanya mbinu maalum kwa ajili ya shetani ili kuhakikisha kuwa yeye ni mwana wa Mungu.Yesu anaishi tu katika kumtukuza na kumpendeza Baba yake!

Lakini hivyo ndivyo ambavyo shetani atajaribu kututendea kutujaza akili zetu na mambo ya hakika yaliyo na ukweli fulani wa kimaanddiko, lakini yote hayo ni ili kutufanya tuende mbali zaidi na yale ambayo Mungu ametuamuru ili atusababishie maumivu au hasara kwa namna fulani. Hivyo watu wanaweza kufikiri, “sawa, sisi ni wana wa Mungu naye ametupatia uwezo kumshinda shetani! Basi hebu tuombe dhidi yake na kuzifunga nguvu zake!” Lakini mtazamo wa aina hii sio wa kibiblia. Ni majivuno. Na inaenda mbali zaidi ya yale ambayo Mungu ametuagiza kuliko kumshinda shetani, inalenga uangalifu wetu tuutupie kwa shetani na hivyo kutufanya tumtukuze yeye na kumhesabia yeye kuwa ni maarufu na mwenye uwezo kuliko ile aliyonayo kwa hakika au inayompasa! Hii kwa kweli inapora utukufu wa Mungu na uweza wake katikati yetu! Bwana Yesu alisema kuwa – walipo wawili au watatu wamekusanyika pamoja kwa jina langu; yeye atakuwa katikati yao. Hakusema kuwa – pale wawili au watatu wamekusanyika pamoja kwa jina lake, shetani atakuwa hapo na kwa hiyo kanisa litahitajika kuomba na kuzifunga na kukemea roho chafu kutoka katika kusanyiko lao! Lakini ikiwa tutafanya aina hii ya mambo nje ya aina fulani za desturi zetu tulizo nazo, hapo tutakuwa tukidhirisha kutokuamini katika Mungu na katika neno lake na tutakuwa tunamwabudu shetani kwa yale matendo ya ushirikina ambayo tunayaita ni vita vya kiroho! Ninalifahamu kanisa fulani katika mji ninaoishi, ambako mchungaji wa hapo aliwachukua watu ili kuombea jengo lote la kanisa – kuzifukuza roho chafu ambazo alisema ndizo zilizokuwa zinaishi katika jingo lile na zinapinga kazi ya Mungu sehemu hiyo! Jambo hili ni aina ya kutokuamini na ushirikina, tunaweza kutumbukia humo kwa mafundisho haya ya kisasa!

Vita vya kiroho inatuhusisha kusimama huku tukiwa tumeshika silaha ya imani katika Mungu pamoja na neno lake kinyume na uongo wote, mashutumu na majaribu ya shetani. Hiyo ndiyo inayoelezwa katika Efeso 6 yote. Haihusiki na kuvaa aina fulani ya silaha za kiroho ili kwamba tuweze kupigana mieleka moja kwa moja na aina fulani ya roho chafu au ya kieneo, tukipiga kelele na kukemea katika maombi. Kuhusiana na kupiga kelele na kukasirika kwa ajili ya shetani, ambayo imeenea sana kwa baadhi ya watu siku hizi, yapo maandiko fulani ambayo yanatuelekeza vizuri. Tumekwisha kuona tayari jinsi Yesu alivyoweza kumkabili shetani kule Nyikani. Hakuweza kupata joto na kukasirika kuhusiana na Ibiilisi, ampigie makelele kana kwamba hapaswi kuwepo pale. Pengine tunaona kushangazwa jinsi ambavyo Mungu alivyomwelezea yule shetani kule katika sura ya kwanza na ya pili ya kitabu cha Ayubu. Mungu anamruhusu Shetani aseme maneno yake na anaruhusu mabishano yake na matendo yake – lakini tu ni kulingana na kusudi lake mwenyewe. Mungu yu salama na mwenye uhakika katika haki yake ya umilele. Yeye anatawala katika haki, na kila mmoja kule mwishoni atahukumia kwa haki ya Mungu. Yeye pia ni mwenye mamlaka juu ya mambo ya wanadamu na yeye anayemruhusu shetani kuwajaribu watakatifu wake. Mungu hachanganyikiwi kuhusu shetani – hukumu yake ya mwisho ni yenye uhakika. Shetani anatupwa katika ziwa la moto. Mpaka hapo, shetani anachofanya ni kuzunguka huku na kule kama Simba angurumaye, naye anatafuta kunyang’anya, kuua na kuangamiza. Bado anawadanganya watu na kupinga kazi ya Mungu. Kwa wale wanao mwamini Krsito, nguvu za shetani zimevunjwa naye hana uwezo dhidi yao, ingawaje kama tulivyokwisha kuona. Mungu anamruhusu shetani hatua fulani, lakini yote hiyo ni kwa ajili ya kuwajaribu watu wake ili kwamba imani yao ipate kuwa kama dhahabu! Lakini katika mfano wa hapo juu si Kristo hapa duniani wala Mungu kule mbinguni aliyechemka kwa kumkaripia shetani. Amepewa nafasi na fursa kulingana na hekima yake Mungu mwenyewe na mamlaka zake, lakini kazi za shetani pia hukemewa na kuvunjwa pale anapoingilia kazi ya Mungu ya kuokoa roho kama tulivyokwisha kuona katika Matendo ya Mitume. Sasa ni Yuda anayeandika katika Agano Jipya anatupatia neno la kutuonya kuhusiana na jambo hili. Yuda 1:8-10. Hapa anatuambia kuwa hata malaika mkuu Mikaeli hakutoa mashutumu ya kukemea dhid ya shetani. Sisemi hapa kuwa shetani anayo nafasi maalumu na uwezo ambao yatupasa sisi kuogopa. Hapana! Hapana kabisa! Aliye ndani yetu ni mkuu kuliko yeye aliye nje ulimwenguni.

Lakini ninapenda tuone maandiko yanavyotufunulia kuhusiana na jambo hili na yanavyofundisha. Lengo langu katika kusema haya yote ni kuona kuwa, hatumpatii shetani nafasi kubwa na uwezo katika kufikiri kwetu na ndani ya maombi yetu kwa kumhesabia umaarufu ambao hastahili kuwa nao; au kwa kwenda mbali na maandiko kwa kujaribu kupigana naye na kumkemea au kupambana na roho zitawalazo maeneo (roho za kimaeneo) kama zinavyoitwa! Yuda hapa anaongelea kuhusu watu wanaoongea uovu juu ya mambo wasiyo yajua au wasiyoyaelewa. Na hivyo ndivyo sawa sawa na hawa waandishi wa kisasa na walimu wa kisasa wanavyofanya. Bila shaka roho chafu ni ushetani. Lakini sasa hawa waandishi wa kisasa wanaongea mambo kuhusu hao pasipo kuelewa wanasema nini hasa! Wanatutaka tukazie macho yetu kwa shetani na roho chafu, tukiwapatia uwezo na mamlaka juu ya miji ambayo kwa kulingana na maandiko hawanavyo! Kisha wanatutaka tujihusishe katika mapambano binafsi ya kirogho pamoja na maroho hayo na kukemea dhidi yao katika maombi! Mambo hayo yote yanaenda mbali zaidi na maandiko na pia yanaenda mbali zaidi na yale yote ambayo Mungu ametuagiza.

Sipendi nikupatie kanuni ya jinsi ya kuomba au kutokuomba katika mazingira maalum ambayo utakabiliana nayo mbali ya kuelekeza maandiko halisi na ukweli wa kiroho ambao unapaswa kutulinda katika kuomba kwetu. Pia sisemi kwamba hatuwezi kupiga kelele au kuomba kwa sauti kuu inapohatijika tunapofanya maombezi – inategemea na aina ya maombi. Ninaloandika ninaliandika juu ya kujaribiwa kwetu tupige kelele kwa hasira dhidi ya Shetani kupita kiasi na bila kujali mafundisho ya Biblia na mfano wa Yesu Kristo. Tunaweza kuhakikishiwa kuwa Kristo aliziangamiza kazi zote za shetani juu ya msalaba na kuharibu mamlaka na uweza pale msalabani. Hii inaweza kutufariji tunapoomba kwa Mungu kuhusu mazingira ambayo tunaamini kuwa shetani anapinga kazi ya Mungu, lakini pasipo kujishughulisha na mambo hayo yao yasiyo ya kibiblia ambayo yanahamasishwa na waandishi hawa wa kisasa!

Nimewahi kuwasikia, watu wakisema miaka mingi sasa, “namchukia shetani” hasa kama mtu ametenda dhambi vibaya au ameumia vibaya. Haya, haikusaidia chochote kumchukia shetani kwa ujumla haitoshi na wala sio hoja yenyewe. Hoja hapa ni kwamba iwapo mtu atajikana mwenyewe na kumpenda pamoja na kumtii Mungu. Ile kinachoweza kutusaidia zaidi katika maisha yetu kiroho ni iwapo tunazichukia dhambi na kuipenda haki (Heb 1:9), ikiwa tunamwamini na kumtii Mungu. Tunapaswa kumpinga shetani kwa moyo wetu wote na wala tusikubaliane na mashauri yake ya udanganyifu au matoleo yake ya kujaribu watu. Hii ndiyo njia kuelekea kwenye furaha, amani, na haki. Kutoka katika maandiko ningeweza kusema kuwa, ni jambo jema sana kutokujihusisha mwenyewe na hisia zozote zile kuelekea kwa shetani. Yesu kule nyikani hakupenyeza uso wake mbele kwa hasira yenye dharau na kuanza kumkemea shetani, akirusha ngumi yake hewani! Je tunapaswa kufanya hivyo? Lakini tunaona kuwa shetani hakuwa na uwezo wowowte juu yake, na Yesu alirudi toka nyikani akiwa amejaa nguvu za Roho – baada ya kuwa amepinga vishawishi vya shetani. Ikiwa unapenda kuchukia kitu chochte hapa duniani, basi uichukie dhambi na katika hali ya kuwa hupendi kufanya lolote lile navyo. Na kama tunawaona wengine wanatenda dhambi, basi hebu tumwombe Mungu ambaye ni tajiri wa rehema na neema 1Yoh 5:16. Hebu tumfuate Yesu ambaye alipenda haki na akachukia maasi (Ebr.1:9) ambaye alipinga na kukataa vishawishi vya shetani pasipo kukemea juu yake kwa hasira, na ambaye kama kuhani mkuu huchukua majina yetu mara kwa mara kifuani pake mbele za Mungu katika maombi! Kut 28:12, 29, Heb 7:25. Nasi tuzifuate nyayo zake, Efs. 6:18.

Hebu sasa tutazame sura nyinginezo za maandiko ambazo hutumiwa kuunga mkono mafundisho hayo mapya.

Daniel 10

Hii ni sura ya aina yake ambavyo hutupatia kumbukumba za uwepo wa kimalaika ambao kuhusishwa na nchi au ufalme. Hata hivyo katika sura hiyo hamna lolote linaloweza kutufundisha au kutufanya tuamini kwamba watu wa Mungu wanaweza kujihusisha na uombaji dhdi ya nguvu hizo.

Wayahudi walichukuliwa mateka huko Babiloni na Daniel aliumizwa na katika kuhuzunika na kumtafuta Mungu kwa niaba ya watu wake. Wayahudi hawakuchukuliwa mateka kwa sababu ya nguvu za juu zaidi za shetani wala haikuwa nguvu za shetani ambazo ndizo zilizokuwa zikiwashikilia matekani huko.

Waisraeli walitenda dhambi ya mara nyingi kinyume na Mungu, na huo umateka waliowekwa ilikuwa ni hukumu ya Mungu mwenyewe juu yao, lakini ni hukumu ambayo alikwisha waonya mwanzoni. Na Daniel aliyatambua hayo yote. Hasa katika sura ile ya 9 tunamkuta Daniel akiomba kwa Mungu akikiri kuwa umateka huo waliofanyiwa ni hukumu ya Mungu kwa dhambi za Israel . Daniel anaungama dhambi za watu wake, ambazo ndizo zilizosababisha hukumu hiyo, na anatafuta rehema za Mungu kwa ajili ya watu wake. Katika ile sura ya 10 tunamkuta Daniel anahuzunika tena kwa muda wa wiki tatu, ambapo baada ya hapo anatokewa na “malaika”; malaika huyu anamwelezea kuhusiana na mapambano yaliyo tokea kati ya roho za kimalaika mstari ule wa 13,20. Malaika huyu ametumwa ili kujibu maombi ya Daniel lakini sasa alizuiwa na “Mkuu wa Ufalme Uajemi”. Lakini baadaye Mikaeli, mmoja wa malaika wakuu, alikuja kumsaidia. Baadaye angeweza kurudi ili kupigana na mfalme wa Uajemi na kisha mfalme wa Uyunani atakuja. Hapa inaonekana kwamba hayo ni mapambano kati ya roho za kimalaika. Daniel alikuwa hapigani dhidi ya mfalme uajemi au dhidi ya roho za kimataifa! Wala tu hakuwa na ufahamu wowote kuhusiana na mapambano ya hao roho wa kimalaika pale alipokuwa akiomba na wala haikuwa ni sehemu ya mbinu zake kuzifunga roho zozote zile zitawalazo maeneo (roho za kimaeneo)! Hakuna hata mahala pamoja katika maombi yake anapopanga kuzifunga roho chafu kana kwamba zenyewe ndizo zinazo husika na kule kutekwa kwa waisraeli au kana kwamba shetani alikuwa na haki ya kisheria juu ya waisraeli kwa sababu ya dhambi zao! Ilikuwa hafanani wala haina ukweli wowote. Waisraeli walitenda dhambi kinyume na Mungu. Kule kutekwa kwao kulikuwa ni matokeo ya dhambi zao na hiyo ndiyo ilikuwa ni hukumu ya Mungu juu yao. Jawabu la hapo ilikuwa ni kuomba kwa Mungu kwa ajili ya rehema zake. Ilikuwa ni yeye Mungu pekee ndiye angewarejesha watu wake baada ya miaka sabini katika nchi yao. Kama alivyo ahidi Daniel 9:2, na hakuna mamlaka yoyote waka uweza ambao ungeweza kuzuia hilo!

Sura hii kwa ujumla inatuonyesha yale ambayo nilikuwa nikiyaeleza katika ile makala yangu ya kwanza hali kadhalika na hii pia, kwa mfano watu wa Mungu wanapeleka maombi yao kwa Mungu kwa niaba ya watu wake na kwa niaba ya kazi yake kati ya wanaume na wanawake. Maombi ya Daniel yanakazia kwa Mungu pekee juu ya watu wake, juu ya rehema zake na juu ya uvumilivu wake. Maombi yake yanakiri kwamba Mungu ni mtawala wa mambo ya watu! Daniel anajihusisha katika kuomba kwa ajili ya watu wa Mungu! Sura hiyo haitafundishi lolote lile kuhusiana na kuomba dhidi ya roho zitawalazo maeneo (roho za kimaeneo) kwa sababu kwa ujumla hazina nafasi wala hazina nafasi ndani ya maombi ya Daniel au katika maombi mengine yoyote yaliyomo ndani ya Agano la kale. Kile ambacho tunakupata katika sura hiyo ambacho ni mtazamo wa kipekee, ni kwamba kulikuwa na mapambano kati ya majeshi ya kimalaika wenyewe kwa wenyewe, lakini haituonyeshi juu ya Daniel akiomba dhidi ya majeshi hayo ya kimalaika. (Wengine wanaamini kwamba “malaika” yule aliyemjia Daniel alikuwa Bwana Yesu mwenyewe.)

Tunapata tena mtazamo mwingine mdogo katika milki ya kiroho wakati Elisha alipoomba kwa ajili ya mtumishi wake mdogo, pale anapowaona maadui wakiwa wamewazunguka. Elisha anamwambia mtumishi wake kuwa wapo wengi upande wetu kuliko walivyo upande wa adui. Kisha anaomba ili Mungu apate kufungua macho ya mtumishi wake ili kwamba apate kuona. 2Falm.6:16,17. Yule kijana ndipo anauona mlima umefurika farasi na magari ya moto! Na jambo hili lilitukia wakati wa Agano la Kale! Na sasa tunapofikiria juu ya sura hiyo ya Daniel. Tunapaswa kuamini kuwaKalvari haijafanya jambo la tofauti katika milki ya kiroho pale tunapo soma sura kama vile Efeso 1:17-23; 2:6, Yn. 2:15-21?! Lakini sasa hata katika Agano la Kale lenyewe, watakatifu wa Mungu hawakujihusisha na mambo ya kuzifunga roho zitawalazo maeneo, kwa sababu kulikuwa hakuna haja kwao kufanya hivyo! Walijua kuwa Mungu ndiye mtawala na maombi yao yalielekezwa kwake nyakati za majaribu na mapambano. Walikuwa wanajihusisha katika kuomba kwa ajili ya watu wa Mungu. Matumaini yao, upendo na utii kumwelekea Mungu ilikuwa ni yale yanayomtukuza yeye na yale yaliyowapatia usalama ao, mibaraka na ulinzi!

Kitabu cha Ufunuo

Waandishi hao wanafanya makosa yale yale wanapoelekea katika Ufunuo 12. Wanafanya hivyo ili kuthibitisha mawazo yao juu ya mbinu za kiwango cha vita vya kiroho. Kuna mapambano kule mbinguni kati ya Mikael na malaika zake na shetani na malaika zake, na shetani ametupwa inje, mstari wa 7 na 8. Lakini hapa napo kile ambacho tayari tumekwisha kukionyesha ni mapambano kati ya jamii ya kimalaika, na ni ishara ya aya ya aina ya kipekee ya mwana aliyenaswa huko juu mbinguni na kutupwa chini ya mbingu ya shetani. Vyovyote vile viwavyo juu ya tafsiri zetu za sura hiyo yote kwa ujumla. Hakuna lolote pale kwa njia ya mifano na mafundisho ili kuunga mkono mawazo kuwa watakatifu wanapaswa kujihusisha katika kuzifunga roho zitawalazo maeneo. Hayo hayakuwa ni maombi ya mashujaa ambao walimshusha chini shetani toka mbinguni! Kwa kweli waandishi hawa wa kisasa wanapenda kurejea katika kitabu cha Ufunuo kwa ujumla, kwa sababu humo nguvu za uovu zinawakilishwa kwa mtindo wa ishara na picha. Wanasema kuwa uwakilishi huu unakumbukikia mamlaka na uweza na kwa hiyo unathibitisha uwepo wa zile roho zitawalazo maeneo. Lakini hakuna hata moja kati ya hayo yote kuwa ndiyo hoja yenyewe! Tunaamini juu ya uwepo wa mamlaka na uweza, lakini hakuna popote pale ambapo watakatifu walijihusisha na kuzitambua pamoja na kuyafunga majeshi hayo ya uovu – hakuna hata katika kitabu cha Ufunuo.

Kinyume chake, alipokuwa akihutubia katika makanisa ya Smirna na Pergamo, (Ufunuo 2:8-17), Bwana anaongelea kuhusu wale walio katika Sinagogi la shetani, na mahala ambapo shetani anakaa. Lakini Bwana hawasihi watu wake kuomba dhidi ya maroho yatawalayo maeneo kana kwamba yenyewe yanayo uwezo wa zaidi kuzuia yale ambayo Mungu alikuwa anataka kuyafanya. Kinyume chake tunaona hapa, kama ilivyo katika sehemu nyingine za maandiko, kuwa Bwana anatumia au anamruhusu adui kuwa tihani au kuwajaribu watu wake, hata katika kifo. Anajitukuza jina lake kwa kupitia watu wake, kwa kuwaonyesha watu, mapepo na malaika kuwa uzima wake ndani ya watu wake ni wenye ushindi katika mambo yote na kwamba watu wake wanampenda Mungu wao zaidi kuliko chochote kile – hata zaidi ya uzima wenyewe. Lakini anawahakikishia juu ya taji ya uzima na kwamba wasiogope lolote lile ambalo shetani anawatupia. Mungu ni mtawala anaweza kuwaokoa watu kutokana na nguvu za giza na za shetani, kama alivyofanya kule Efeso, naye anaweza kumruhusu shetani kujaribu mabaya yake kwa watu wake Mungu kwa nje, ili kusudi kulitukuza jina lake na kuwafanya watu kuwa kama dhahabu. Kati ya nyaraka kwa makanisa yote saba hakuna hata sehemu moja inayoonyesha kuwa shetani kwa namna fulani anafanikiwa katika hizo kazi za Mungu kwenye miji hiyo. Hapana, kuhusika kwa Bwana ilikuwa ni kuhusu dhambi, hali ya kiroho na mafundisho ya uongo kati ya watu wake mwenyewe tu, ambao ndio aliokuwa anawajibika nao na ambao alikuwa anawasihi wafikie toba.

Yeremia 1:9,10

Hiyo ni sura nyingine ambayo wanapendelea sana kuikumbukia wakiweka kama mfano wa “mbinu za kiwango cha vita vya kiroho”. Wanatueleza kuwa Yeremia alipewa uwezo wa Mungu kuzifunga roho za kimaeneo, kwa vyovyote vile mistari hiyo haina lolote lile la aina hiyo. Katika Amosi 3:7, tunaambiwa kwamba “Bwana Mungu hatafanya lolote lile, bila kuwaunulia watumishi wake manabii siri yake”, na katika mstari wa 5 wa Yeremia sura ya kwanza, tunaambiwa kuwa Mungu amemchagua Yeremia kama nabii. Kwa maneno mengine Mungu angeweza kusema kwa kupitia nabii Yeremia, hukumu zile ambazo yeye Mungu atakwenda kuhakikisha kuwa zinapokea kabla Mungu hajafanya hivyo. Ataweza kutangaza baraza na amri zake kwa kinywa cha Yeremia. Nasi tunao mfano wa karibu katika mstari unaofuatia ambazo Yeremia anaona mafunuo ambayo yanatabiri juu ya hukumu, ambayo Mungu anakwenda kuileta juu ya Yerusalemu kutoka Kaskazini. Hivyo ndiyo maana ya ule mstari wa kumi, mstari huu haurejei kwenye aina yoyote ile ya kuzifunga roho zitawalazo maeneo kwa kupita Yeremia au aina yoyote ile ya vita vya kiroho! Roho hizo za kitaifa zilikuwa hazianzishi mashambulizi juu ya Yerusalemu na kwa hiyo kuleta upinzani wa kazi ya Mungu hapo! Hiyo ilikuwa ni hukumu ya Mungu kwa watu wake. Hakuna sehemu yoyote ambapo Yeremia anatafuta kuzifunga roho zitawalazo maeneo ambazo zinategemewa kuipinga mipango ya Mungu wala hafundishi maombi kama hayo. Kitabu cha Yeremia kwa ujumla kinaonyesha mambo ambayo nimekuwa nikiyasema kwa muda mrefu, kwamba Mungu anahuzunishwa na hali ya moyo na dhambi za watu wake na hii ndiyo tatizo pekee la kweli ambalo limekwisha kutambuliwa. Mbali na maonyo ya tangu mwanzo ya hukumu ya Mungu, huduma ya kiroho ya Yeremia inamhusisha yeye katika kuwasihi watu wa Mungu kutubu na maombolezo kwa niaba yao – Yer.4:1-6; 14:7-9. Hiyo ni mistari miwili michache tu kati ya habari zinazolingana katika Yeremia!

Ezekiel 4:1-3

Katika sura hii, Mungu anamwagiza Ezekiel kuchukua tofali na achore ramani ya Yerusalem juu yake. Kisha ajenge ngome juu yake na kufanya boma juu yake. Sura hii inatuonyesha jinsi Mungu anavyotangaza hukumu yake mwenyewe dhidi ya Yerusalem kupitia maneno na matendo ya ishara ya nabii Ezekiel. Hata hivyo, hii ndiyo sura ambayo hawa waandishi wa kisasa wanapenda kuitumia kukumbushia kama habari ambayo inaunga mkono mafundisho yao kuhusu “uchoraji ramani ya kiroho”! Yaani, anatuambia kuwa mistari hiyo inatuonyesha kuwa tunapaswa kuchunguza na kugundua ni dhambi gani kuu, kukosa haki, na usitawi au uovu wa jamii unaochukua nafasi katika mji huo, hata kurudi nyuma zaidi hata ya miaka 100, na katika maeneo gani ya mji huo mambo hayo yanachukua nafasi zaidi. Kwa maneno mengine tunatakiwa kuchora aina ya “ramani” ya kiroho ya mji wetu au jiji. Eti hiyo, wanasema, itatusaidia kutambua roho za aina mabli mbali zitawalazo maeneo ambazo zinayo “haki ya kisheria na mamlaka” juu ya jiji hilo kwa sababu ya dhambi hizo zilizopita. Wanadai kwamba hapo ndipo sasa tunaweza kwa ufasaha na ufanisi tukaomba dhidi ya roho hizo mbaya pamoja na kizifunga! Hii inafikiriwa kuwakilisha “ujengaji wa boma” ya kiroho katika mji! Hii inaweza vile vile ikahusisha na mambo ya “maombi ya matembezi” kuzunguka maeneo fulani ya mji. Hayo yote yanafikiriwa kuwa yanaweza kuukomboa mji kutokana na haya maroho ya kimaeneo na ndipo tutakapoweza kuhubiri sehemu hiyo kwa mafanikio! Je, huu sio roho ya udanganyifu nyuma ya aina hii ya mafundisho ambayo yanaweza kupotosha maandiko namna hii?! Ezekiel hakujishughulisha na aina yoyote ya mambo kama haya, ya kushughulika na kuzitambua na kuzishambulia roho hizo za kimataifa ili aweze kukomboa Yerusalemu! Ezekiel hakuhitaji kutafuta lolote lile lihusulo roho hizi za kitaifa, na sababu moja kubwa ilikuwa ni kwamba roho hizo zitawalazo maeneo (roho za kimaeneo) halikuwa ni tatizo kwake. Tatizo halikuhitaji uchunguzi wowote! Lilikuwa ni wazi kama vile siku ilivyo wazi! Waisrael walikuwa wametenda dhambi na kuasi dhidi ya Mungu mara nyingi na walihitaji watubu kutoka ndani ya mioyo yao!

Ilikuwa ni Mungu ambaye anasababisha kuzingirwa kwa watu wake, iwe kama hukumu juu yao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao! Na Mungu analitangaza hilo kwa uwazi zaidi kwa watu wake kupitia matendo ya Ishara ya nabii Ezekiel. Ezekiel alikuwa hazifungi roho zitawalazo maeneo ili kwamba wasioamini kule Yerusalemu wangeweza kumrudia Mungu! Yeye alikuwa akitangaza hukumu ya Mungu kwa watu wake mwenyewe, ambayo ilikuwa haitoi mwanya wa kutoroka, iwapo watu wake watakuwa hawajamgeukia yeye kwa mioyo yao yote! Mafundisho hayo yote yahusuyo “kuchora ramani za kiroho” ni yenye kasoro na inaanzisha mashambulizi juu ya injili ya Bwana Yesu Kristo. Mmoja wa waanzilishi wake wakubwa ni George Otis ambaye mafundisho yake tuliyaangalia mapema katika makala zilizopita.

Tunachoweza kuona hapa, tutakipata pia katika sura zote ambazo waandishi hawa wa kisasa huzirejea. Yaani, kwa vile wameshindwa kutupatia hata mfano mmoja tu wa mafundisho yao kutoka katika Biblia; wanajaribu kutumia habari yoyote ile ambayo kwa namna yoyote ile inawarejesha kwenye tukio moja la mafundisho yao na mara moja wanalichukulia maanani kuwa habari hiyo inaunga mkono mafundisho yao yote juu ya “vita vya kiroho”. Kwa hiyo, iwapo kuna mstari wowote unaoturejesha kwenye “mamlaka na uweza” au mstari unaoturejesha” kuzifunga” au mstari wowote unaoongelea kuhusu “kuzishusha chini”, basi mstari huu ndio wanaoutumia ili kuunga mkono mfumo wao mzima wa mafundisho yahusuyo “vita vya kiroho”! Katika kufanya hivyo, wanachafua maana halisi ya mistari ile wanayoitumia. Lakini sasa, tunapoiangalia mistari hiyo wanayoirejea, ndipo tunaona kuwa mistari hiyo inaonyesha tu ukweli ambao nimekuwa nikiuelezea katika makala hii. Yaani kwamba Mungu anahusika na hali ya mioyo ya watu wake pamoja na dhambi, na kwamba ni kupitia maombezi ya watakatifu wake kwa Mungu na kupitia tangazo la neno la Mungu kwa watu wake; kwamba kazi ya Mungu katika kuokoa watu inapaswa kutimilizwa! Vitabu vya Daniel, Ufunuo, na Yeremia wote wanaonyesha hili – hali kadhalika na sehemu nyingine za Biblia.

Mahali palipoinuka

Mungu aliwaambia Waisrael kuzibomoa kabisa mahali pa juu pa ibada za sanamu za mataifa mengine pale watakapo fika ili kuimiliki nchi, (Kumb. 12:2). Lakini hawa waandishi wa kisasa wanasema kuwa mahali pa juu panawakilisha maroho yatawalayo maeneo (roho za kimaeneo) na wanatoa mifano namna ambavyo mataifa na makabila ya kipagani waliamini kwamba miungu yao mbali mbali ilitawala juu ya maeneo maalum. Kwanza, tunaweza kusoma kuwa, haileti tofauti yoyote iwapo mahali pa juu panakumbukia kwa roho zitawalazo maeneo au la; kwa sababu hatuoni sehemu yoyote katika kumbukumbu ya Torati ambayo Mungu anawasihi watu wake kujishughulisha na “vita vya kiroho” na maroho ya aina hii; wala hatuna hata mfano mmoja wa Waisrael wakifanya hivyo. Maana yake hapa ipo wazi kabisa kuwa. Kuabudu sanamu wa mahali pa juu, inawakilisha dhambi dhidi ya Mungu wa asili ya msingi mkuu. Mungu alizuia hilo kwenye amri zake ya kwanza. Na kwa hakika aliwahitaji kuzivunja aina yote ya mahala pa masanamu. Tatizo la msingi halikuwa roho za kimaeneo, bali kule kuwepo na kuabudu kwa mahala pa juu kuliwakilisha dhambi ya waisrael na uasi, dhidi ya Mungu. Tatizo halisi ni katika mioyo ya watu na wala siyo kule angani! Matengenezo yake yalikuwa ni neno la Mungu likiwajia waisrael ili kuwaelekeza kwenye kutubu ambayo kwa vyovyote ingehusisha kuvunjwa kwa maibada ya sanamu ya mahali pa juu na kurejea kwa Mungu kwa mioyo yao yote. Kama nilivyokwisha kusema mahala pengine, pasipo kutubu, kwa vyovyote vile kutampatia shetani uwanja na fursa ya kupotosha mioyo yao zaidi. Lakini sasa jawabu hapa sio kumfunga shetani, isipokuwa ni toba halisi ya watu wa Mungu ambao ndiyo inayomnyang’anya shetani ile fursa ya kufanya kazi katika maisha ya watu! (Mwandishi wa vitabu mmoja anasema kwamba, waisrael wengi waliamini kuwa “nchi ya Mungu” ilikuwa ni Kaanani, na kwamba hii ndiyo inayounga mkono wazo la maroho fulani kutawala juu ya maeneo fulani ya kijiografia! Lakini kama wewe unaijua Biblia na mistari kama hii; Zab. 24:1- “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana”, ndipo sasa nitaacha kwako kutoa maamuzi yako kuhusu hoja hizi!) Sasa, kwa sababu 1 Kor.10:20, ninaamini kuwa watu wale wanaojihusisha katika Ibada za sanamu wanayatumikia mapepo, na kwamba majeshi ya mapepo yapo nyuma ya mambo kama hayo. Na ulimwengu wa Kirumi wa nyakati za mtume Paulo kulikuwepo na kujaa kwa maibada ya jinsi hiyo. Lakini hata hivyo hakuna mahala popote pale ambapo Paulo anawasihi watakatifu kuzitambua na kisha kuzifunga “roho hizi za kitaifa”. Lakini katika hamu yao kubwa ya kuthibitisha kuwepo kwa maroho haya ya kitaifa, waandishi hawa wa kisasa mara nyingi hurejea kwenye kuamini kwa mataifa ya kipagani na makabila yao katika Agano la Kale na kati ya makabila ya siku hizi. Wanasema kuwa watu wapagani hapo kale na nyakati hizi wanaamini kuwa roho mbaya zinatawala juu ya maeneo maalum na kwamba, kwa hiyo tunapaswa kuchukulia maanani mambo haya na kwamba huenda ukawepo ukweli fulani ndani yake. Ni huzuni kuona kuwa wao wanajaribu kupata mkazo mkuu wa mawazo yao ya roho za kimaeneo, kutoka nje ya Biblia; na ni kutoka katika imani za ushirikina za watu wale anaojihusisha na mambo ya uchawi.

Sasa maandiko yanasema wazi kuhusiana na kuwepo kwa mamlaka na uweza, lakini katika Agano Jipya hapajatajwa lolote juu ya roho hizi zitawalazo maeneo. Hata hivyo, ikiwa kuna vitu ambavyo wewe unaweza kuviita ni roho za kimaeneo au hapana hilo siyo jambo ninalohusika nalo katika makala hii. Kuhusika kwangu kukuu, ni kwamba, wapo watu ambao wanawaonya na kuwalazimisha watu wa Mungu ili kujaribu na kutambua majina na tabia ya maroho haya mabaya na kisha kujaribu kujihusisha kukabiliana nazo ana kwa ana na kupigana na maroho ya aina hii. Kufanya hivyo ni kinyume na Biblia na kwa hiyo ni hatari kwa hao wanaoweza kukosea katika hali hiyo! Na kufundisha watu kuwa mbinu za aina hii ni za muhimu kwa ajili ya kuieneza injili ni udanganyifu na mashambulizi kwenye moyo wa Injili.

Hii inawakilisha habari kuu na hoja ambayo wanaitumia kutoka katika Agano la Kale. Kwa hiyo sasa tutakwenda kuangalia namna wanavyoitafsiri misitari katika Agano Jipya.

Mathayo 12:22-30

Sasa ijapokuwa hayapo mafundisho yoyote yale katika sura hii yanayohusu kuzifunga roho zitawalazo maeneo (roho za kimaeneo) ili kwamba kazi ya Mungu ipate kuendelea katika maeneo fulani ya kijiografia, bado hawa walimu wa kisasa wanapenda kurejea kwenye sura hiyo, kwa sababu sura hiyo inaongelea kuhusu “kumfunga mtu mwenye nguvu” ule mstari wa 29. Ni wazi kutokana na sura hii, kuwa yale ambayo Bwana anayaongelea ni kuwatoa mapepo kutoka kwa mtu binafsi. Hivyo ndivyo ilivyo tokea katika ule mstari wa 22 na mafarisayo baadaye wakamshitaki Yesu kwa kutoa mapepo kwa uweza wa shetani, pia hapa inajulikana kama Beelzebuli, lakini yeye Yesu anawathibitishia kuwa hiyo inafanyika kwa kidole cha Mungu kinachomwezesha kuwatoa mapepo. Na ni kutokana na habari hii ndipo anaongea kuhusu kumfunga kwanza mtu mwenye nguvu kabla hajaviteka vitu vyake.

Lakini sasa kadiri tunavyoendelea kuisoma habari hiyo, Bwana anakazia ukweli wake kuwa, hata sio mapepo ambayo ndiyo tatizo kuu, isipokuwa ni kule kutokutubu au ugumu wa moyo wa watu wenyewe. Yesu hakuwa na shida hata kidogo katika kuwafukuza mapepo yatoke kwa watu. Lakini yeye hawalazimishi watu kutubu! Lakini kutokuamini na ugumu wa moyo ndicho kinacho sababisha yeye kushangaa na kutoa machozi, Luka 19:41. Na kaatika ile Luka 13:34,35, Yesu anawaelezea hamu yake ya kutaka kuwakusanya pamoja naye. Lakini hawakutaka na hivyo wameachiwa nyumba yao ukiwa! Anawaambia mafarisayo kuwa ilikuwa ni rahisi kwa waninawi kutubu walipohubiriwa na Yona (kwa hakika hapa hakuweza kuzifunga roho za kimaeneo kwanza!). Lakini sasa mkuu kuliko Yona alikuwepo hapa, yaani Yesu, na bado wayahudi walikataa kutubu, mstari wa 41. Kati ya maswala haya yote, roho za kimaeneo halikuwa ndiyo tatizo lao, lakini kila suala lilikuwa na matokeo yake ya tofauti kwa sababu ya utofauti wa hali ya mioyo ya watu! Lakini tena Bwana anaendelea kuelezea kuwa mara tu roho mchafu amtokapo mtu na anarudi tena na kuiangalia nyumba yake, “Ikiwa tupu, imefagiliwa na kutunzwa vizuri”, ndipo huenda na kuwachukua wenzie pamoja naye na kuja kukaa katika nyumba hiyo na hali ya mtu huyo sasa huwa ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa mwanzo. Kisha Bwana anasema, “hivyo ndivyo itakavyokuwa katika kizazi hiki cha uovu”. Na kama tulivyo kwisha kuona katika sura zilizopita ya Mathayo, Yesu anailaumu miji ambamo amekwisha fanya kazi kubwa – ambayo imehusisha pia na kuwatoa mapepo kwa watu – kwa sababu mbali ya hayo yote waliyoyaona hawakutubu. Yesu alifukuza roho chafu kutoka kwa watu lakini hawakuruhusu maisha yao ya ndani kujazwa na kukaliwa na matunda yapasayo toba. Pengine hii ingeweza kufanya mioyo yao iwe imeandaliwa (nyumba zao) kwa ajili ya Bwana! Lakini badala yake mioyo yao isiyo na toba iliyaacha maisha yao ya ndani kuwa “matupu” na kuandaliwa kuvamiwa hata na mapepo mengi zaidi! Maelekezo tunayoyapata katika sura hii ni kwamba, watu wanaweza wakawa na hamu kubwa sana ya kupokea “mibaraka” ambayo Mungu anaitoa bure, lakini wanaweza kufanya hivyo pasipo hata kutaka kubadili maisha yao! Sura hii inatuonyesha uwezo wa Bwana wa kutoa mapepo kutoka kwa watu, lakini hiyo pia haileti maana yoyote iwapo watu hawatatubu kikweli! Lakini hakuna lolote lile ndani ya sura hiyo linalo wakilisha mafundisho yahusuyo kuzifunga roho ambazo zinadhaniwa kutawala miji.

Mathayo 16:15-20

Kadhalika sura hii inanukuliwa kwa sababu inaonyesha mamlaka ambayo kanisa limepewa “kuzifunga”. Kuzifunga nini? Haya, kwa vyovyote vile hawa walimu wa kisasa wanasema kuwa hii inahusisha pia kuzifunga roho za kimaeneo. Lakini hakuna lolote lile katika sura hii linalotuambia namna hiyo. Hata hivyo, iwapo tutaiangalia ile sura ya 18 mstari wa 15-20, hapo panatupatia habari ambayo inatufanya tuyaelewe maelezo haya ya Yesu, na habari yenyewe hapa ni nidhamu ya kanisa. Wafafanuzi wengine wanaihusisha sura hiyo na ile ya Yohana 20:23, pale ambapo Yesu anawapa uwezo mitume kuzizuia au kuziachilia dhambi za watu wengine. Ukiijumlisha na hiyo, watu wengi wanakiri kwamba kuna umakini mkubwa wa tafsiri ya kigiriki katika Mathayo 16:19 ambayo inasema, “lolote mtakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote mtakaloliachilia duniani litakuwa limeliachiliwa mbinguni.” Hii kwa vyovyote vile ingeweza kuleta maana nzuri inaonyesha kuwa mamlaka ya kanisa imesimamia juu ya utambuzi wa kiroho au ujuzi wa yale yanayokubaliana na utendaji kazi wa mapenzi ya Mungu na haki yake hapa duniani, kuliko usimamizi wa uweza na mamlaka za kanisa kama inavyoona yafaa. Kwa hiyo katika Mtd. 5, hukumu juu ya Anania na Safira halikuwa tu ni suala la Mtume Petro kupitisha hasira yake, lakini kile alichokisema na kukifanya ilikuwa ni dalili ya akili za Mungu mwenyewe katika muda huo; alipo kuwa akifanya kazi kwa uhuru na bila kukoma kupitia kanisa la Mungu – yeye ambaye amepewa zaidi mengi yatahitajika kwake.

Kwa hiyo katika Mt. 18:15-20 Yesu analiweka jambo la kufunga na kuachilia katika habari maalum ya nidhamu ya kanisa. Iwapo Yesu angependa kutufundisha juu ya umuhimu wakufunga na kuachilia uweza wa kiroho kwa ajili ya kueneza injili, angeweza kufanya hivyo katika sura hizo – lakini sasa hakufanya hivyo!

Marko 5:1-19

Wanarejea katika sura hii ili kuonyesha watu kuwa zipo roho zinazohusika katika mikoa kijiografia. Wanaonyesha hilo katika ule mstari wa 10. Pale ambapo mapepo yanamwomba Yesu asiwafukuzie mbali na nchi ile. Hivyo inafikiriwa kuwa roho hiyo ni ya aina ya “roho zitawalazo maeneo”, lakini tunapoangalia katika jambo hilo hilo katika Lk.8:31, tunaona kwamba sababu iliyomfanya pepo huyo amwombe Yesu; sio kwa sababu kuwa walikuwa wanahofia kuwa Yesu atawapeleka katika nchi nyingine, bali ni kwa sababu walikuwa wanaogopa kuwa Yesu angewapeleka kwenye gushimo! ( Tazama pia Rumi 10;7 na Ufunuo 20:3 ). Hata hivyo, mwandishi mmoja mkubwa anaendelea kusema kuwa; eti baada ya wale nguruwe kutumbukizwa katika kifo chao maroho hayo yaliyowakalia walenguruwe yaliwaachilia na kutoka na yakaenda kuwashawishi watu katika mkoa ule wawe kinyume na Yesu – ndio maana kwamba walimwomba Yesu awaachilie mstari ule wa 57. Lakini sasa, tunaona tena katika habari ya Luka tunasoma kuwa, Yesu Kristo aliporudia katika mkoa ule, “watu hao walimpokea kwa furaha!” – Lk.8:40. Je, maroho hayo yalikuwa yamesafiri au labda yamelala usingizi kwamba sasa watu hao walimpokea Yesu kwa furaha?!  Hapana! Mtu huyu aliyeponywa aliwahubiria Yesu kwao! Ilikuwa ni mahubiri ya Kristo ambayo ndiyo yaliyoandaa na kuifungua mioyo yao! Kwa hiyo tena tunaona kuwa sura hiyo hiyo wanayoinukuu siyo tu haithibitishi mafundisho yao isipokuwa kwa kweli inakazia yale ambayo yamesemwa katika makala hii!

Mhamasishaji mmojawapo anayeongoza katika mafundisho hayo ya kisasa, anakiri wazi kuwa kuna sura chache sana katika Agano Jipya ambayo inaweza kutupatia mifano hii ya “”maroho ya kimaeneo”. Kwa kweli, sura hiyo hapo juu ndiyo pekee anayoitegemea katika kutambua kuwa labda pengine ndiyo iwe kwamba ni mfano ulio wazi! Lakini kama vile tulivyokwisha kuona, sasa sura hiyo sio mfano ulio wazi kabisa wa mafundisho yake. Zaidi ya yote, hata kama wangeweza kutupatia mifano ya Agano Jipya juu ya roho hizi za kimaeneo, bado hawajaanza kutuonyesha kwamba maandiko hayo yanafundisha au kutusihi sisi tuombe dhidi yake na kuzifunga roho hizo ili kwamba kazi ya Mungu upate kuendelea! Na ni jambo hili ndilo lipo katikati ya moyo wa mafundisho yao! Na ni jambo hili ndilo tunalolijali kuwa sio la kibiblia na lisilo na afya yoyote. Lakini kwa kuwa hawapati mifano yoyote ile ndani ya Biblia hivyo wanatumia muda wao mwingi katika kujaribu kwa kuthibitisha kuwa roho hizi za kimaeneo zipo!

Pengine hata tungeweza kutaja hapa kuwa, waandishi hawa wa kisasa wanatumia sura hii kushauri kuwa tunapaswa kutafuta majina ya maroho haya ya kimaeneo ili kuweza” kuyafunga”. Ijapokuwa katika sura hii na ndipo sura pekee ambayo Yesu anauliza jina la mapepo hayo, lakini pia haionyeshi kuwa yeye alipenda kuyajua majina yao ili apate kuyafukuza. Katika mashauri mengine yote yaliyomo katika Agano Jipya – roho chafu zinatolewa nje pasipo Yesu au mitume kuomba kujua majina ya mapepo hayo. Na kwa vyovyote haupo ushauri wa mbali katika Biblia ambao tunahitaji au tunapaswa kuugundua majina ya “roho za kimaeneo” kabla ya “kuzifunga roho hizo!”

Matendo ya Mitume 19

Hiyo ni sura nyingine tena ambayo pengine ingeweza kuaminiwa kuwa inaweza kuonyesha kuwa roho za kimaeneo zinaishi na zinapinga kazi ya Injili; ijapokuwa inakubaliwa kuwa bado sura hiyo haiwezi kuthibitisha hilo! Tunaambiwa na waandishi hawa wa kisasa kwamba roho hizo za kitaifa zilizokuwa nyuma ya uungu wa Diana wa Efeso, zilileta upinzani katika kazi ya Mungu kupitia mashambulizi ambayo Demotria mtengenezaji wa vyombo vya vyuma alianzisha. Lakini hakuna lolote kati ya hayo linaloleta maana yoyote. Kupitia mahubiri na huduma aliyoifanya Paulo, miujiza mingi ilikwisha tendeka na umati mkubwa wa watu tayari ulikwisha rejea kwa Bwana, lakini hawa waandishi wa kisasa wanasema kuwa roho za kimaeneo zinazuia hayo yasitokee! Hivyo unatakiwa kuzifunga kwanza kabla watu hawajaanza kugeuza kwa Bwana kwa wingi! Tunachoweza kusema hapa basi ni kuwa haya maroho ya kieneo yalikuwa yamechelewa kiasi, katika kuifanya kazi yao, na hata yale waliyoyafanya, haya kusababisha lolote lile kufuatana na uzuiaji wa Injili – usiku mmoja wa misukosuko ambao ni Demotria pekee na wafuasi wake walipata kukemewa! Ni kweli, wanaposema kuwa sura hii haiwezi kuthibitisha lolote lihusulo kuwepo na kazi ya roho za kimaeneo!

Ninafikiri katika kukata tamaa kutafuta chochote cha kuunga mkono mafundisho yao, ndipo huja na kila aina ya mawazo na ubunifu. Kwa mfano, katika Mtdo.19:20, inasema kuwa neno la Mungu lilizidi na kuongezeka kwa wingi na “lilishinda”. Na mwandishi mmoja anadai kuwa kwa neno la Mungu kushinda, lazima lishinde “juu ya kitu Fulani”, kwa hiyo kitu fulani ndicho kinachopinga kazi ya Mungu. Na “kitu fulani” ni kitu gani? Haya eti ni “roho za kimaeneo” tunaambiwa hivyo! Waandishi hawa wote wanajarbu “kukisia” namna Paulo “labda” alivyojiunga na ndugu wengine kuomba dhidi ya roho za kimaeneo ambazo zilitawala juu ya mji wa Efeso, ili kwamba kazi ya Mungu iweze kufanikiwa katika mji ule! Lakini neno la Mungu halitaji hayo.

Kadhalika mhamasishaji mmoja maarufu wa mafundisho hayo anakumbushia Luka 11:22, mahala ambapo Yesu alitaja “kumshinda” mtu mwenye nguvu. Katika sura inayolingana na hiyo pale katika Marko 3:27 inaonyeshwa kuwa badala ya lile neno la “kumshinda”, Yesu anaongelea kuhusu “kumfunga” mtu mwenye nguvu, hiyo ni nguvu za mapepo. Mwandishi huyo wa vitabu anaendelea tena kutuambia kuwa, maneno hayo ya “kumshinda” na “kumfunga” (ambayo kwayo anamaanisha kuzifunga roho chafu) kwamba yako sawa sawa ili kwamba kila unapoliona neno “kushinda” katika agano Jipya, basi hiyo inaweza kuonyesha kuwa ni kuzifunga roho mbaya roho za kimaeneo! Tunaambiwa pia kuwa Yesu alipokuwa anayaandikia makanisa saba ya Asia na akiwasihi “kushinda”, eti alikuwa anafanya hivyo akiwataka watakatifu kuzifunga roho za kimaeneo kwa mafanikio makubwa! Lakini tunapoangalia katika kile Yesu anachokiongelea kwa makanisa hayo, hakuna lolote lile kwa dhahiri linalounga mkono mawazo hayo yao. Hoja za jinsi hii zinachafua neno la kweli, kwa vile Yesu hapa anaongea kuhusu watakatifu wasimame na kushikilia imani, upendo na utii mbele ya kukabiliana na kila aina ya matatizo na majaribu na vishawishi. “Kushinda” inaonyesha katika mwenendo wetu kiroho na kukua mbele za Mungu, na wala sio kupigana katika maombi dhidi ya roho hizo za kitaifa! Ninasema tena na tena kuwa haya mafundisho ya kisasa yanafanikiwa tu kutunyang’anya ule ukweli.

Kwa njia hiyo hiyo, wao hunukuu Yakobo 4:7 ambako tumeambiwa kuwa tujikabidhi kwa Mungu na tumpinge shetani. Wao wanatafsiri kule kumpinga shetani kuwa kama ni kujumlisha pamoja na kushambulia na kuzifunga roho za kimaeneo jambo ambalo Yakobo hataji chochote kile cha aina hiyo! Hapa Yakobo anaelezea kuhusu mwenendo wa maisha yetu kiroho mbele zake Mungu.

Paulo anatusihi, tusilichafue neno la Mungu wala tusilichukue kwa hila bali tuligawe neno la kweli katika haki. 2Kor.2:17; 4:2; 2Tim 2:15. Mifano niliyotaja hapo juu inashindwa kabisa kutekeleza hayo yote!

Matendo ya Mitume 13:4 – 12

Katika sura hii yule Elina Mchawi anajaribu kumzuia liwali wa nchi ile aliyejulikana kwa jina la Sergio Paulo ili asiweze kuamini. Mtume Paulo anamkemea Eliaa na kumletea upofu juu yake. Hapa sasa tunao mfano wa mtume akitumia mamlaka alizopewa na Bwana ili kushughulika na upinzani huu ulio dhihirika wa kimapepo. Ukiipinga kazi ya Injili (kwa mfano unaofanana na huo katika Mtd. 16:16-18) sasa, baada ya kuwa Paulo amekwisha mshughulikia Elima, yule liwali wa nchi ile akaamini, na hii inapaswa kutuonyesha sisi kuwa pengine na roho hizi zitawalazo maeneo ndizo zinazowashikilia watu wasiweze kuamini. Hata hivyo mwandishi ambaye ndiye anayeijenga hoja hiyo, yeye mwenyewe anakiri kwamba, sura hii kwa kweli haitupatii ushahidi wowote ule au uthibitisho kuonyesha kuwa roho hizi zitwalazo maeneo ndizo zilizohusika na matatizo hayo. Kwa hiyo angalau ameonyesha uaminifu kuhusu hilo. Lakini sasa, waandishi hawa wa kisasa wao hawaelezei kwa nini wao wanayaita matukio hayo kuwa ni mifano ya “mbinu za vita za kiroho” (Hii ni kuwa kinyume na roho hizi za kitaifa au roho zitawalazo maeneo), pale ambapo kulingana na mafundisho yao wao wenyewe, matukio haya yanahusika na kiwango cha chini au kiwango cha vita ya kiroho ya kilozi – hii ni kwamba kushughulika na mtu binafsi na nguvu zao za kiulozi katika lolote like liwalo, hakuna lolote lile ambalo linafundisha au kuonyesha kwetu chochote kile kuhusiana na kuzitambua na kuzifunga roho za kimaeneo.

Hitimisho

Waandishi pamoja na walimu hawa wa kisasa hutumia muda wao msingi wakijaribu kuonyesha kuwa kuna hata mambo haya ya roho zitawalazo maeneo, na labda mbali ya ule mfano mmoja uliomo katika kitabu cha Daniel katika Agano la Kale, hawawezi kuelezea jambo hili zaidi – bila shaka hawawezi kupata kutoka katika Agano Jipya. Hii ndiyo sababu wanarukia imani nyingi za kipagani za kiaguzi ili kusudi waweze kupata ushahidi fulani juu ya elimu yao hiyo. Lakini kama nilivyokwisha kusema, na hata kama wanaweza kuonyesha kuwa roho zitawalazo maeneo zipo, hawawezi kuanza kuthibitisha mwelekeo wao na mafundisho yao juu ya maombi dhidi ya roho hizi pamoja na kuzifunga. Wanashindwa kabisa kutupatia hata mfano mmoja kutoka katika maandiko yote ya watakatifu wakiomba dhidi ya roho hizi za kitaifa au za kimaeneo. Wanashindwa kabisa kuturejesha hata kwenye andiko mojawapo linafundisha kwamba kwa namna fulani kazi ya Mungu imezuiwa katika miji fulani au jiji fulani au nchi, kwa sababu ya roho hizi zitawalazo maeneo na kwamba watakatifu wanahitajika kuomba dhidi yao kabla watu hawajaweza kuamini na kuifanya kazi ya Injili kuendelea.

Mpendwa msomaji, ufuate yale yote yanayofundishwa na maandiko ya neno la Mungu, lakini usilogwe na mafundisho haya ya kisasa kukufanya uende zaidi ya yale yanayofundishwa na Biblia na papo hapo hayaongezei kwenye Injili ya Kristo bali kwa kweli yanaipinga Injili.

© David Stamen 2013

RUDI KWA HOMEPAGE

 

24 responses to “VITA VYA KIROHO : ROHO ZITAWALAZO MAENEO

  1. Ibrahim mwinuka

    May 3, 2015 at 5:03 pm

    Barikiwa

     
  2. Anonymous

    January 22, 2016 at 12:52 pm

    Ndugu yangu mpendwa, dunia inabadika siasa inabadika watu wanabadika , wewe uko tu pale pale?je mzee eli alipokuwa anaishi na samweli husoma kilichotokea?kijana anaitwa wala hajui sauti ya Mungu, kwa kuwa siku hizo mafunuo yalikuwa hakuna,but leo mafunuo yapo mpendwa Mungu anafunuwamambo kwa wale wampendao na kumtafuta kwa bidii jinsi ya kupingana na kupata ushindi…..Mungu akubari.

     
  3. Anonymous

    April 8, 2016 at 1:36 am

    Tatizo ninaloliona hapa ni kujiongeza mtu hataki kujiongeza anataka tu copy and paste hii ni shida

     
  4. Wakujenga

    May 4, 2016 at 4:09 am

    Ukiona unatumia juhudi kubwa kukosoa badala ya kueleza ukweli unaoufahamu kuhusu jambo fulani ujue ni ishara unahitaji kujifunza jambo hilo ili likunufaishe;

    Mwandishi wa makala hii unayo fursa ya kuomba mafunuo ya neno la Mungu kutoka kwa Roho mtakatifu badala ya kupinga walioyapata wengine.

     
  5. ISAYA DAUDI MATARO

    July 15, 2016 at 1:15 am

    Hakika haya mafundisho ni sahihi, sasa kitabu chake nakipataje.

     
  6. Placide

    September 11, 2016 at 2:55 am

    Nafuraisana Namaneno Ya Mungu, Naombatu Kutumiwa Maubiri Nama Vesimingi.

     
    • Mwl.Reuben Mwangulube

      February 10, 2017 at 10:12 am

      wote mliofurahishwa na makala hii ni wale wale mnaopeperushwa na upepo tena wavivu wa kuyachambua maandiko sijui kama hata Biblia Mnaijui.Kwa Jina la Yesu mpate Kufunguliwa Akili zenu Msiwe kama Mwandishwa Makala hii.Mbarikiwe.

       
  7. Anonymous

    September 15, 2016 at 9:23 am

    Mafundisho yako sitasoma tena ..maana unafanana na kiongozi kipofu yaani wewe hujui kama kwenye bibilia kuna maeneo yalikuwa yanatawaliwa na mapepo..pwani ya wageras watu walikuwa hawapiti, Mkuu wa anga la uajemi haukumsoma? Vipi Efeso kule mungu anaeitwa Atemi mpaka watu wanamtetea kuwa yeye ndio mungu mkuu?

     
    • dsta12

      September 15, 2016 at 11:24 am

      Ni wazi, kama nilivyoandika kwenye makala, kuna “falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Hiyo ni wazi. Sijui kama ulisoma makala yangu nzima. Kwenye makakla nilionyesha hamna mstari mmoja katika Biblia unaotuonyesha au kutufundisha ni lazima kufunga au kuomba dhidi ya roho zitawalazo maeneo ili Injili ishinde pale pale. Aidha, hamna mstari mmoja katika Biblia unaotuonyesha au kutufundisha ni lazima kufunga au kuomba dhidi ya roho zitawalazo maeneo – nani aliyefanya hivyo katika Biblia? Hakuna. Naona na hata wewe hukunukuu Biblia kuthibitisha unalodai.

       
      • Brian

        September 23, 2016 at 3:58 am

        Asee Bwana dont fool people ww… Daah. Maana cjui hio elimu umetoa wapi…. Kama hujui kuna hio vita… Mwombe Mungu akufunulie kwa Roho mtakatifu… Usije ukaangamia bure…

         
        • dsta12

          September 23, 2016 at 11:59 am

          How can I fool people? Why haven’t you quoted just one verse which shows us that someone prayed against territorial spirits of any kind? That would settle the question. You haven’t quoted such a verse because there is no such verse in the Bible – not in the Old Testament nor in the New Testament. Jeremiah was called to PROPHESY against the sins of Israel and their idolatry. There is not one verse that says he engaged in prayer against any kind of spiritual principality or power. If you had read my article properly you would have realised this; if you read your Bible you would realise this. Daniel prayed to God concerning God’s work among His people and their return to Jerusalem – nowhere did he pray against spiritual principalities and powers of any kind. That was the angels’s explanation but what he – the angel – was doing. But please, quote us a verse that shows a believer anywhere in the Bible engaging in prayer against any kind of spiritual principality or power.

           
  8. Brian

    September 23, 2016 at 3:54 am

    Naomba niulize… Kwa hilo somo lako… Maana yake Agano la kale lifutwe kabisa….. Maana halina mafundisho ya kufatwa… Vipi wakati Yeremia anaambiwa juu ya kuvunja madhabahu za kipepo… Inakuaje hapo….

     
    • dsta12

      September 23, 2016 at 8:32 am

      Ni jambo la urahisi, Brian. Utupe mstari mmoja tu kutoka Biblia nzima ambao unasema muumini aliomba dhidi ya ‘falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho’ katika mambo yake. Karibu, nukulu tu. Yeremia hakufanya hivyo. Au karibu, nukulu mstari kutoka Yeremia. Yeremia aliagizwa na Mungu kutabiri na kufundisha juu ya dhambi na sanamu ya Israel na kuwaambia waache dhambi na sanamu zao – lakini yeye hakuomba dhidi ya ‘madhabahu za kipepo’ katika maombi yake. Usemi ‘madhabahu za kipepo’ hamna katika kitabu cha Yeremia. Au karibu nukulu tu.

       
      • pastor sadick kinanga

        November 16, 2016 at 6:50 am

        Nadhani unao ufahamu mdogo KIROHO unaongelea jambo ambalo wewe mwenyewe hajui Elisha aliyaponya maji yaliyosababisha mapooza unasoma Biblia gani ndg?

         
  9. nova

    January 24, 2017 at 10:34 am

    Nashukuru kuona mawazo yako ni vyema ufahamu mawazo ya Mungu si kama yetu yako juu sana (Isaya 55:8,9.)na akili yako ikichukua maandiko bila ufahamu Wa Roho Mtakatifu utapata shida Yeremia3:33 neno linasema niitenami……nitakuonnyesha mambo…..na….usiyoyajua. Hivyo Mungu hufunua. Nabii yoeli alitabiri 2:28,29, hivyo kaz ya Roho nikufunua mambo.Yasikusumbue haya Mtume Paulo anasema injili ihubiriwe kwa usahihi ama unafiki haimsumbui anachofurah nikuwa injili inahubiriwa.

     
    • Anonymous

      March 5, 2018 at 10:58 am

      KWELI VOVA UPO VEMA BARIKIWA SANA

       
  10. Mwl.Reuben Mwangulube

    February 9, 2017 at 11:30 am

    Unafahamu Kuwa Kuna Uwezekano Mkubwa Ardhi ya Nchi/maeneo ya Biashara/eneo la kujenga Nyumba Au Ofisi Inaweza Kukabidhiwa Au Kumilikishwa Kwa Mungu Muumbaji Ama Kwa miungu (shetani)? Tusome wote Kitabu cha ( 2 Wafalme 17 : 22 – 27).
    22 Nao wana wa Israeli wakaendelea katika dhambi zote za Yeroboamu alizozifanya; hawakujiepusha nazo; 23 hata BWANA akawaondoa Waisrael wasiwe mbele zake,kama vile alivyosema kwa kinywa cha watumishi wake wote,manabii.Basi Waisraeli walichukuliwa mateka kutoka nchi yao wenyewe,waende nchi ya Ashuru,hata leo. 24 Naye mfale wa Ashuru akaleta watu kutoka Babeli,na Kutha,na Ava,na Hamathi,na Sefarvaimu akawaweka wakae katika miji ya Samaria badala ya wana wa Israeli; wakaumiliki Samaria,wakakaa katika miji yake. 25 Basi ikawa walipoanza kukaa huko,hawakumcha BWANA;kwa hiyo BWANA akapeleka simba kati yao,nao wakawaua baadhi yao, 26 Kwa hiyo wakamwambia m wakasema Wale wa mataifa uliowahamisha,na kuwaweka katika miji ya Samaria ,hawaijui kawaida

     
    • dsta12

      February 9, 2017 at 1:27 pm

      Mistari hii inahusu taifa la Israel wakati wa Agano la Kale. Tafsiri yako inakosa sana na fundisho lile inawaongoza wengi siku hizi kuingia mambo ya ushirikina ambayo hayana msingi katika mafundisho ya Biblia. Ni jambo la rahisi, Reuben, fundisho lako ni wapi katika mafundisho ya Agano Jipya? Toe mstari mmoja katika Agano Jipya tu ambao unathibitisha dai lako.

       
  11. Mwl.Reuben Mwangulube

    February 10, 2017 at 9:42 am

    maeneo ya disco ni roho zipi zinatawala? au maeneo ya vilabu vya pombe za kienyeji ni roho zipi zinatawala? na maeneo ya huduma za injili ni Roho wa namna gani anayetawala? Maana hayo yote ni maeneo.

     
  12. dsta12

    February 10, 2017 at 12:11 pm

    Ni jambo la rahisi, Reuben, fundisho lako ni wapi katika mafundisho ya mitume katika Agano Jipya? Toe mstari mmoja katika Agano Jipya tu ambao unathibitisha dai lako.

     
  13. Anonymous

    February 20, 2017 at 6:12 am

    mshamba wa rohoni wewe

     
  14. Ndikumana Jean Marie

    April 15, 2017 at 6:45 pm

    Jina la bwana lisifiwe sana kwa jinsi Mungu anavyojifunua na kuona pale ambapo tumepoteza.na itaji kupata mafundisho zaidi.asante

     
  15. Anonymous

    June 18, 2017 at 7:18 pm

    kama kweli wewe nimtumishi wa mungu kazi iko hivi kweli unaweza kuihoji biblia kuwa agano la kale halina mashiko nakama halina mashiko injili ingekuwepo muombe mungu akusaidie kujua neno.

     
  16. Anonymous

    July 24, 2018 at 7:06 pm

    hii nayo Kali duh! Mungu atusaidie Sana.

     

Leave a reply to Mwl.Reuben Mwangulube Cancel reply